Maeneo ya Magereza na Majeshi yanaongoza kwa migogoro na Wananchi

Maeneo ya Magereza na Majeshi yanaongoza kwa migogoro na Wananchi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Serikali imesema ni ukweli usiopingika kuwa maeneo mengi yenye magereza pamoja na majeshi yamekuwa na migogoro na wananchi wanaoishi jirani kuhusiana na umiliki wa ardhi.

Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. George Simbachawene amesema hayo bungeni mkoani Dodoma wakati akijibu maswali yaliyoelekezwa kwa Wizara hiyo.

Amesema maeneo ya majeshi yalikuwa mbali na makazi ya watu lakini kadri siku zinavyoendelea yameonekana kuzingirwa na makazi ya watu.

Waziri Simbachawene amesema kwa sasa ni ngumu kuhamisha magereza ambayo yamezingirwa na makazi ya watu kutokana na miundombinu iliyowekwa lakini Serikali inatafakari nini cha kufanya ili kuzuia migogoro ya namna hiyo.

Katika swali la msingi Mbunge wa Jimbo la Urambo Mh. Magreth Sitta alitaka kujua ni lini mgogoro uliopo jimboni kwake kati ya gereza na makazi ya watu utatatuliwa ,mgogoro amba umeanza tangu mwaka 1998.
 
Kuna maeneo yamehodhiwa na majeshi yetu ni makubwa mno hata kuyalinda hawawezi.
 
Back
Top Bottom