Maeneo ya Mikocheni yamejaa wakongwe wanaong'ang'ania ujana

Zurie

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2014
Posts
2,012
Reaction score
5,571
Habari wakuu,

Katika pitapita zangu mitaa ya Mikocheni nikiwa naenda Chuo(ndio mimi mwanafunzi ila msinisakame) nimekutana na wazee wanaong'ang'ania ujana.

Hawa ni wazee wa namna hii:-

1. Babu wa makamo tu ambaye ana vitukuu lakini amevaa pensi, tisheti, cheni ya kilo 3 na pete kadhaa. Pia ni asubuhi tu anaenda dukani lakini kavaa miwani ya jua. Ninachowapendea ni wanatema yai zuri tu akikuona " How are you sweetheart?" au " Hello baby, you good?". Ila umri wao ni umri wa kumrejea muumba na kufanya toba.

2. Bibi mtu mzima ngozi ishajikunja hadi basi (si kwamba nakejeli naelezea tu) lakini alfajiri ana kiskintaiti yuko road anakimbia. Nywele imetiwa piko, mvi 1 ikitokea tu inatiwa rangi nyeusi fasta. Bibi anajipodoa anaweka brazilian hair, wanja wa lulu, heels ili mradi tu kuficha umri wake lakini wenye macho yetu tunawang'amua fasta.

Sasa ninachojiuliza kunani Mikocheni? Maana kwetu Stakishari hakuna mambo haya.
 
Wangapi wamekuomba mbututu?


Kumbe ww bado denti ndio maana msumbufu sn
 
Uzuri wa hivi vizee vinajua kukutunuku...kuna huyo mmoja nilikutana naye News cafe ya masaki nikalisalimia, halikuitikia likanambia mambo! sasa katika story mbili tatu likaniuliza binti unalipwa mshahara sh ngapi ofisini kwenu,nikaliambia laki tano (hapo nadanganya) likasema wow they pay u alot...ebana eh si akanihesabia akanipa hiyo hela ohooo jamani nilihisi kudata hiyo ilikua mda kidogo alafu nilikua nimefulia hahah, hakuwa na papara kibabu gagula cha watu! ila huezi amini tokea siku ile sikuwahi kumtia machoni nilikuja kugundua kana wadhifa huko juu (mdomo koma) chondechonde kibabu ukisoma hii meseji jua ni yule binti yako mpendwa ulimsifia ana akili sana hahahah [HASHTAG]#STAKIPOVU[/HASHTAG]...
 
Waache huko ndio walikojenga hawawezi kuhamia Goba au Kongowe.
 
Hapo number mbili ndiyo kimbilio langu, mademu hawanisomi kabisa kwenye rader zao....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…