Zurie
JF-Expert Member
- Jul 6, 2014
- 2,012
- 5,571
Habari wakuu,
Katika pitapita zangu mitaa ya Mikocheni nikiwa naenda Chuo(ndio mimi mwanafunzi ila msinisakame) nimekutana na wazee wanaong'ang'ania ujana.
Hawa ni wazee wa namna hii:-
1. Babu wa makamo tu ambaye ana vitukuu lakini amevaa pensi, tisheti, cheni ya kilo 3 na pete kadhaa. Pia ni asubuhi tu anaenda dukani lakini kavaa miwani ya jua. Ninachowapendea ni wanatema yai zuri tu akikuona " How are you sweetheart?" au " Hello baby, you good?". Ila umri wao ni umri wa kumrejea muumba na kufanya toba.
2. Bibi mtu mzima ngozi ishajikunja hadi basi (si kwamba nakejeli naelezea tu) lakini alfajiri ana kiskintaiti yuko road anakimbia. Nywele imetiwa piko, mvi 1 ikitokea tu inatiwa rangi nyeusi fasta. Bibi anajipodoa anaweka brazilian hair, wanja wa lulu, heels ili mradi tu kuficha umri wake lakini wenye macho yetu tunawang'amua fasta.
Sasa ninachojiuliza kunani Mikocheni? Maana kwetu Stakishari hakuna mambo haya.