Katibu wa Itikati Mafunzo na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Njombe Josaya Luoga, amesema katika maeneo yote ambayo vyama rafiki havijaweka mgombea zitapigwa kura za ndio au hapana.
Katika kura hizo mgombea anapaswa kufikisha asilimia hamsini au zaidi ya kura za ndio ili aweze kushinda katika nafasi anayogombea.
Aidha amesisitiza iwapo mgombea atapata kura za ndio chini ya asilimia hamsini basi uchaguzi utalazimika kurudiwa katika maeneo hayo.