Maeneo yenye watu washamba kanda ya ziwa

Maeneo yenye watu washamba kanda ya ziwa

Imekua tabia ya mda mrefu sasa kuwachukulia watu kutoka maeneo ya visiwa vya ziwa Victoria kua ni watu washamba wasio jua chochote sana sana kisiwa cha UKEREWE kinaonekana ni kisiwa cha watu washamba sana ila leo ningependa kutoa orodha ya watu muhimu nchini walio tokea ukerewe
  • Piusi Msekwa Amewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola (CPA) kati ya mwaka 1999-2002, pia Mjumbe wa Kamati ya Kurekebisha Sekta ya Sheria kati ya mwaka 1993-1994 na Mjumbe wa Tume ya Rais ya Kuangalia Mfumo wa Vyama vya Siasa nchini kati ya mwaka 1991-1992. Nyadhifa nyingine ambazo amewahi kuzishikilia, ni Uenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi katika Mamlaka ya Maendeleo ya Mitaji kati ya mwaka 1985-2000 na Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi katika Chuo cha Uongozi wa Wanyamapori barani Afrika kati ya mwaka 1985-2000. Vilevile aliwahi kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu kati ya mwaka 1984-1989, Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi katika Chuo cha Ushirika Moshi kati ya mwaka 1984, Mjumbe wa Tume ya Kurekebisha Sheria mwaka 1983 na Mjumbe wa Kamati ya Rais ya Kupunguza Matumizi ya Serikali kati ya mwaka 1982-1983.
  • Mama Getruda Mongella = Gertrude Mongela ameshika nyadhifa mbalimbali za kitaifa na kimataifa. Miaka 1993-1995 alikuwa Katibu Mkuu wa Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Masuala ya Wanawake na kuhudhuria mkutano wake wa nne uliofanyika Beijing, China mwaka 1995. Amewahi kuwa balozi nchini India (1991-1993), Waziri Asiye na Wizara Maalum, Waziri wa Ardhi, Maliasili na Utalii, mshauri maalum wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi, na Utamaduni

Uzi bado unaendelea......

Ni eneo gani jingine watu wana lichukulia poa lakini lina watu muhimu na wenye mambo makubwa ?
Tiririka chini uzi huuu
Kwa kweli ni washamba ....kama mtetezi ndio unakuja na hoja za Msekwa na Mongella ....aseee acheni ushamba mnatudhalilisha Kanda ya ziwa
 
Hakuna kabila lililo bora zaidi ya jingine, kila kabila au ukanda una ushamba wake kiuharisia. Ni sawa na kusema lugha furani ni bora kuliko lugha fulani huo ni ushamba pia.

Wachaga, masai, wasukuma, wahehe, wazaramo, waruguru, wagogo, wanyakyusa nk. Kila mtu anaushamba wake over.
 
Kwa kweli ni washamba ....kama mtetezi ndio unakuja na hoja za Msekwa na Mongella ....aseee acheni ushamba mnatudhalilisha Kanda ya ziwa
Ungeelewa nini thread inamaanisha sizan kama unge comment hiv
Hapo nimezungumzia wilaya ya ukerewe tu sjaizungumzia kanda ya ziwa yote
Hiv ningesema niizungumzie kanda ya ziwa unadhan thread ingekua fupi namna hii
 
Sawa ndugu unataka kunamby butiama wanakaa wachaga na wahehe 🤔🤔??
Bitiama ni Zanaki, Musoma ni mchanganyiko, Wakurya wanatoka Tarime.

Mchaga akikwambia kwao ni Same inaleta maswali mengi ingawa Same IPO mkoa wa Kilimanjaro lakini Same na Mwanga ni upareni, Uchagani ni Moshi, Rombo, Hai na Siha. Umeelewa?
 
Ungeelewa nini thread inamaanisha sizan kama unge comment hiv
Hapo nimezungumzia wilaya ya ukerewe tu sjaizungumzia kanda ya ziwa yote
Hiv ningesema niizungumzie kanda ya ziwa unadhan thread ingekua fupi namna hii
Yaani Wewe Unataka Kuwatosa Wenzio Wa Ukerewe Lakini Ukweli Ndio Huo.

Kanda ya Ziwa Yote Ni Washamba
Niseme tu Pamoja na Wewe[emoji23][emoji23][emoji23]

Moja Ya Tabia Kubwa Kabisa ya Ushamba Ni "Kujimwambafai" Ambayo Tayari Umeidhihirisha.

Fikiria Msekwa Na Mongela Kwa Heshima Zao Ndio Iwe Fimbo Ya Kuwaona Kanda Ya Ziwa Yoote Sio Washamba Hapana.

Hapa Kwa Ushamba Wako Unakusudia Tuwaoneni Woote ni Waheshimiwa [emoji23][emoji23][emoji23]

Sasa Huo Ndio Ushamba Yaani Baba Yako Akiwa Meneja Basi Watoto na wajukuu Wote Mameneja.

Dah Kweli Ushamba Mzigo. Usiwatenge Wenzio Wa Ukerewe Bwana Nyinyi Woote Ni Washamba tu.

Tena Hao Wazee Uliowataja Ni Katika Watu Wachache Sana Wa Kanda Ya Ziwa Ambao Hawajadhihirisha Ushamba Wao Na Ndio Maana Umekimbilia Ukerewe.

Tena Nathubutu Kusema Angalau Ukerewe Kuna Washamba Wachache Sana Kuliko Hayo Maeneo Mengine Ya Kanda Ya Ziwa [emoji23][emoji23]

Tena Haimaanishi Kuwa Ushamba Ni Kutosoma Hapana
Au Kutokuwa Na Cheo Hapana
Au Kutokuwa Na Uwezo Au Kipato Hapana Na Ukifikiria Hivyo Unakosea.

Yaani Mshamba Hata Akisoma Na Wote Mnamjua Huyu Kasoma Atataka Akulingishiie Kuwa Kasoma.
Au Akiwa Na Pesa Na Wewe Unajua Kuwa Ana pesa Atataka Ajigambe Kuwa Anazo Pesa.
Au Awe na Cheo Nawe Unajua Anacho Lakini Atataka Kila Mtu Ajue Yeye Ndio Mtawala Wenu. Nk

Yaani Huo Ndio Ushamba

Kwa Bahati Mbaya Huku Kutaka Sifa Sana Ndio Wakikutana Na Wajanja Wanawasifia Huku Wanawaibia Na Wao Ndio Wanakuwa Mabingwa Wa Kupika Takwimu Yaani Kutengeneza Ushahidi Ili Wasishitukiwe Kuwa Wanaiba.

Mwisho Wa Siku Unakujagundua Nimepigwa Umeshachelewa
Jamani eee Ni Kweli Watani Ni Ndugu Lakini Nyie Washamba Kweli [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
kanda ya ziwa inawashamba na malimbukeni !.
ninaishi nao kanda ya ziwa .mtu hakipata pesa kidogo kijitutumia kujiona wengine wamefili maisha na yeye ndio ana akili kuliko wote.

nazani yale ya mwendazake ilikuwa mfano tosha
Usiwasingizie wasukuma hapa sifa hii wanayo wajita kule anakotoka yule Komandoo waziri wa mambo ya ndani na yule mwanaharakati hawa watu ka kabila kadogoo lakini kila kitu wanajua wabishiiiii kujimwambafai hata mtu akijenga choo akaezeka ni shida mtaani
 
mi nashindwa kuelewa MSHAMBA ni yupi hasa!!!??!!, maana kwangu mimi hata mtu awe msomi sana, awe maarufu sana, awe na madaraka makubwa popote, awe na mapesa mengi mno, isuue ya USHAMBA inaweza kumwangukia tu, hakuna cha mkerewe, mkwere, msukuma, mzaramo, mchaga, unaweza kuwa MSHAMBA tu, kwa sababu ushamba unagusa vionjo vingi sana, kutokana na utaratibu fulani katika sehemu/jamii fulani, kwa wakati huo
 
Imekua tabia ya mda mrefu sasa kuwachukulia watu kutoka maeneo ya visiwa vya ziwa Victoria kua ni watu washamba wasio jua chochote sana sana kisiwa cha UKEREWE kinaonekana ni kisiwa cha watu washamba sana ila leo ningependa kutoa orodha ya watu muhimu nchini walio tokea ukerewe
  • Piusi Msekwa Amewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola (CPA) kati ya mwaka 1999-2002, pia Mjumbe wa Kamati ya Kurekebisha Sekta ya Sheria kati ya mwaka 1993-1994 na Mjumbe wa Tume ya Rais ya Kuangalia Mfumo wa Vyama vya Siasa nchini kati ya mwaka 1991-1992. Nyadhifa nyingine ambazo amewahi kuzishikilia, ni Uenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi katika Mamlaka ya Maendeleo ya Mitaji kati ya mwaka 1985-2000 na Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi katika Chuo cha Uongozi wa Wanyamapori barani Afrika kati ya mwaka 1985-2000. Vilevile aliwahi kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu kati ya mwaka 1984-1989, Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi katika Chuo cha Ushirika Moshi kati ya mwaka 1984, Mjumbe wa Tume ya Kurekebisha Sheria mwaka 1983 na Mjumbe wa Kamati ya Rais ya Kupunguza Matumizi ya Serikali kati ya mwaka 1982-1983.
  • Mama Getruda Mongella = Gertrude Mongela ameshika nyadhifa mbalimbali za kitaifa na kimataifa. Miaka 1993-1995 alikuwa Katibu Mkuu wa Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Masuala ya Wanawake na kuhudhuria mkutano wake wa nne uliofanyika Beijing, China mwaka 1995. Amewahi kuwa balozi nchini India (1991-1993), Waziri Asiye na Wizara Maalum, Waziri wa Ardhi, Maliasili na Utalii, mshauri maalum wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi, na Utamaduni

Uzi bado unaendelea......

Ni eneo gani jingine watu wana lichukulia poa lakini lina watu muhimu na wenye mambo makubwa ?
Tiririka chini uzi huuu
Mshamba mu1 hiv ety watu muhim kuna mtu ambaye siye muhimu kiazi mbatata we😇🤣😅
 
Ushamba ni ushamba tu hata ungekuwa na degree nane still you are a layman
 
Back
Top Bottom