Mafanikio bila mizizi, ni kuteleza kwa kasi

Mafanikio bila mizizi, ni kuteleza kwa kasi

Alloyce PR

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2020
Posts
817
Reaction score
881
"Kijana, unapopata mafanikio, usisahau Baba na Mama yako, waweke karibu na baraka zako. Kama una wadogo zako na uwezo wa kuwasaidia, wavushe kwa kuwajengea msingi wa kujitegemea, si kwa kuwawekea utaratibu wa kukuomba pesa kila mara. Mke/mme uliye naye, mpe heshima anayostahili na yenye hadhi kubwa. Jiepushe na ulimbukeni wa mahusiano. Yoyote akuombaye nafasi ya kujitafutia kipato, msaidie ajiinue endapo unauwezo wakufanya hivyo; akikuomba pesa bila dharura, mpe kazi afanye, kisha mlipe ujira wake. Kwa kufanya hivyo, unajenga kesho yenye mshikamano, maana siku ukikwama, hujui ni nani atakayekuvusha."— Alloyce, P.R.
 
Duniani watu hawapo sawa,tupo makundi makundi,kuna mtu yupo kwaajili ya wengine,yaani always anaamka mapema, anapiga kazi,anachelewa kulala,hajawahi kusaidiwa hata siku moja.

Kuna mwingine ni mvivu yeye ni mtu wa kusaidiwa tu,kuumwa ni yeye,kukaa mahabusu ni yeye,kusaidiwa Kwa kila kitu ni yeye,unakuta ana watoto watano lakini wanaishi Kwa ndugu zake.

Ni kawaida kukuta Boss au mkurugenzi wa kampuni kakonda,hali vizuri na yupo stressed.lakini wafanyakazi wake wanakula good time.
 
Back
Top Bottom