"Kijana, unapopata mafanikio, usisahau Baba na Mama yako, waweke karibu na baraka zako. Kama una wadogo zako na uwezo wa kuwasaidia, wavushe kwa kuwajengea msingi wa kujitegemea, si kwa kuwawekea utaratibu wa kukuomba pesa kila mara. Mke/mme uliye naye, mpe heshima anayostahili na yenye hadhi kubwa. Jiepushe na ulimbukeni wa mahusiano. Yoyote akuombaye nafasi ya kujitafutia kipato, msaidie ajiinue endapo unauwezo wakufanya hivyo; akikuomba pesa bila dharura, mpe kazi afanye, kisha mlipe ujira wake. Kwa kufanya hivyo, unajenga kesho yenye mshikamano, maana siku ukikwama, hujui ni nani atakayekuvusha."— Alloyce, P.R.