Mafanikio katika Maisha-Kila unachokiogopa sana ndio kitakachotokea

Mafanikio katika Maisha-Kila unachokiogopa sana ndio kitakachotokea

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,713
Reaction score
6,121
Habari za wakati huu;

Leo natoka nizungumzie hofu na nafasi yake katika mafanikio.Sitaki kueleza maana ya mafanikio ingawa najua kabisa kwa wengi wetu kuna picha zinakuja kwenye akili zetu ambazo ndio maana ya mafanikio kwetu ila napenda zaidi kuacha hilo eneo ubaki na tafsiri yako hio hio.Ubaki na tafsiri yako hapo ulipo kulingana na mazingira yako na hali yako na hilo litakuwezesha kufika mbali zaidi yakule ninakotaka ufike.

Nataka nisisitize swala moja la muhimu sana."Ukitaka kufanikiwa anza hapo ulipo na hicho ulichonacho"Nasisitiza hili kwa sababu nimegundua kwamba sababu ya mimi kutokufanikiwa ni kutokutaka kuanza nilipo kwa kutumia nilichonacho.Nimepoteza muda mwingi sana,nguvu nyingi sana Pesa nyingi n.k. kwa sababu tu ya kujaribu kukwepa kuanza nilipo kwa kutumia kile nilichonacho.

Unaweza usielewe hili kama nisipoliweka sawa.Nimepoteza Pesa nyingi kulipia kodi za pango za ofisi ambayo sikuitumia,Nimetumia pesa nyingi sana kuajiri wafanyakazi ambao hawakunizalishia,nimepoteza muda mwingi kununua vitendea kazi ambavyo sikuvitumia,nimepoteza muda mwingi sana kufanya mambo ambayo hayakuwa na tija katika mafanikio yangu kwa sababu tu nilikuwa nikijaribu kukwepa kuanzia pale nilipokuwa.

Uwezo wangu haukuhitaji mimi kumiliki ofisi na kuajiri wafanyakazi lakini kwa sababu nilitaka kuanza katika levels fulani tofauti ni level yangu ya kweli basi nilijikuta nikiwekeza rasilimali zangu huko bila kupata faida yoyote ile zaidi ya kujikuta nikienda mbele na kurudi nyuma kila mara.

Nasisitiza sana umuhimu wa kuanza hapo ulipo kwa kutumia ulichonacho bila kujidhili wala kujikweza ili kufikia malengo yako.

Swala la pili na la muhimu ni swala la kushinda HOFU na kuitumia kama ufunguo wamafanikio yake.Ukweli mchungu katika maisha ni kwamba kila unachokiogopa kwamba kitatokea ndio kitakachotokea.Kama hofu yako ni kufilisika kwa hakika utafilisika,kama hofu yako ni kushindwa kwa hakika utashindwa,na kama hofu yake ni kudharauliwa kwa hakika utadharauliwa na kama hofu yako ni kubaki nyuma kwa hakika utabaki nyuma na kama hofu yako ni kofu kwa hakika utakufa.

Ni ukweli mtu kwamba kile unachokiogopa ndicho kitakachotokea katika maisha yako,lakini pia ni habari njema kwamba kila ambacho unataka kitokee mpaka kinakutia hofua pia kitatimia na kuwa kweli.Ukweli huu uko hivi.Wewe unataka kumiliki biashara kubwa ila uwezo wako kwa sasa ni kuanza na genge na kwa hesabu zako ni kwamba genge litakulipa utaweka akiba utafungua biashara kubwa zaidi na maisha yataendelea ila sasa hofu yako kubwa ni kwamba watu wanaokujua wakushangaa na kukucheka,nyanya zitaozea gengeni ndizi zitaoza n.k. basi ukweli ni kwamba hayo yote yatatokea lakini habari njema ni kwamba ukiweza kuya shughulikia hayo basi utafikia lile lengo lako kubwa.


Nasisitiza tena kwamba hofu ya kushindwa inatufanya wengi tuogope kuchukua hatua huku tukisahau kwamba kushindwa kujaribu ni kushindwa kubaya kuliko kujaribu kisha ukashindwa.UKIJARIBU UKASHINDWA UNAPATA UZOEFU,UKISHINDWA KUJARIBU UNAPOTEZA UZOEFU

Niwatie moyo kwamba MAISHA LAZIMA YAENDELEE MPAKA USHINDI UTIMIE
 
Back
Top Bottom