Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndio kina nani hao wachokonozi?We jamaa uko kwenye ile team ya wachokonozi.?
Ingia Youtube search jina hilo.Ndio kina nani hao wachokonozi?
Mie nitakiwa nimefanikiwa nikiweza kucika miaka 80 na bado naweza piga 3some jamani.To whom brain 🧠 is given, Sense is expected.
Kitu au jambo unalodhani na kuona kwamba kwako ni mafanikio makubwa sana, Kwa mwingine bado ni kitu au jambo dogo sana.
Kuna wimbi kubwa sana la Motivational speakers ambao wao hujiona kwamba ndio wana uelewa mpana sana kuhusu suala zima la mafanikio.
Yani hawa motivational speakers hudhani kwamba wao tu ndio wanaelewa kuhusu maisha na mafanikio ya kila binadamu hapa duniani. Wanashindwa kujua na kuelewa kwamba kila mtu ana vipaumbele vyake kuhusu maisha na namna anavyotaka mafanikio yake yawe.
Kuna msemo mmoja wa kimombo unasema "Beauty lies in the eyes of the beholder" kwamba uzuri wa kitu au jambo upo machoni pa mtazamaji, mtu mwenyewe.
Kitu unachokiona kwako ni kizuri sana, kwa mwingine anaweza kukiona cha kawaida au kibaya.
Vivyo hivyo, Linapokuja suala zima la "mafanikio" kila mtu hapa duniani ana namna yake anavyo tafsiri na kila mtu huwa na vipaumbele vyake kuhusu mafanikio ya maisha yake.
Sasa utakuta kuna hawa motivational speakers uchwara ambao hata hawatambui na wala hawaelewi kwamba kila mtu ana vipaumbele vyake kuhusu mafanikio. Wao hukurupuka tu na kuanza kushauri jamii nzima ya watu.
Utawasikia wakisema, Ukitaka kufanikiwa, Mara oh! fanya hivi, fanya hiki, fanya kazi hivi, anzisha biashara hii, acha tabia hii n.k
Watu wengi hufanya Hasty generalization kwenye suala zima la mafanikio. Watu wanatumia maisha yao binafsi, maisha ya mtu fulani au maisha ya jamii fulani ya watu kufanya hitimisho la mafanikio kwa watu wote.
Kwamba ukifuata nyayo za mtu au watu fulani ndio utafanikiwa.
Wanasahau kwamba kila mtu ana vipaumbele vyake kuhusu mustakabali wa mafanikio katika maisha yake.
Kwa mfano, Waafrika wengi hasa watanzania mtu akishajenga nyumba, akanunua gari, akapeleka watoto wake English mediums na kufungua biashara. Basi anaona hayo ndio mafanikio na ndio kamaliza kila kitu maishani. Wengi huona kwamba haya ndio mafanikio.
Na ndio hawa watu kutwa kucha wapo kwenye social media kujifanya wao ndio ma experts wa kushauri jamii nzima kuhusu mafanikio.
Wanasahau kwamba kuna watu mafanikio yao katika maisha sio kujenga nyumba, sio kuzaa, sio kusomesha, sio kufanya biashara, sio kununua gari.
Watu wengi hawajui na hawatambui kwamba kuna watu mafanikio yao hapa duniani ni kuona kwamba wanatatua changamoto zinazoikabili Dunia kwa kuleta majibu chanya. Ambapo kwao majibu hayo, watu hawa ndio huona mafanikio kwao. Kutokana na tafiti zao za kiuvumbuzi.
Watafiti, wanasayansi, wadadisi na wavumbuzi mitazamo yao kuhusu "mafanikio" Ni kuona kwamba wanatatua changamoto zinazoikabili Dunia kwa kuleta majibu, njia na mbinu za ku solve matatizo hayo hapa duniani.
Sasa utakuta kuna mtu amejikakamua akanunua ist 🚗 tena kwa mkopo, Anaanza kujifanya bingwa wa maisha wa kila sekta na kuanza motivations uchwara kuhusu mafanikio kwenye social media.
Kumbe ni ulimbukeni na ushamba unamsumbua...😄
Watu kama kina Albert Einstein, Isaac Newton, Nikola Tesla, Marie Curie, Ernest Rutherford, Michael Faraday, Max Planck, Alessandro Volta, Stephen Hawking, Archimedes, Galileo Galilei pamoja na wanasayansi na watafiti wengine wengi.
Wangekuwa na hizi mentality za kibongo bongo kuhusu mafanikio sidhani kama leo hii kungekuwa na mafanikio makubwa katika nyanja za sayansi na teknolojia.
Tatizo la jamii ya watu wa sasa hasa waafrika ni kudhani kwamba mafanikio ni kumiliki mali na biashara tu.
Wanasahau kwamba kuna watu wana mitazamo tofauti kuhusu mafanikio, Pia kuna watu hawana hata lengo la kumiliki hizo mali na biashara. Na wala sio vipaumbele vyao.
Mafanikio sio kumiliki mali au biashara tu.
Success is subjective.
I'm out.
Yeah mkuu hivi ni vipaumbele vyako katika maisha na ndio mafanikio yako ukitimiza.Mie nitakiwa nimefanikiwa nikiweza kucika miaka 80 na bado naweza piga 3some jamani.
Sitaki magari wala majumba mengi. Mie natala afya njema yakuweza kugegeda basi
Sasa mzabzab tatizo wewe una HIV+ huwezi kuishi hadi 80🤣years miaka 70 mwishoMie nitakiwa nimefanikiwa nikiweza kucika miaka 80 na bado naweza piga 3some jamani.
Sitaki magari wala majumba mengi. Mie natala afya njema yakuweza kugegeda basi
Ata 50 kuiona siweziSasa mzabzab tatizo wewe una HIV+ huwezi kuishi hadi 80🤣years miaka 70 mwisho
Utafika kwa uweza Wa MunguAta 50 kuiona siwezi
Akili ndogo,huwezi kumwelewa mtoa uzi ana akili sanaMafanikio ni kumiliki
According to youPESA, recognition na madaraka ndio kipimo kikubwa zaidi cha mafanikio.
Wafungwa nao wanaona mafanikio ni kuwa na uhuru tu.Mimi nadhani mafanikio makubwa kabisa hapa duniani ni kuwa HAI na AFYA njema.
Kama umewahi kuugua sana ukalazwa hospitali ukiwa hujiwezi, halafu ukawa unaona watu wazima wanapita pita wakiendelea na maisha yao, utanielewa.
Naomba nikupinge,bila ya kua na afya njema mkuu bado wwe hujafanikiwa!!Naomba nikupinge bila kuwa na material thing mkuu bado wewe haujafinikiwa
Akili kisoda huelewa ndani ya box tuAkili ndogo,huwezi kumwelewa mtoa uzi ana akili sana
The so-called Servants of God need to live by their words (to walk the talk) and not just paying a lip service to the Gospel they can't practice..Msitazame matendo yao bali neno wanalowalisha hukumu watapewa na Mungu