Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 10,509
- 16,734
Imeelezwa kuwa mafanikio yaliyopatikana ya hivi karibuni dhidi ya corona covid 19 iliyoitesa dunia kwa zaidi ya mwaka yanweza yote kupotea.
Sababu ya kwanza ni kutokana na watu wengi kulegeza tahadhari dhini ya ugonjwa huo na sababu ya pili ni kutokana na kuwa kile kirusi cha awali kilichopatiwa chanjo zake kimeonekana kubadilika mara kwa mara na kujitokeza kwa sura nyengine maeneo mbali mbali ya dunia.
Hayo yameelezwa hivi karibuni na bwana Rochelle Walensky wa nchini Marekani ambaye ni mtaalamu wa kupambana na maradhi ambukizi.
Amesema baada ya kupungua kwa maambukizi na vifo kuanzia mapema mwaka huu hasa baada ya kutolewa chanjo kwa baadhi ya makundi ya watu, imeonekana kupanda kwa ghafla kwa athari za maradhi hayo kwa asilimia 2 mpaka imerudi tena wastani wa vifo 2000 kwa siku.