😂😂😂 Tindo bana ! Kwa hiyo shida yenu ni uzee na uchakavu wa CCM eenh ? USA: Republicans, Democrats! UK: Labour, Conservatives! Hivi ni vyama vya kizazi kipya Sindio !
CCM: UVCCM
CDM: BAVICHA
Vyama vyote vina evolve with time, most important thing is to ensure with certainty that the country doesn't lose focus on it core ideology ya kuwaletea wananchi maendeleo hata kama itachukua muda mrefu. Tanzania ya 2020 sio ile ya 1961 for sure !
Nchi nyingi za kiafrika zilijaribu kuondoa madarakani serikali za vyama vikongwe eg. Zambia ya Chiluba, Somalia etc only to find themselves engulfed in endless tumoils and social upheaval! So for me I would argue against wholesale condemnation of political party simply because of old age but also agree on the need to modernise such organisations to reflect the current needs and aspirations of their followers.
Julius Malema wa SA amejaribu sana kukizodoa chama chake cha zamani ANC, lakini kwa kiasi kikubwa ameshindwa! Leo taifa hilo likabidhi uongozi kwa EFF si ni balaa kubwa ! The country will be thrown into hell , wiping out all the gains (socio-political) they have made so far though economically bado kuna gaps kubwa.
Kwa hiyo uzee wa chama kwa maoni yangu sio tatizo! Muhimu ni kwenda na wakati kukidhi matarajio ya wengi na si lazima ya wote. Nchi yetu iko ndani ya mfumo wa vyama vingi tangu 1992, lakini mpaka Leo mimi sijaona chama mbadala wa CCM kimfumo, sera, uendeshaji n.k. Chadema ambacho ndio kina aminika kuwa kikubwa zaidi na chenye wafuafi wengi upande wa upinzani hadi leo mfumo wake wa uongozi ni kitendawili kama tulivyo shuhudia sarakasi wakati wa chaguzi zake mwezi jana.
Viongozi wengi wa upinzani ni Mungu watu na wababe, Mbowe, Zitto, Lipumba, Maalim Seif...minyukano ya ndani kwa ndani haiishi ! Nepotism ndio usiseme. So they may purportedly be representing new generation but in fact they are no better than old guard.
Hivyo vyama vya US & UK naona umevitaja kwa bahati mbaya, hivyo vyama vimekuwa vikikaa madarani na kutoka kutokana na kukubalika kwake kwa umma na sio nafasi ya rais ndio inayoamua matokeo ya uchaguzi yaweje.
Kuwepo kwa vijana ndani ya vyama sio kwa sababu ya mifumo bora, bali huo ndio mfumo wa kawaida wa binadamu yoyote, kwani huzeeka na kufa hivyo ni lazima kuwe na hayo makundi. Kwa taarifa yako hata kwa wanyama utaratibu wa vijana upo. So nothing new in here.
Naona umetaja kuhusu kuviondoa vyama umeitaja Zambia na Somalia ili kuupa utetezi wako nguvu. Kama ni kutendeka haki kuhusu kubadili vyama, ni vyema ungeitaja hiyo Zambia na jirani zetu mpaka ndani ya jumuiya ya EA, Kenya. Hebu nipe tofauti yetu ya kisiasa, kiuchumi, kijamii, kielimu, kibiashara katika nchi hizo mbili za mfano na sisi, ili tujue ni hatari kuitoa ccm madarakani. Huenda utajibu hili ili nijue kuwa una jipya.
Kuhusu kuwa eti ccm ndio umeiona iko vizuri kimuundo au kisera nk, hapa ni mambo ya mwamba ngoma. Ukweli ni kuwa chama au mtu yoyote mwenye akili timamu anaweza kuongoza nchi hii. Huyo anayekudanganya kuna mfumo au sera anakudandanganya mchana kweupe. Kwa taarifa yako nchi hii inaongozwa na utashi wa rais aliye madarakani, yaani tabia na utashi binafsi ndio sera na mwelekeo wa nchi hii. Mfano mzuri wa ninachokiongea, nchi hiii imekuwa ikibadilika kila anapoingia rais mpya, sio kwa ajili ya sera bali utashi binafsi wa rais. Ndio maana unaona kwenye katiba yetu inasema Tanzania ni nchi ya ujamaa na kujitegemea, lakini toka hiyo katiba imeendikwa kwa hisia za Nyerere, toka ameondoka madarakani ujamaa haujawahi kutekelezwa nchi hii zaidi ya tabia binafsi za aliye madarakani na kikundi chake cha ulaji. Marais wote watano ndio imekuwa sera za nchi hii.
Nchi hiii hakuna sera wala nini, bali ukiwa rais unatekeleza yake unayoweza, unakuwa na genge lako la ulaji linapigia debe kadiri inavyowezekana hayo unayayaamini, ukitoka anakuja rais mwingine na mbwembwe zake. Mfano wa hiki ninachosema ili ujue hamna sera bali mbwembwe za viongozi, wakati wa JK tuliimbishwa uchumi wa gas kama wendawazimu, na yakapigwa mashairi yote unayoyajua ww. Kweli tukawekeza kwenye bomba la gas. Kaja rais mwingine baada ya JK, ukitaka kujua hakuna sera, kaja rais mwingine yeye kaenda kwenye umeme wa maji! Ukimuuliza imekuwaje sio umeme wa gas tena, anaongea kwa sauti ya chini kuwa gas sio yetu bali ni ya wajanja! Ukitaka kujua hamna cha sera bali utapeli wa kundi la walaji, ngoja aje rais mwingine kabla huo mradi wa umeme wa maji haujaisha au ukiwa umeisha, usishangae akasema anajikita kwenye umeme wa jua au nuklia kutokana na mabadiliko ya tabia nchi! Halafu na yeye atakuwa ni kikundi chake cha kupiga propaganda kama zilivyo kuwa enzi za JK au sasa kwa Magufuli.
Kuhusu hao viongozi wa upinzani kutokutoka madarakani, hapo una hoja za msingi. Lakini mazingira ya vyama vya upinzani ni tofauti na wa chama tawala, wengi wa viongozi wa hivi vyama ndio kama engine ya vyama hivyo kuwepo, na hawana marupu rupu yoyote wanapotoka kwenye uongozi wa vyama hivyo, kwa mantiki hiyo hugeuza vyama hivyo kuwa sehemu ya kuendeshea maisha kwa baadhi yao. Tofauti kabisa ya viongozi wa ccm wa juu, wengi wao utakuta pia walikuwa na nafasi nyingine za kiserikali hivyo bado wanaendelea kulipwa hata baada ya kustaafu. Na kuna upendeleo fulani ambao huupata toka kwa mwenyekiti wa ccm, ambaye mara nyingi huwa rais wa nchi, kwani huwateua kuingia kwenye bodi mbalimbali ili wasife njaa na wapate sehemu za kutolea stress. Sababu hiyo ya hofu ya kimaisha ndio maana unaona ccm iko tayari hata nchi hii iingie kwenye machafuko, na wao huamini amani ya nchi hii ni ccm kuwa madarakani, kwani wanajua hao wazee wote wanaoishi kwa fadhila za ccm, watakufa vifo vya aibu iwapo ccm itapoteza madaraka.