Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Nahic amekuja katika mda muafaka na wakati sahihi na ni mtu sahihi shikamoo mh jp
 
Binafsi nimefurahishwa na kasi ya Dkt. Magufuli. Naamini wapo pia wengi wanaoungana nami katika furaha hii. Magufuli ameanza kwa kasi ambayo kama ataimaintain, Tanzania haimalizi miaka mitano itakuwa tayari ni nchi yenye kipato cha kati.

Hata hivyo wapo baadhi yetu ambao wanakejeli kasi hiyo. Hao kwangu ni watu waliozoea ubwete na bora liende!. Wanamwona Magufuli kuwa ni mtu atakayekuwa kauzibe kwao!

Wapigaji wote, wavivu wote na wazee Wa madili wote watamchukia Magufuli ila mi niseme na niwaombe tu kwamba tumpe support huyu jamaa kiukweli atatufikisha mahali Fulani!

Tuwafichue wote wanapanga kumhujumu (najua wanajulikana), tuwakatae kwani hawana nia njema na taifa letu.

This time Tanzanians need a person of Kagame calibre to order things!. Mazoea sasa bhaaaas na kwamba Hapa kaaaaaaazi tu!

Wana ccm wataumia zaidi so mlisema ukawa wataisoma no. Naona kibao kimeanza kuwageukia sasa mnapost kujihami enhee. Kweli mungu si juma wala athumani,
 
Hii imekaa vizuri sana.Hongera.
Binafsi nimefurahishwa na kasi ya Dkt. Magufuli. Naamini wapo pia wengi wanaoungana nami katika furaha hii. Magufuli ameanza kwa kasi ambayo kama ataimaintain, Tanzania haimalizi miaka mitano itakuwa tayari ni nchi yenye kipato cha kati.

Hata hivyo wapo baadhi yetu ambao wanakejeli kasi hiyo. Hao kwangu ni watu waliozoea ubwete na bora liende!. Wanamwona Magufuli kuwa ni mtu atakayekuwa kauzibe kwao!

Wapigaji wote, wavivu wote na wazee Wa madili wote watamchukia Magufuli ila mi niseme na niwaombe tu kwamba tumpe support huyu jamaa kiukweli atatufikisha mahali Fulani!

Tuwafichue wote wanapanga kumhujumu (najua wanajulikana), tuwakatae kwani hawana nia njema na taifa letu.

This time Tanzanians need a person of Kagame calibre to order things!. Mazoea sasa bhaaaas na kwamba Hapa kaaaaaaazi tu!
 
Utaaibika tu.Mlizoea ubwete,mtakula joto ya jiwe.
tutampima kwa matokeo kama vifaa vya kutosha mahospitalini, madawa ya kutosha, wafanyakazi wa kutosha hasa elimu na afya, vitendea kazi vya kutosha mashuleni, wanafunzi wenye sifa elimu ya juu wote wanapata mikopo, barabara nzuri, maji salama, umeme wa uhakika, uchumi wa mtu mmoja mmoja umekua n.k hatutampima kwa ziara maofisini
 
Tanzania imedharaulika sana kwa kuwa omba omba wakati tunamatumizi ya ovyo ovyo magofuli nakuombea Mungu ufanikiwe ktk kurudisha heshima ya inchi yetu
 
Mwandishi Mwingereza aitwaye Lewis Carroll aliwahi kusema, ''If you don't know where you are going, any road will get you there''.

Wakati wa kampeni za uchaguzi Mkuu, tuliwasikia UKAWA wakimponda mgombea Urais wa CCM kama hana lolote kwa sababu CCM ni ile ile. Kuna wengine walidiriki kusema CCM imeishiwa pumzi na iwekwe kando. Wengine wakasema kama CCM ni kitanda chenye kunguni kama Dk. Magufuli anavyosema, basi wao hawataki kuhangaika kuwauwa kunguni bali watakichoma moto na kununua kitanda kingine.

UKAWA walicheka na kumdhihaki Rais Magufuli aliposema amepania/kudhamiria kuleta mabadiliko bora pindi atakapoingia madarakani kwa kubana matumizi ya serikali, kuongeza mapato ya serikali, kuboresha mfumo wa utendaji na ufanisi, kupitia kodi na ushuru unaowaumiza wakulima, wafugaji na wavuvi, kupitia upya baadhi ya sheria zinazoleta kero kubwa kwa wananchi, kuunda serikali ndogo, kupunguza au kumaliza kero za watumishi wa umma na kupendekeza muundo wa kitaasisi ili kutekeleza kwa ufanisi ahadi zake.

Two weeks down the line, UKAWA kwa sasa wameanza ''kudandia treni'' ya Rais Magufuli kwa mbele wakati huo huo baadhi yao hawajatuambia kama wanamtambua ni Rais wa Tanzania.

Eti wanadai wameanza kumkubali Rais Magufuli kwa sababu ameanza kutimiza Ilani ya UKAWA! Wamesahau ni wiki mbili zilizopita walikuwa wanasema Rais Magufuli hana lolote jipya katika mchango wa mabadiliko bora nchini. Kuna wengine kwa sasa watadai Rais Magufuli ni UKAWA. Wanachofanya kwa sasa ni kutaka kuhalalisha hii dhana ya kuitwa nyumbu na bendera fuata upepo!

Kabla ya viongozi wa UKAWA kuanza 'kudandia treni' ya Rais Magufuli kwa mbele, lazima wawaombe radhi Watanzania kwa kutaka kuliangamiza taifa kupitia mgombea wao wa Urais wa Tanzania ambaye walituletea na kuanza kutuuzia kwenye gunia wakati wanafahamu ni mra rushwa, fisadi na hafai kuwa Rais wa Tanzania.

Mtu muungwana ni yule anayeomba radhi na pia taifa la waungwana ni lile linalosamehe baada ya kuombwa radhi.

UKAWA kabla hamjaungana na juhudi za Rais Magufuli, lazima muombe radhi kwa wapiga kura wengi, otherwise, endeleeni kusimama na Lowassa mwenye mabadiliko fake yakisaidiwa na Ilani yake ya Uchaguzi yenye vipao mbele vitatu, 1)Elimu, 2)Elimu na 3)Elimu.

Kwa wale wanaoamini uwepo wa Mwenyezi Mungu, kwa sasa wanasema Mwenyezi Mungu bado analipenda Taifa letu kwa kutuletea Rais Magufuli.

DSC02819.jpg
 
Acha maneno mengi,thibitisha unachosema. Usiwajazie maneno mdomoni hao unaodai. Bure kabisa
 
mpaka sasa Dk. Magufuli anaonyesha uhai labda aje kuharibu badae
kwani hata Dk.Jakaya alianza hivo hivo
 
Rais Dk. Magufu ana nia ya kweli kulijenga taifa imara. Wiki mbili sasa nipo Arusha asilimia kubwa ya wakazi wa Arusha wanaanza kumkubali hasa ile yotuba yake ya Ijumaa tar20 bungeni. Kila la kheri Rais wetu mpendwa.
 
Hamna jk hakuanza hivi,jk akuanza kwa kupunguza matumizi na wachapakaz,af hyu hyo ndo tabia yake,wala hagezi,nadhani mnamjua
 
Hamna jk hakuanza hivi,jk akuanza kwa kupunguza matumizi na wachapakaz,af hyu hyo ndo tabia yake,wala hagezi,nadhani mnamjua

Akiendelea hivo tutapata mabadiliko ya kweli.
 
Acha maneno mengi,thibitisha unachosema. Usiwajazie maneno mdomoni hao unaodai. Bure kabisa

Asante Sana MsemajiUkweli kwa kuleta uzi huu! Ukiwa walikuwa na Sera ya 1) ELIMU 2)ELIMU 3) ELIMU hii ilikuwa ni kuwahadaa wananchi kukimbia kuzungumza NENO UFISADI kwani key people wa UKIWA/CHADOMO walikuwa wananuka UFISADI kama hadaa za ulaghai hazikutosha walikuja na VIPAUMBELE kwa ajili ya kuwashika Wananchi wasio jitambua kwa yafuatayo 1) Babu seya atakuwa huru 2) Uamsho watakuwa huru 3) Mama lishe kila kona 4) Boda boda kila raia 5) Milo 5 kwa siku kila Mtanzania..... 6) Nyumba za tembe kuondoka Tz baada ya Mwezi mmoja....
 
Sema hawe mqkini maana alipokua ujenz2 alimsimamisha Rostam aziz kujenga barabara atakazozisimamia,maake aliharib kaz,ndo maana jamaa hakutaka hawe
 
Back
Top Bottom