Nimetafakari sana, nimegundua kuwa kwa hakika watanzania tulikuwa tunahitaji Rais kama Magufuli.
Ninachosikitika zaidi ni kwamba, baadhi ya watanzania wenzetu ama kwa makusudi au kwa kutokujua wanabeza kazi nzuri anazozifanya Rais wetu Magufuli na serikali yake.
Watanzania wengi walikuwa wanaimba MABADILIKO bila kujua gharama za hayo mabadiliko.
Binafsi naona haya ndiyo mabadiliko tuliyoyasubiri kwa miaka mingi sasa. Kimsingi huwezi kusema unafanya mabadiliko halafu ukabaki katika hali ile ile. Tunapotaka mabadiliko ya kiuchumi hatunabudi kujifunga mkanda kwanza ili kutengeneza miundombinu ya kiuchumi na hivyo kurahisisha maendeleo ya huo uchumi. Mimi naamini kuwa, kama tutakwenda kwa mwendo huu , kwa hakika baada ya miaka michache Tanzania itakuwa ni yenye maendeleo makubwa sana.
Naomba tumuunge mkono Rais wetu Magufuli ili kufikia malengo haya. MAENDELEO HAYAJI KAMA NDOTO.
hatuwezi kupata mabadiliko ya kweli kama CCM bado ipo madarakani.
Nchi inakabiliwa BAA LA NJAA, rais anasema tusitangaze kama kuna njaa. Mwenzake wa Kenya ameshatanga kwa raia wake. [Afu unasema ndo rais wa wanyonge).
Walisema sukari imefichwa kumbe ni uongo, bei imepanda mpaka sasa serikali imeshindwa kuishusha (inajinasibu ni serikali ya wanyonge, sijui wanyonge gani)
Tanzania ya sasa inatawaliwa ktk misingi ya udini {ukiristu} na ukanda
Zabuni za ujenzi Chato kapewa mtoto wa dada yake{afu unasema ndo rais tuliyemuhitaji}.
Mpaka sasa hakuna fedha za mfadhili yoyote iliyotolewa kusapoti bajeti yetu, Makusanyo yote ya ndani ya ndani yanatumika kulipa mishahara na madeni tu.
Pamoja na kubana matumizi , shilingi ya Tanzania imezidi kuporomoka dhidi ya Dollar ya marekani, na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa za kuinusuru
Na kila anaelalamika mnasema alikuwa mpigaji hata kama ni mjasiriamali aliekopa hela benki kufanya biashara zake halali.
Watu wamepiga hela za Lugumi, hakuna hatua zozote za kumwadhibu aliehusika.
Walituaminisha kwenye kampeni mwaka 2015, Lowassa ni fisadi. Wamejenga mahakama ya mafisadi. Mpaka sasa hawawezi kumkamata ilhali wana kila kitu cha kumkamata.
Serikali ya CCM imeishiwa Pumzi, inaelekea KUFA.
Si mzima wewe, ukapimwe akili