Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Ijapo Mhe. Rais JPM alipiga maandamano marufuku, nadhani wakati umefika wa watu kukaidi marufuku hiyo na kuingia barabarani kuunga mkono jitihada hizi kubwa alizofanya za kubainisha na kukabili wizi wa raslimali za taifa letu.

Naona ni wakati wa Watanzania wote, pasipo kujali itikadi zetu za kisiasa, kuingia barabarani kuonyesha mshikamano katika kuzuia wizi mkubwa unaofanyika kwa nchi yetu. Kumbuka, tusipoingia kuandamana kuunga mkono, ipo siku wataingia wanaoshadidia wizi huo.
 
"Kama unataka kuandamana andamana wewe mwenyewe na familia yako ""

Sisi wenzako tupo bize kutafuta pesa na wewe endelea kushabikia siasa
 
Daaah ko mwanzon ulikuwa humpend au leo umefanya kumpenda kisa hili huhisi ni unafiki mkuu
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, mara nyingi sasa, Rais Magufuli amesikika akisisitiza kwamba yeye ana nia njema na taifa hili. Chochote anachofanya lengo lake ni kulisaidia taifa kutoka kwenye mikono ya 'wapiga dili' na mafisadi.

Hakika nakubaliana kabisa na anachokisisitiza Rais.

Lakini kwa kuwa Rais Magufuli ni mwanadamu mwenye moyo wa nyama, naye anaweza kabisa kujikwaa katika kutekeleza hiyo nia njema. Naamini Marais Mkapa na hata Kikwete nao walisema (na pengine walikuwa) kwamba wana nia njema na Tanzania. Ripoti iliyosomwa leo Ikulu, imetia doa hizo nia njema zao. Leo wanasemwa kila kona ya nchi kuwa sababu ya taifa kuibiwa sana. Watu sasa wanatamani Marais hao wafikishwe mahakamani kwa makosa ya kuhujumu uchumi. Bahati mbaya katiba yetu imetoa kinga. Ibara ya 46 kifungu cha 3 cha katiba ya JMT ndiyo inatoa kinga hiyo.

Imeandikwa:

"Isipokuwa kama ataacha kushika madaraka ya Rais kutokana na masharti ya ibara ya 46A(10), itakuwa ni marufuku kumshtaki au kufungua mahakamani shauri lolote la jinai au la kumdai mtu aliyekuwa anashika madaraka ya Rais baada ya kuacha madaraka hayo kutokana na jambo lolote alilofanya yeye kama Rais wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya Rais kwa mujibu wa Katiba hii."

Kifungu hiki ndicho kinawafanya Rais Mwinyi, Rais Mkapa na Rais Kikwete kuendelea kula pensheni za serikali, licha ya madudu waliyoyafanya kupitia 'nia njema' zao walipokuwa madarakani.

Sasa Bwana mkubwa anajinasibu kuwa yeye ni wa tofauti, siyo kama waliomtangulia. Sawa. Lakini yeye ni mwanadamu pia, kuna kujikwaa kunakosababishwa na yeye binafsi au mtu aliyemtega.

Pendekezo langu: ili kuepusha hali ya kuja kusikitika baada juu ya 'nia njema' ya Rais Magufuli, pale itakapotokea ndivyo sivyo, napendekeza Rais afanye mabadiliko ya kifungu hicho hapo juu. Aondoe hiyo kinga kabisa. Yeye ana nia njema, na amesema mara nyingi anajiamini. Basi, hata kama yeye atajikwaa, namuomba akibadilishe ili kuepuka kuwapata marais wenye 'nia njema' kama za watangulizi wake.

Rais Magufuli tafadhali ondoa kinga ya Rais iliyotolewa na Katiba ya JMT kupitia sura ya 46, kifungu cha 3.

Kila la kheri.
 
Nyani haoni kundule lake!
Huyu mkulu anapata kitu gani kizuri kutoka kwa Bashite ambapo mama Jesca hana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…