Nimefikiria Kwa mwezi nakusanya wastani wa Tshs 1.1 Trillion. Kati ya hizo fedha natakiwa kila mwezi nilipe mshahara billion 550 Tshs, alafu matumizi ya kawaida kama safari mafuta na ununuzi wa vitendea Kazi ni billion 340 TShs.kila mwezi.
Jumla ya matumizi ya kawaida na mishahara inakuwa Billion 890 Tshs, nabaki na kiasi cha Billion 210 Tshs. Kutoka kwenye makusanyo yako ya kawaida kwa mwezi.
Sasa hizi Tzs 210 billion ndio kwa ajili ya maendeleo, kujenga reli, barabara, ndege na viwanja vyake, kusambaza maji na umeme nchi nzima, kujenga shule na maabara, kujenga hospitali, kujenga bomba la mafuta, kununua vivuko, haya machache mengine unaweza kuongezea ya kimaendeleo na hapa bado sijapigwa na watoto wa mjini hawa hawazuiliki hata uwe vipi utawapunguza tu au kuweka mazingira magumu ya kupiga lakini watakupiga tu.
Dah hapa lazima upate hekima ya Ki Mungu la sivyo hupigi step kabisa.