Habari wadau ,Mimi in mmoja wa watanzania niliovutiwa sana na habari zinazoenea katika media habari za ushujaa wa Dr.magufuli,
Tanzania kwa muda mrefu tulihitaji mtu wa kariba hii
Nimefuatulia bunge na vyombo vya habari kwa muda mrefu toka awamu ya raisi wa tatu nimegundua kuna repetition of the words
1) mkapa alisifiwa sana bungeni akitajwa kuwa shujaa na mwanamapinduzi wa uchumi wabunge hawahawa walishangilia na kuvunja viti kwa kulewa na uzalendo wake tena wakimtaja kuwa ni mzalendo baada ya mwalimu hata Mimi niliamini hivyo.
2)sikwmbii kikwete ilikuwaje maana alipambwa kwa kila aina ya sifa wengine walidiriki hata kupendekeza aongezewe muda kwa Yale mazuri aliyotufanyia watanzania,huko bungeni ndio sikuambii alipata kila aina ya sifa kutoka kwa wabunge wasomi
3)awamu ya tano sikuambii naomba uwe shahidi wangu wa kile kinachoendelea wabunge walewale wanaendelea kumwaga sifa kwa mkuu wetu wengine wanadiriki kukata na viuno kabisa wakisfu na kukejeli kama sio kuhoji uzalendo wa yyte yule asiyefanya kama wao
NDUGU YANGU Mimi naomba niwe wa mwisho kusifu na kupongeza kila linalotokea humu nchini nimegundua wale waliosifiwa mwanzo kwa mbwembwe ndio wanaohisiwa Leo kuwa wameliingiza taifa katika hasara kubwa,mikataba mibovu hasa sekta ya madini na gesi.Naomba niwe wa mwisho ili nimsubiri ajaye yeye atatudhihirishia kama huyu wa sasa alikuwa safi ama la?
Nimejifunza kutoamini katika makelele na mbwembe maana ndizo zilizotufikisha hapa.my friend iam against the mass,I have choosen my way minority is my new way.KUNA HAJA SASA YA WABUNGE KUANZA KUSHTAKIWA MAHAKANI
AHSANTE