Ni wazi sasa vilio vya watanzania kuhusu rasilimali zao sasa kimepata mtu wa kuvisikiliza, haijalishi ni njia ipi JPM anatumia, ingawa kwangu naona yuko sahihi kabisa, ni lazima sasa wote tuungane, hata kama kuna makosa katika utekelezaji wa hatua zake, tuungane pamoja kurekebisha kasoro hizo na tupambane pamoja, si wakati wa kusikiliza wasomi wasio jasiri, wasomi ambao kwa muda wote wametumia usomi wao na madaraka waliyopewa kutudanganya na kuwa sehemu ya wizi wa rasilimali zetu.
Wabunge na Viongozi wetu wa upinzani, hayo ndio mliyaibua katika mijadala yenu Bungeni na katika majukwaa, tutawashangaa mkibaki nyuma katika vita hivi.
Wakili msomi Tundu Lissu, ungana kwa hiari na timu ya Raisi kuonyesha usomi wako na uzalendo wako kupigana vita upande wa JPM, wewe ni mtanzania, tambua katika mkataba wowote ule, kuna masuala kama Fraud, Misrepresentation, Unfair Enrichment na mengi tu hufanya mikataba kuvunjwa, mbona unaangalia MIGA tu na mikataba ya kinyonyaji ya kimataifa, tumia weledi wako na mikataba ya kimataifa yenye sura za kinyonyaji ibadilishwe pia, anza kuingia kwenye issues ambazo tunafikiri ndio za kiwango chako sasa, kesi za uchaguzi na uchochezi waachie vijana waanze kupractise.
Kwa hili la rasilimali zetu, tuko pamoja na Raisi wetu