Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania


Tumwunge mkono kukiuka katiba na sheria zilizopo? Yapo mazuri anafanya katika hilo hakuna atakayekataa kumwunga mkono. Lakini anapokosea halafu mnakimbilia kumsifia na kumwunga mkono huo upuuzi hauwezekani kwa watu waelewa. Huwezi kuapa, unamnyooshea Mungu biblia halafu unasigina ile katiba kwa makusudi, ukiambiwa unakuja juu.
 
shikamoo mkuu
 
GTs,

Vitu ambavyo Dkt Magufuli alishafanya mpaka sasa ni:
1. Kuondoa wafanyakazi hewa/vyeti fake zaidi ya 9,000 serikalini
2. Kuitisha majadiliano yenye mlengo wa kulifaidisha taifa ktk rasilimali zake
3. Kulihuisha shirika la ndege la taifa kwa kununua ndenge mpya
4. Kurasimisha uhamaji wa serikali toka Dar es salaam kwenda makao makuu ya nchi Dodoma
5. .....

Ongezea kwenye list
 
JE HAYA NDIO ILIKUWA KIPAUMBELE CHETU KAMA TAIFA?
 
Naona hadi TBC kuna vipindi vya propaganda kama hizi ambapo sio mbaya, kinachosikitisha na kukatisha tamaa ni kuwa wanaoyasema haya ndio hao hao waliomsifia JK kwa moyo na nguvu zote na waliwakemea sana waliomkosoa kama wanavyowakemea wanaokosoa sasa!
 
Hao wafanyakazi hewa walikua wanachama wa ccm,alikuta sukari 1800@,sembe 1200@ kg sasa hivi sukari mpka 3000@kg na sembe 1800 kg bdo mafuta ya kula na vinginevyo,ficha ujinga kusifia upuuzi wa kijinga

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kati ya hayo yote yamemnufaisha vipi mwananchi? Mmesema kulikua kuna wafanyakazi hewa lakini mpaka sasa hakuna ongezeko la mishahara.
 
viwanda vikuwapu.. Maigizo, Maisha bora yakowapi... Maigizo, kuzuia mikutano ya kisiasa... Maigizo
 
hayo yote nakubaliana nayo swali la msingi why life is becoming tougher than/ before you add back your list?
 
Mleta uzi naona umebaki umeduwaa baada ya kupewa za uso za kisawasawa..
6.Ameweka traffic lights Chato.
 
kutoongeza mishahara, kuto ajiri, utekaji, mauaji kibiti, kuzuia mikutano ya kisiasa.
 
hayo yote aliyofanya yanamgusa vipi mfanyakazi na mkulima maskini? maisha yanazidi kuwa magumu udhubutu wake unasaidia nini?
 
Wakuu habari zenu.Mimi ni mwananchi wa kawaida wa nchi yetu pendwa ya Tanzania.Nimekua nikipitia maada tofauti tofauti humu ndani hasa zinazozungumzia siasa na habari za serekali lakini nilichogundua ni kwamba watu wengi wamekua wakizungumzia mapungufu tu yanayojitokeza ktk serekali ya raisi Magufuli na kusahau yale yote mazuri aliyoyafanya katika kipindi hiki cha miaka miwili (hadi kufikia sasa).Na hii ndio sababu hasa iliyonivutia kuanzisha uzi huu ili tuweze kukumbushana mambo mazuri aliyoweza kuyafanya yeye binafsi au serekali yake kwa ujumla tangu aingie madarakani hadi sasa.Humu tupo watu wa mikoa tofauti tofauti kama kuna kitu chochote kizuri ambacho serekali imekifanya katika mkoa wako au mkoa mwingine au katika taifa kwa ujumla na kinamanufaa naomba utujuze na sisi ili tuweze kuelewa na mazuri ya serekali maana kila siku tunasikia mapungufu tu.

Asanteni!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…