habari wadau..
kiukweli kila napomuona magufuli napata amani sana ya moyo..
hasa nikifikiria acacia walivyokuwa wanatuibia na kuwapiga risasi watanzania kwa kushirikiana na jeshi letu la polisi.. na huku viongozi wakubwa wakichekelea kisa wanapewa 1% ya mapato ya acacia na kutumbua na familia zao...
nikikumbuka mgambo waliokuwa wanamwaga vyakula vya mama ntilie..
nikikumbuka wamachinga walivyokuwa wanapigwa mabomu ovyo... leo napowaona kariakoo wanajimwaya mwaya kusaka ugali wao bila wasi wasi... japo wanaziba njia ila napata amani ya moyo kuona wanyonge wana amani ya kusaka ugali wao...
ukweli kabisa na Mungu ananiona sikukupigia kura mwaka 2015.. nilimpigia kura lowassa.. sababu nilijua ccm wote ni wale wale wanaolindana na wanafaidi madini na cake za taifa wenyewe....
ila nimeujua ukweli wewe ndio rais kweli wa wanyonge sio wale waigizaji waliopanda dala dala siku za kampeni tu...
kwa hali hii unayoendelea nayo nakuombea heri sana na mungu akulinde katika kujenga tanzania mpya ambayo kila raia ana haki ya kupata cake ya taifa.. awe amesoma au hajasoma... awe katavi au oysterbay...
nikikumbuka makodi ambayo wakulima maskini wa jembe la mkono walikuwa wanalipishwa na halmashauri zao na huku matajiri kina acacia wakisamehewa kodi... nasikia hasira sana...
magufuli ongeza spidi baba... ongeza spidi sana twende kwa kasiiiiiii..
mtu yeyote anaekupinga unayoyafanya ni mnafiki anataka nchi ya rushwa irudi