Poleni sana ambao nitawakwaza, Sawa mimi ni Mpinzani tena nina kadi
ambayo nimeilipia, lakini upinzani hauwezi kunifanya niwe Mnafiki na
kuuficha Ukweli.
Kipindi ambacho tuliteseka na kusaga meno hakuna aliyetujali, ni kipindi
ambacho Korosho ilikopwa na ikalipwa kwa awamu 3 mpaka 5, kilikuwa
ni kipindi kichungu sana sio tu CCM hata wapinzani wenzetu hawakuona
umuhimu wetu. Nikumbushe tu Tumewahi kukopwa Korosho na mpaka
leo hatujalipwa, wanaokumbuka wanakumbuka.....................
Leo wenzetu wengine naona munamsifia na kumpongeza Kikwete kuwa
alikuwa Bora, sawa ni haki yenu kwa sababu muliona manufaa yake.
Leo hii Tandahimba Tumemsimamisha Mbunge wa Upinzani Ndg. Katani A Katani
cha ajabu huyu ndiye Kinara wa ununuzi wa KANGOMBA tena mbaya zaidi ana
kashfa ya kununua korosho mbovu kutoka mkoa wa pwani....... sitaki kulizungumzia
hilo, wanaotuangusha na kutuletea matatizo kwa sasa ni viongozi wa vyama vya Msingi,
ushirika na viongozi wengine wa Halmashauri ambao wakibanwa vizuri matatizo
yatakwisha.......................... Mbunge wa CCM aliyepita ni mbovu, huyu wa upinzani hamna
kitu tena alikuwa na ushirikiano mkubwa kabisa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa
wa Mtwara ambaye muda huo alikuwa Kiongozi wa Chama kikuu cha ushirika. Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Mtwara na Mbunge wa Tandahimba CUF wameshirikiana sana kutuhujumu
Rais Dr.John Pombe Magufuli umeanza vizuri sana kwenye zao hili la Korosho
najua sio mtu wa kuokea Ovyo Ripoti za Kupikwa, KANGOMBA inahusisha baadhi
ya Vigogo. Kuwa SERIOUS na eneo hili la KANGOMBA ndio kwenye chanzo cha
matatizo yote haya ambayo yamebaki.
WAKULIMA WA KOROSHO TUNAKUKUBALI SANA, kipindi chako kifupi mabadiliko ni
makubwa sana.