Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Baki na ujinga wako, hata kufikiri hutaki kufikiri.

Kwa kukusaidia tu wewe popoma, kigezo cha umri kilikuwa bado hakijatimia, wakati huo alikuwa ana umri wa miaka 36.
Mjenga anadai Magu angekuwa Rais since 1995, singojr anajibu kuwa kwanini isiwe 1961 kama jamaa ameamua kujitoa akili, mimi nikachagiza kuwa Magufuli amezaliwa 1959 (wakati huo ana miaka 2). UPOPOMA wangu huko wapi hapa bro?
 
Mjenga anadai Magu angekuwa Rais since 1995, singojr anajibu kuwa kwanini isiwe 1961 kama jamaa ameamua kujitoa akili, mimi nikachagiza kuwa Magufuli amezaliwa 1959 (wakati huo ana miaka 2). UPOPOMA wangu huko wapi hapa bro?
Duuuhh, ''Fikiri kabla ya kutenda"

Natengua kauli mkuu.
Nilikuelewa vibaya, ulipotaja mwaka wake wa kuzaliwa nilikuelewa kuwa unamaanisha mwaka 1995 ndio angekuwa na sifa ya kuwa rais kwa kigezo cha umri. Ndio maana nikakuuliza ''nini kilishindikana" kwa sababu akilini mwangu nilijua alikuwa bado hajafikisha umri wa kuwa Rais kwa mjibu wa Katiba.

Kumbe wewe ulikuwa ulikuwa unampinga yule uliyemjibu na ndio ulikuwa unapingana na hoja ya kuwa Rais toka mwaka 1995 kama mimi.

Niwie radhi mkuu, nisamehe sana!!!
 

Tuko pamoja mkuu
 
Nakuunga mkono mkuu,ila binafsi ningependa wahujumu wote washuhulikiwe bila huruma,naona kama kasi ni ndogo sana.Inakuaje mpaka leo hatujasikia yeyote aliyefungwa kwa uhujumu uchumi?I don't understand what is happening.Yaani wanatumbuliwa tu halafu wanaachwa watambe mtaani! Hapana, hatutakuwa tumefanya kitu.Washuhulikiwe hawa, ili iwe fundisho kwa wengine.
 
bila shaka kikwete and co wanajisikia vibaya sana kuona jamaa anavyo wa-prove wrong ktk utendaji wao.nina shaka hao ndio watakuwa wa kwanza kupanga mikakati ya kishetani ya kummaliza.magufuli my president be extra carefully.
Safi sana kijana tupo pamoja
 
For sure we need to Magufulify Africa so that we reach where so many other developed nations have reached.
 
Magufuli keep on walking on that trajectory, up to now we're still on the right track!!
 
Pigeni sana kelele lakini "Hapa Kazi Tu "
 

Attachments

  • IMG_20180525_151114.jpg
    258.6 KB · Views: 32
  • IMG_20180525_151259.jpg
    187.4 KB · Views: 30
  • IMG_20180518_124207.jpg
    247.6 KB · Views: 30
JPM NI ZAIDI YA TUMJUAVYO

Niungane na Watanzania Wengi kwanza Kumshukuru Mungu kwa Kutuinulia Ndugu John Pombe Magufuli, kama Mwenyekiti wa CCM Taifa, Sidhani kama katika Wakati Huu tunaweza Kuwa na Mtuwa Aina yake, Wengi wananielewa ninachomanisha.

TATU BOMBA
Katika Maisha ya Siasa nimejifunza kuwa UZOEFU ni Muhimu, lakini Hauwezi kuzidi Ubunifu , Uweledi, Uthubutu na Utashi wa Kisiasa.

Ingizo la Ndugu Mizengo Peter Pinda waziri Mkuu Mstaafu, na Ndugu Makongoro Nyerere sikuelewa Vizuri, ila alipopendekeza Jina la Ndugu Dkt. Bashiru Ally Kakurwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM nilielewa huu utatu mtakatifu.

KWANINI HAWA WATATU
Tuanze na Ndugu Pinda , ukitazama viongozi wakuu wenye Umri, uzoefu na uadilifu ambae mienendo yake hata baada ya kumaliza kazi ya Uwaziri Mkuu utakubaliana na mimi kuwa Ndugu Pinda ni ingizo Sahihi ukiwaacha Marais wastafu, sisemi ni Bora kuliko wengine lakini Haiba yake inahitajika zaidi katika kushikilia Dhana ya Uzoefu kwenye Chama na Serikali, Uwepo wake utaisaidia CCM kwa miaka 10 ijayo.

Ndugu Makongoro Nyerere, wengi bado wanauliza Kaingia kufanya nini? Kwa wanaomjua Makongoro katika Siasa za UDAMBWIUDAMBWI, kama hunielewi Jiulize Kwanini Ndugu Wasira bado ana Nguvu kwenye CCM japo alikosa Ubunge kule Bunda, Sina maneno ya kuwaelezea hawa watu ila itoshe kusema kuwa CCM inahitaji watu wa Aina ya Makongoro ambao Wamezaliwa na kukulia ndani ya Misingi ya Chama cha Mapinduzi.

UJIO WA DKT. BASHIRU CCM
Ndugu Magufuli kama Ni kwenye Mpira wa Miguu amemudu kuucheza na kumaliza Dk 90 akiwa Nyota wa mchezo.

Ujio wa Dkt. Bashiru kama Katibu Mkuu wa CCM unasadifu Mambo Muhimu yafuatayo :-
1. Chama kimeanza kujenga safu ya Utendaji wa watu wenye Uweledi wa Modern Politics siasa za kisasa zinazohitaji Hoja na Sio kelele, Dkt. Bashiru kama wengi wakivyosema wamefundishwa nae Siasa pale Udsm na mimi nikiwa Mmoja wapo 2003-2006 , mbali na kuwa mwalimu wa Sayansi ya Siasa jambo zuri ni kuwa yeye ni Muumini wa Siasa za kumkomboa mtu Mweusi katika Umajumui wa Maendeleo.

CCM imeanza Kurudisha Misingi ya kuanzishwa kwake chama cha Wakulima na Wafanyakazi (hapa kwa Wafanyakazi ni pamoja na wafanyabiashara au mtu anaefanya kazi halali ya kumuingizia kipato) ambacho kinaanza Kuwavutia Wasomi wa Kati, kawaida na wale wa kiwango cha Juu.

2. Ccm Inaanza kuonekana kwa vitendo kuwa ni chama Cha Wote ili mradi uwe na Uweledi na Maarifa ya Kuongoza, haijalishi ulikuwa Nani Ccm Utapata fursa ya kusimama na Kuongoza, Hili limetimia kwa Dkt. Bashiru ambae mimi nimemjua mwaka 1998 akiwa mwenyekiti wa Tawi la Ccm Abiyani pale Ubungo, na zaidi ya Hapo wengi wamekuja kumuona akiwa Mwenyekiti wa Tume ya kuhakiki Mali za CCM , hakuwa mtu maarufu au Mashuhuri ndani ya CCM

Hii ni Karata nzuri katika Kuwaaminisha wananchi kuwa Ccm sio mali ya mtu au kikundi fulani Bali ni Bidii na maarifa yako tu, sasa naamini watu ambao ni Wasomi watagombea nafasi ndogo na za kawaida mfano kata z matawi, Wilaya na Mkoa.

3. Ujio wa Dkt. Bashiru unatoa fursa ya kuanza kushughulikia tatizo SUGU la matumizi mabaya ya RASILIMALI za Chama, yeye amezunguka Karibu nchi nzima ameona chama kikoje na kina nini, katika siasa za sasa suala la kujiimarisha KIUCHUMI ndio Agenda kubwa ambayo itaendelea kuleta Uhai wa chama mana uko mbeleni naona kila dalili ya kuondolewa au kupunguzwa kwa Ruzuku kwa Vyama vya Siasa mana zinatafunwa tu kama fedha za Capacity Charge kwa IPTL, Songas na Richmond.

HITIMISHO
Naomba nihitimishe kwa Kuwatazama watu wawili wakubwa kwanza ni Wana CCM wenzangu, na pili Dkt. Bashiru
Ndugu zangu wana CCM Tumepata Katibu Mkuu Mweledi, Mbunifu na Msomi najua wako *Majeruhi* baadhi waliofisadi Mali za chama najua hawa hawatamtaka kabisa Dkt. Bashiru watamkwamisha kila kona na kumuhujumu , mimi nasema hao mafisadi ni wachache sisi wanachama ni wengi hivyo mkae kimya kwa sasa muacheni Katibu Mkuu mpya afanye kazi, najua mtaibuka na Agenda zenu mfu kuwa Hakijui chama na Sio mzoefu, ila mjue siasa zimebadilika sasa ni siasa za hoja na Sio Matusi au kushambuliana, lakini mwenyekiti alishasema anataka kujenga Ccm mpya ndio hii sasa.

Kwako Dkt. Bashiru, wewe kwangu ulikuwa Mwalimu tuliona misimamo yako, hukuogopa na tunaamini uku utaendeleza zaidi.
Yako Mambo Mazuri unapaswa kujifunza kutoka kwa Mtangulizi wako Ndugu Kinana, yeye alikuwa kama Kisima Jangwani chukua Mazuri yake, endeleza pale alipoishia ila kubwa Endelea Kujenga Umoja , Mshikamano,UTII na uadilifu kwa Chama na wanachama, Wasaidie wenzako kufanya vizuri, na wale wanaofanya vizuri waendeleze wafanye vizuri zaidi na zaidi , Naamini katika Wewe, tutamuona Mwalimu Nyerere kwenye Chama, mana tumeshamuona Serikalini kupitia Dkt. John Pombe Magufuli.

Jua pia kuna wanafiki Wachache sana japo wana Vinguvu kwa Kiwango cha PhD

Usiyumbe Wala Kuyumbishwa

Wako katika Uzalendo
Jerry C. Muro
 
Jerry hana Ipad au Computer? Naona amepambana na kasimu kake ka tochi kuandika andiko hili. Nyota hizi ni few evidencing which validate the reality
 
Huyo ndio Jerry Muro wa Kilanya....Shikuterewia ko iruwa kusumane mae!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…