Binadamu ni kiumbe cha ajabu sana kisichosaidika kwa lolote,kila jambo linapotokea Duniani huwa lina maana yake,liwe baya au zuri.
Binadamu anapenda mazuri tu hapendi mabaya,Binadamu hajui kuwa ni lazima augue ili Daktari apate ajira.
Ni lazima atende jinai ili askari wapate ajira,kifupi ni kwamba mazuri na mabaya yote yana faida sawa.
Wakati nafundishwa Biashara ya FOR EX nilikula hasara hadi nikawa nashinda njaa,kwanini nili ing'ang'ania Sana hiyo Biashara ?
Wakati nasoma Business administration, lecturer wangu alikuwa akinieleza kuwa " where there's big loss there's also big profit ".
Leo hii nikiangalia nyuma nabaki kuishangaa Dunia na maajabu yake, hivi ndiye Mimi wiseboy. Ambaye Leo hii nakula nachotaka kwa Sababu ya faida ya Biashara iliyowahi kunipa hasara hadi nikataka kujiua?
Kama hayati Nelson Mandela asingefungwa miaka zaidi ya 25 Leo hii hakuna mweusi ambaye angekuwa rais South Africa, kama kusingekuwa na Bahari Ndege zisingekuwepo.
Kila jambo na maana yake chini ya jua.
Sifa kubwa ya Bomu ni kwamba,pale linapokutana na upinzani,yaani sehemu ambayo linataka kuilipua inapokuwa ngumu zaidi na Bomu nalo huwa linaongeza uwezo wa kulipua yaani huwa linapata nguvu zaidi.
Sasa hivi watu wanapiga kelele eti Rais Magufuli anaua upinzani,anaua vipi upinzani wakati ndo anaupa nguvu upinzani?
Hata yeye anajua fika kuwa upinzani ndo unapata nguvu zaidi na siyo kufa.
Sasa ubaya wake uko wapi?
Nawapa Home work ya miaka 15 ijayo au 20 kwa wabishi.
Kama Una watoto watatu kwa mfano,mtenge mtoto mmoja,mnyanyase,usimsomeshe na kama vipi mfukuze hata nyumbani.
Baada ya miaka kadhaa utakuja kuona ni nani kabarikiwa kimaisha kati ya Huyo uliyekuwa ukimnyanyasa na hao uliokuwa ukiwapenda.
Narudia tena kila jambo lina maana yake chini ya jua,ni lazima wachungaji wapigwe ili kondoo watawanyike na hapo ndo watapata Green pasture.
Huwezi kufanikiwa kibiashara bila kupata loss kubwa.
Huwezi kushinda vita kubwa bila adui yako kukuelemea.
Mtabaki kulalamika tu,"ooh anaua upinzani " kumbe uwepo wake ni mpango wa Mungu ili wapinzani wachukue dola.
Formula ya Mungu si formula ya mwanadamu.
Niia za Mungu si njia za mwanadamu,mawazo ya Mungu si mawazo ya mwanadamu.