Na
Augustino Chiwinga
0659438889.
Anaitwa Mheshimiwa Daktari John Joseph Pombe Magufuli, Rais wa Tanzania wa awamu ya 5.
Ni Amiri Jeshi Mkuu lakini pia ni Mwenyekiti wa Chama kitukufu Chama Cha Mapinduzi.
Ni mwanamageuzi namba moja mzalendo mchapakazi hodari faraja ya wanyonge na mpenda watu wake.
Ni namba moja katika kulinda na kutetea raslimali za nchi.
Ni Namba moja katika kujenga uchumi mpya wa Viwanda.
Ni namba moja katika kutumbua mafisadi ,wahujumu uchumi na wala rushwa.
Ni namba moja katika kuinua kilimo,uvuvi na ufugaji.
Rais Magufuli ameimarisha upatikanaji wa pembejeo na zana za kilimo, kuimarisha huduma za ugani, kuimarisha huduma za umwagiliaji, kuwezesha upatikanaji wa masoko na kuhamasisha Sekta binafsi, vyama vya ushirika na kuanzisha viwanda vya kusindika mazao ya kilimo.
Ni namba moja katika kuwasikiliza na kuwatetea wanyonge .
Ni namba moja katika Elimu . Kahakikisha wanafunzi wanasoma bure na wale wa elimu ya juu wanapata mikopo.
Ni namba moja katika ukusanyaji mapato. Kutokana na juhudi zake makusanyo ya ndani kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yaliongezeka kutoka wastani wa Shilingi Bilioni 850 kwa Mwezi mwaka 2015 hadi Shilingi Trilioni 1.3 kwa Mwezi mwaka 2017 sawa na ongezeko la asilimia 34.6.
Ni namba moja kwenye Afya. Katika kipindi cha kuanzia Novemba, 2015 hadi Novemba 2017, Serikali imeongeza Vituo vya kutolea huduma za Afya kutoka Vituo 7,014 mwaka 2014/2015 hadi 7,284 mwaka 2016/2017, sawa na ongezeko la Vituo 269 .
Vilevile, Serikali imeongeza bajeti ya dawa kutoka Shilingi Bilioni 31 mwaka 2015/16 hadi kufikia Shilingi Bilioni 260 mwaka 2017/2018. Hadi mwezi Juni, 2017, asilimia 83 ya dawa muhimu zaidi
( essential medical items ) zinapatikana katika Bohari ya Dawa na hali ya upatikanaji wa dawa kwenye Hospitali kufikia mwishoni mwa mwezi Julai 2017 ni asilimia 86.3.
Ni namba moja katika miundombinu .Amejenga barabara madaraja ,meli na vivuko mbalimbali.
Ni namba moja katika usafirishaji na uchukuzi.Amenunua ndege mpya na anatuletea treni ya umeme.
Ni namba moja katika Ulinzi.Mipaka ya nchi yetu iko salama,ametokomeza majambazi na viashiria vyote vya uvunjifu wa Amani vilivyojitokeza.Watanzania sasa wanalala na kuamka salama.
Ni namba moja katika Nishati.
Sasa anajenga mradi mkubwa wa kuzalisha umeme Mto Rufiji wa Megawtt 2100. Pia Kwa upande wa umeme vijijini, Serikali imekamilisha kwa asilimia 100 Mradi Kabambe wa Umeme Vijijini Awamu ya Pili (REA Turn-key Projects phase II), jumla ya wateja 172,000 kati ya wateja 250,000 wameunganishiwa umeme na sasa hivi mradi wa umeme vijijini awamu ya tatu (Turnkey III) unatekelezwa kote nchini ambapo jumla ya vijiji 7,673 vinatarajiwa kupatiwa umeme.
Ni namba moja katika ,Utawala Bora Demokrasia Uwazi, Haki za Ubinadamu na Uongozi wa kiutumishi.
Ni namba moja katika kukuza uchumi. Uchumi wetu umekua na kuimarika.Ukuaji wa Pato la Taifa umekua kwa asilimia saba (7%) na hivyo kuifanya Nchi yetu kushika nafasi ya tatu kwa ukuaji wa uchumi barani Afrika.
Ni namba moja katika Huduma ya Maji. Mheshimiwa Rais ameanzisha kampeni ya kumtua ndoo mama kichwani yenye lengo la kumhudumia mwananchi kupata maji kwa umbali mfupi. Serikali imeboresha huduma ya maji vijijini ambapo hadi Septemba 2017, jumla ya miradi 1,423 ya maji vijijini ilikuwa imekamilika na kufanya jumla ya vituo vya maji vilivyojengwa kwenye miradi kufikia 117,190. Vituo hivyo vina uwezo wa kuhudumia watu 29,297,500, sawa na asilimia 79.
Pia miradi mbalimbali mikubwa ya maji inaendelea kujengwa kote nchi nzima.
Ni namba moja katika kuwawezesha wananchi kiuchumi. Vyama vya Ushirika vimeongezeka kufikia 10,596 zikiwemo SACCOs 5,640. Vyama hivyo vina jumla ya wanachama Milioni 1.3 na vina hisa zenye thamani ya Shilingi Bilioni 52.9. Aidha, Serikali kupitia Mifuko mbalimbali imetoa mikopo ya jumla ya Shilingi Trilioni 1.4 kwa zaidi ya wananchi 750,500.
Pia, katika Mwaka 2016/2017, Halmashauri zilitenga Shilingi Bilioni 28.4 kwenye Mfuko wa Maendeleo ya Vijana na Wanawake ambapo hadi Juni, 2017 Shilingi Bilioni 8 zilikopeshwa kwenye vikundi 6,076 vya vijana vyenye wanachama 30,380.
Ni namba moja katika mawasiliano.
Mkongo wa Taifa wa mawasiliano umefikishwa katika maeneo yote yanayohudumia wananchi hivyo kushusha gharama za mawasiliano na kuongeza wigo wa mawasiliano
Pia Serikali inafikisha huduma za simu za viganjani kwa wananachi wote ambapo kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Kata 443 zenye uhitaji wa huduma za mawasiliano zimepata wazabuni wa kupeleka mawasiliano husika. Kati ya kata hizo 443, upelekaji wa mawasiliano umekamilika katika kata 391 na Kata 52 zilizobaki zinategemewa kufikishiwa huduma hiyo kabla ya mwisho wa mwaka 2019. Vilevile, kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote Serikali ilitoa zabuni ya kufikisha huduma ya mawasiliano katika kata 75 zenye vijiji 154 ambazo zimekamilika mwezi Juni, 2018.
Kwa haya acha machache wacha tuendelee kumuunga mkono namba moja wa Tanzania anafanya maendeleo zaidi ya alichohaidi wakati wa kampeni alipokua anaomba kura.
Magufuli Oyeee.
Augustino Chiwinga
0659438889.