Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Kesho asubuhi njoo na vyeti vyako vya shule kama huna basi njoo hata na kadi ya chama hapa ofisi ndogo lumumba upewe kazi ili njaa isiendelee kukutafuna

Jamaa inaonekana una njàaa kali sana
 
Write your reply...Hakuna nyongeza ya mishihara kwa watumishi wa umma.
 
haa haa naona namba za simu kote. duh hivi sisi vijana tutatumika na wanasiasa hadi lin?
Wilaya gani unadhani ipo wazi?
Kaulize makarai ya ufipa
Haha sisi vijana tuna hali ngumu sana sio kwa kujitongozesha huko lakini sawa usijali utafikiliwa umemwaga sifa kemu kemu ila jua sio hisani
Raisi kufanya hayo ni jukumu lake pamoja na kodi tunayo lipa
Jamaa ni lijinga kweli

Linasifia na kumtukuza MWANADAMU

Nyimbo za mapambio zimekolea kama yule Msomi uchwara banseni bana
bahati mbaya sana baba jesca sidhani kama ana nia ya kuongeza shemeji au mke
Yaan kwanza ni Verified user ukaona haitoshi Ikabidi uweke namba Mwanzo mwa mada ukaona bado haitoshi ukaweke namba baada ya Mada tena.


I
Wanafiki ni watu hatari saaana. Wakishajua unataka nini ndo wanakupa.

Wakijua demu anapenda sifa, wanamsifia then the rest is history!!!

Mh pokea zifa za wanafiki ili wapate kile wanataka
Khaaa UMEJITAHIDI
Nyongeza
Magufuli alichofaulu kwa asilimia nyingi ni kuwajaza watumishi na wananchi nidhamu ya uoga pamoja ya kudhoofisha vyama vya upinzani.
Umemaliza??
Tutakupigia
Kesho asubuhi njoo na vyeti vyako vya shule kama huna basi njoo hata na kadi ya chama hapa ofisi ndogo lumumba upewe kazi ili njaa isiendelee kukutafuna

Jamaa inaonekana una njàaa kali sana
Hiyo namba ya simu ya kazi gani!? U dc sio kitu cha mchezo
Write your reply...Hakuna nyongeza ya mishihara kwa watumishi wa umma.
Aaaamen .
Hivyo nyie wote mliotoa hizo coments zenu hapo juu mnaroho na mioyo ya kupambana na maisha kweli?

Nyie wote hapo mlipo mawazo yenu yote mnataka kuishi kama waamerika au wa-Europe. Sasa mnafikiri hao wa-amerika na wa-Europe vijana wao wa zama hizo kabla maendeleo hayaja wajia wangekuwa na mioyo iliyokata tamaa kama yenu, hayo maendeleo waliyo yapata leo yangeonekana kweli?

Kama hamjui basi mwelewe kuwa misingi ya maendeleo yao hayo yalitokana na viongozi wao wenye vision kama Rais wetu John Joseph Pombe Magufuli na ambao walikuwa na mioyo ya ushupavu wa ku-risk maisha yao kwa ajili ya maendeo na maisha bora ya wananchi wao.

Maisha bora hayaji yenyewe bali huja kwa njia ya bidii ya binadam kufanya kazi kwa ufanisi na hivyo kila mmoja wetu kutoa mchango wake kwa jamii.

Kabla ya kuwalaumu vijana wenzetu ambao wanafarajika na matendo ya Rais wetu na kuamua kuchukua nafasi zao kumsifu kwa juhudi na jitihada zake, ingekuwa busara kwenu kwanza kujiuliza nyie wenyewe mchango wenu kwa jamii ni upi? Je, mmezaliwa na kuja duniani kwa ajili ya kuwakatisha tamaa wengine kwa frustrations zenu za maisha?

Maendeleo ya Amerika ya leo yalianza na George Washington Rais wao wa kwanza aliyeongoza mkataba wa Philadelphia uliofanyika mwaka 1787, England ya leo yalianza na malkia wao wa wakati huo Queen Elizabeth I "The Virgin Queen" baada ya kushinda vita dhidi ya waspania mwaka 1588, Ufaransa nao revolution yao waliyoifanya miaka 1787 na 1788 ya kumwondoa mfalme wao King LUDWIG XVI na wajerumani yalianza na Emperors wao Willhelms na Bismark.

Kwa hiyo mtaona vijana wao hawakuwa depressive and desperate kama nyie, badala yake waliwaamini na kuwasikiliza viongozi wao na kufanya bidii ya kazi kuyatumikia mataifa yao ili kuondoa umasikini na shida zilizo kuwa zinawakabili wakati huo kwa ajili yao na vizazi vyao vya leo na vijavyo na ndiyo maana na sisi tunayahusudu maisha yao leo.

Kwa nchi iliyo jaliwa kuwa na neema kubwa ya rasilimali kama nchi yetu, sikutegemea kuona vijana wanaokaa vijiweni na kuanza mazoea ya uzomeaji na ukatishaji tamaa kwa wazalendo wetu badala ya wao wenyewe kujishughulisha na maarifa ya ubunifu wa kutafuta njia
zitakazo wawezesha wao kutumia utajiri wetu huo na hivyo kutoa mchango wao kwenye pato la taifa letu la kujenga nchi ya viwanda. Taifa imara na lenye maendeleo linajengwa na vijana mashupavu wakishirikiana na viongozi wao wenye vision ya kuleta mabadiliko yao na sio vijana ambao ni mazombi wanao subiri kupewa amri ya kitendo cha uhaini na hatimaye kuishia kaburini.

Msimwoone Rais Magufuli kama ni mjinga, ana malengo yake mwenyewe ambayo amejiwekea kwa mafanikio yetu sisi wote na vizazi vyetu vilivyopo na vijvyo. Ni wajibu wetu kushirikiana naye kwa hekima na taadhima. Ebu jiulizeni wenyewe; moja Tanzania hii leo baada ya uchaguzi wa 2015 na matatizo yote yale tuliyo kuwa nayo, tungekuwa wapi sasa? Mbili mnajua watoto na wajukuu wenu wangekuwa na maisha gani huko mbeleni, kama ambavyo mnajua mambo ya ovyo yaliyotendeka, yangeendelea kutendeka?

Nyie ndiyo vijana mnaotegemewa kuliondoa Taifa letu kutoka hapa lilipo kwenda kwenye Taifa lenye neema mbeleni. Neema haiji kwa kukaa vijiweni na kuanza kukandia na kuwazomea watanzania wenzetu ambao wanania moja kama sisi wote ya kuliona Taifa letu nalo likipiga hatua, bali inaletwa na wananchi wenye mwamko wa kishujaa katika kufanya kazi kiufanisi.

Mnawaona wenyewe wenzetu wachina, wavietnam na south Corea walivyo piga hatua za maendeleo katika nchi zao! Miaka 30 iliyopita wachina walikuwa kama sisi wategemeaji wa NGOs, lakini kipindi cha mda mfupi tu wamekuwa Global Players. Kwanini? Kitu gani kimetokea kwao?

Maendeleo dugu zangu hayaji kwa kukaa kijiweni na kuwavunja nguvu wazalendo wetu kwa visions zao. Maendeleo yanakuja kwa michango yetu ya vitendo na sio kwa domo la kisiasa.
Kama mnadhani vyama vingi ndiyo solution ya maendeleo basi nawaomba angalieni nchi zenye vyama vingi kama Italy, DRC na nyinginezo, nadhani hapo ndipo mtatambua faida na hasara zake.

Maisha hayana "nostrum" mkae mkijua, bali ni ubunifu wetu wenyewe ndiyo utatuwezesha sisi ishi vizuri na kudumisha umoja na amani yetu nchini. Pia nawaomba mzingatie kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi duniani ambayo ina makabila mengi, sasa kama machafuko yatatokea hatujui hasara zake zitakuwaje na matokeo gani na kwa mda gani?

Nawasihi sana tuachane na unafiki wa akina Msigwa, Mbowe, Tundu Lissu, Zitto Kabwe na Lema. Hii mijitu iko tayari kufanya chochote kile kwa manufaa yao binafsi. Mazombi haya yasioyotaka kuona hali alisi ya watanzania ilivyo, wako tayari kupokea kwa shangwe kubwa kuona Rais Magufuli na watanzania kwa ujumla tunaporomoka kwenye maadhimio yetu ya kulikwamua Taifa letu.

Nawasikitikia sana watu kama Zitto Kabwe na Tundu Lissu, hawa watu kwa karisma na ubobeaji wao katika maswala ya uchumi na sheria Rais Magufuli angewahitaji vibaya mno katika serikali yake ili wakashirikiana naye katika kuleta maendeleo ya nchi yetu. Kwa maamuzi waliyo amua kuyafuata kupinga kila kitu serikali inacho kusudia kufanya, kusema kweli ni pigo kubwa kwa Taifa letu. Tumewapoteza vijana wetu ambao wangeweza lisaidia Taifa letu.
 
We jinga...usije nikariri tena afu ukakomenti huu ujinga wako chini ya andiko langu,eti raisi Magufuli ana malengo yake na hii nchi ana malengo yake nchi ya babaake hii,tunataka rais atayeonesha dira ya malengo ya nchi,anayetii katiba na kuiheshimu siyo anayekuja na malengo yange.
Hao vijana wa Ulaya unaowasifia hawakuwa na upuuzi wa kusifia na kujipendekeza hivi ndo maana wakafanya mapinduzi kwenye nchi zao na kuleta maendeleo.
Huyo Magufuli kama unampenda sana kanywe nae chai usinipangie kumsifia mtu ambaye kwangu naona hanifai,kama anakufaa ni wewe usilisemee taifa zima.
Au unamuona Mungu,Mungu mwenyewe hapendwi na wote kina kama hawa @Kiranga.Atakuwa huyo unayetaka asifiwe tu kwa matakwa yako...UMENIUDHI SANA.
 
Unachoongea ni kama alichokifanya mwenzio.Kumtukuza huyo mnayemtukuza. Unaweza kunambia Magufuli ana vision gani na nchi hii? Unadhani maneno anayoongea kwenye mikutano yake ni vision? Inaonekana ulienda shule kujifunza ujinga.Rais asiyetaka kuheshimu sheria za nchi,bunge na mahakama hana vision yotote zaidi ya kujitajirisha kwa kujificha kwenye kichaka cha uzalendo.Wewe unadhani uzalendo ni kumsifia rais au kiongozi yoyote? Rais akifa ina maana uzalendo wako unakuwa umekufa,mim na wengine uliowaita wanafki tunasimama na Tanzania ambayo hata rais asingekuwa Magufuli tungepambana kuhakikisha nchi yetu inaenda mahali ambapo miaka 50 hadi 100 baadaye watoto wetu watakuwa proud...SIPO HAPA KUMFURAHISHA RAIS,NIPO KUIFURAHISHA NCHI YANGU.
 
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji120] Hiyo inaonyesha dhahiri ni kiasi gani umekosa hekima na busara ya ku-argue na watu ambao wanajua nini maana ya maisha. Wewe katika karne ya 21 bado unatumia nyenzo za "Tarzan" katika kutafuta solution ya mawazo yako? Karne ya 21 wewe bado unatumia nyenzo za Jungle? Wewe umesoma shule na vyuo vipi? Binadam aliye elimika na mwenye busara hata weza anza na kauli "We .... jinga" ndiyo iweje sasa? Nikuogope? Kama upo humu na unatoa coments za kizombi lazima tuta ku-crash tu hata kama utatumia njia ya Jungle. Hayo Mambo ya vitisho peleka kwenu bush na umfanyie mke wako na watoto wako sio mimi.

Kwa mtazamo wangu naona wewe huna hata chembe ya uelewa aidha wa maisha wala wa uongozi. Maisha kwa taarifa yako ni utamaduni ambao jamii imejiwekea kulingana na resources zao zilizopo. Uongozi ni njia ya kuifanya hiyo jamii kupata fursa ya kutumia Resources zake kwa manufaa ya jamii nzima kwa kufuta taratibu za kijamii na manzingira hiyo jamii iko.

Unazungumzia katiba kama vile mtu asiye elewa nini maana ya katiba na nini maana ya uongozi?

Nikuombe kitu unisaidie, niambie basi katiba ya CHADEMA ina semaje? Na Mbowe mwenye kiti wenu anafanya nini?
Miaka zaidi ya 25 sasa sijasikia hata siku moja mkiwateua viongozi wengine. Je mnazingatia katiba yenu?

Of cause Magufuli anaiheshimu katiba, una kipengee cha katiba ambacho wewe unaona amekikiuka? Kama kipo ni kipi? Na yeye anafanya nini kinyume na kipengee hicho?

Ndiyo inajulikana kuwa hii nchi sio ya baba yake, lakini yeye ni kiongozi wa serikali ambaye amechaguliwa kidemokrasia na kwa msingi ya katiba. Hapa naona hujui unalo litaka au?

Nasikitika kukutambulisha kuwa sijakueleza wala kukulazimisha umpende yeye na kumwona yeye kama Mungu wako, bali hiyo ni kanuni moja wapo ya katiba ya kuheshimu kiongozi wako, au hulijui hilo? Ndiyo maana narudia kusema tena unazungumzia kuhusu katiba wakati kanuni na sheria zilizomo humo huziui juu ya mwenendo na mamlaka ambayo Rais anayo?

Kuudhika kwa ajili ya argument yangu katika demokrasia ni kitu cha kawaida na usitegemee kama mimi nitatoa au kuchangia hoja ambayo kila mmoja ataifurahia, kama nitakuwa nimevunja sheria basi kuna vyombo ambavyo vinahusika na uwajibishwaji wa mwenendo wangu.

Wito wangu kwako; jifunze kuwa na busara na ujipange katika maelezo yako. Hatuko kwenye mapango ya Ol Doinyo Lengae hapa, hapa tunashindana ki-arguments!
 
Nalazimika kukujibu japokuwa nimepata uhakika kuwa hauna akili.
Umeuliza katiba ya CHADEMA inasemaje,kwanza katiba ya CHADEMA haina ukomo wa uongozi,Mwenyekiti atachaguliwa kila baada ya miaka mitano mpaka pale wanachama watapoona hafai (siyo wanaccm).
.Unasema CHADEMA haijawahi kufanya uteuzi wa Viongozi miaka 25 sasa? Are you serious?
.Magufuli haheshimu katiba ndiyo,anazuia mikutano ya kisiasa wakati katiba ina ruhusu.
.Anafungia hovyo vyombo vya habari vinavyoandika uweli.
.Hafuati sheria za manunuzi ya umma (ndege,ujenzi wa barabara ma vinginevyo anajiamulia tu) ...hapa narudia kukuambia hii nchi siyo ya babaake wala yake.
LA MWISHO MKUU,KAMA WEWE NI JINGA UTABAKI KUWA JINGA TU,SINA JINA LINGINE LA KUKUITA KAMA AKILI YAKO HAIPO SAWA.
 
Kwa nini hujaweka namba kama mwezako?? Tutakupataje sasa??
 

Umeandika Andiko reeefu kweli kweli ila lisilo na Mantiki ,unachotakiwa kujua ni kuwa hatuwezi kufanana Akili woote tukasifia.Inawezekana umesimama Jangwani na unaona Mwisho Magomeni ,wenzio hatuishii kuona Magomeni kama wewe.Sifia tu sisi tutakosoa ili kuboresha zaidi.
 
Pole sana mkuu sikujua kama nimeandika andiko reeefu kweli kweli, kwa sababu najua elimu na busara haina ukomo. Kama ingekuwa ndiyo hivyo basi hata vitabu tunavyosoma vingekuwa na page moja tu.

Msomi na mpenda kueelew wa kweli huwa urefu wa andiko sio issue kwake, ila kilicho andikwa ndiyo cha msingi.

Sijasema wote tufanane akili na ni kitu ambacho hakitawezekana, ila kwa wapenda demokrasia ni vizuri na ni busara tuka mweshim kiongozi wetu na kumwacha amalize awamu yake ya tano kwa kushirikiana naye katika kufikia malengo yake aliyo yakusudia.

Tunaweza tukamtoa 2020 endapo tutaona
Hatakelezi yale aliyo ya ahidi, lakini kwa hali jinsi inavyo onekana, sidhani kama kuna lazima wa kuchangia kiongozi mwingine wa chama chochote kile. Atapita tu.

Magufuli ni kiboko wenu. Huyo jamaa sio mtu wa longo longo huyo ni jembe.
 

Na huku kumtukuza kwako pafanye kama sehemu yako ya Sala ya kila Siku ,usisahau kumkumbuka mungu wako mdogo.
 
Na huku kumtukuza kwako pafanye kama sehemu yako ya Sala ya kila Siku ,usisahau kumkumbuka mungu wako mdogo.
Sababu zako za personal na Rais mimi sio mwamuzi, kama amekuingilia uhuru wako kiuchumi tumia mkondo wa sheria kudai haki zako.

Mimi binafsi sina matatizo naye. Simtukuzi yeye ila naona faraja ya kuona kuwa ni Rais anaye jali shida za wananchi wenzake na kujaribu kutafuta ufumbuzi unaostahili pale inapo bidi ili kutatua shida hiyo kulingana na madaraka yake.
 


Kwani alipo chaguliwa ilikuwa ni akafanye nini ?.Kuna haja ya kuwatukuza Viongozi wanao wajibika katika Majukumu yao ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…