Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Uzalendo UPI sasa wa vitendo au wa majukwaani, mzalendo halisi ni MWALIMU aliishi kwa maneno na vitendo hakuwahi hata kununua baiskeli kwa kodi zetu kupeleka kijijini kwake.Hakuwahi kuwa na kasfa yeyeto, japo alifail uchumi Lkn ametuachia manufaa tele tele,umoja,mshikamano,ardhi kuwa ya umma,lugha ya kiswahili nk.
Ntakuchagua tena MAGUFULI 2020, unayoyafanya nimelizika nayo 100%, sioni sababu yakukunyima KURA yangu
 
Mzalendo? Yupi? Anae tesa na ku ua wanao jaribu kukosoa maovu yake? Au una zungumzia anae shusha uchumi kila siku?
 

Huwa sikubaliani na Musiba lakini nikiwaza sana naona kama kuna mambo anayosema yanaukweli. Mimi nikakutuhumu wewe unalipwa na Jamii Forums kila mwezi kinakushinda nini kufungua kesi kama ni uwongo!!!

Kuna kesi nyepesi kama hiyo? si kiasi cha yeye kuitwa mahakamani adhibitishe tu, Au nakosea jamani?
 
Tumia akili yako kufikiri, usitumie makalio.

Mimi nikafungue hio case unategemea nisimame kama nani mahakamni? Nidai fidia ipi wakati si husiki hata nukta katika huo uwongo/uchochezi kwa viongozi anaoandika, wala hao aliowachafua sio baba zangu au ndugu zangu au viongozi wangu.

Ila naongea kama raia anaopenda nchi yake, na sitaki kuanzishwa kwa chuki/fitna/visasi baina ya viongozi, tutakao umia ni sisi raia wa chini.

Huyo musiba unaemtetea ameandika upuuzi kuhusu mtu kama ABDULRAHMAN KINANA (anajua mzee wa watu alivo pambana kuinusuru kifo hio CCM yenu au anaropoka tu kuuza magazeti).

Na huo uongo kuhusu kikao cha sisi baina ya Zitto , Rostam Aziz, Bernad Membe, Lowassa. Na kushabikia wale wasimamizi wa waandishi wa habari kukamatwa na kuwaita ni wapelelezi wa kimataifa??? Kushabikia raia/wafanya biashara kukamatwa??? Kama sio uchochezi baina ya seikali/viongozi/wafanya biashara ni nini???
 
Hahahaha
Nyie majamaa mna matatizo makubwa walahi
 
nikupe hongera mheshimiwa rais kwa jinsi unavyoamua maamuzi "magumu" huhitaji kufikiria mara mbili.ukiamua umeamu. daima mbe"re" nyuma mwiko. kama kuna a"sa"ri tutajua"ga" "mbere kwa mbere"
ushauri wangu kwako (mimi mwananchi mnyonge ambaye nanyongwa na haki yangu sipewi"

kuwaonesha wewe hubabaishwi, hutishiki... hizo korosho mkuu ziletwe dar. tena usinunue kwa 3000 kwa kilo. nunua hata kwa 5000 kwa kilo.zilete dar mkuu. gawa kwa wananchi angalau nusu kilo kilo kwa kila mtu.watanzania wengi tunapenda korosho. tatizo bei yake baba... bei ndo inatuangusha.

na korosho zitatusaidia sana kwenye nguvu za kiume kwa wengine ambao zimepungua. hapo mkuu wala huhitaji hata kuja kuomba kura mwaka 2020.tunakuchagua tu. au kama vipi hizi korosho ziweke mpaka mwka 2020. wakati wa kampeni kwenye mikutano yako uwe unagawa kamfuko hata ka nusu kilo kwa kila mwananchi. hakyanani unapita kwa kura nyingi sana. kuna mikoa hawajui hata ladha ya koroshow. ni tamu sana koroshow.

hata wanaogombea ubunge nao wapewe tumifuko.tutawachagua ka mfuko kadogo kamoja ka nusu kilo kwa kura.tuachane na ule utaratibu wa zamani wa tshirt,kofia na kanga.wanaohujumu uchumi wataabishwe sana.watu walidhani serikali haina pesa.pesa zipo tatizo ni matumizi tu ndo hamna.na kama kutakuwa na zao lingine watu watalega lega kununua hakuna kuremba. serikali inunue maisha yasonge mbele.

ccm woyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.
 
Nampongeza Rais wetu kwa kazi nzuri anazofanya. Watanzania tulihtaji rais wa namna hii kurudisha heshima ya watz nje na ndani ya nchi. Kuna mambo mengi tu Rais wetu tunahtaj kumpongeza na kumuomba aendelee hv hv ili nchi isonge mbele. Marekani na nchi zingine za ulaya hazitasita kuwa na sisi kwa sbb hamna taifa ambalo linaweza kuacha ushirikiano na TZ kwa rasilimali tulizonazo.
Pili Rais aangaze zaidi kwenye taasisi za serikali na za elimu ya juu kuhusu uwiano wa watumishi na utendaji kazi wa kila mtumishi. Kuna taasisi zingine watumishi wengi kuliko uhalisia....ili taifa lijikwamue lazima tukubali kuchange mind zetu leo hii ukienda nchi za nje huwezi kupata kazi kirahisi mfano India n.k wanafanya interview zaidi ya nane kumpata mtu anayetakiwa. Nakumbuka ilifikia mahali kila mtu ni jeuri tu.

JPM heko heko sana. Endelea kupiga kazi mungu akubariki na kukupa maisha marefu.

NAWAKILISHA.
 
Jamani huyu baba Mungu amuweke tu miaka mingi. Yaan kabla ya Magufuli hili taifa lilikuwa linatafunwa na kila mtu kuanzia wafagizi hadi mameneja na wakurugenzi kama shamba la bibi vile!!!
Ahsante sana kudhibiti rushwa, walau sasa hivi hakuna rushwa kila mahali, ingawa inasemekana kuna jipu anajiita 'Jiwe' na mwanae madereva wanatafuna bado hazina ya nchi yetu. Raisi wetu mpenzi Magufuli najua hujashindwa kudhibiti yote haya.

Ahsante kwa kutujali wakulima mhe baba jpm mpenzi wa watu na malaika!! Najua hii ya korosho ni mwanzo tu, mwakani utapanga bei ya mazao yote, na kama mfanyabiashara anaona haimlipi jesh litanunua nyanya, pilipili, mahindi, maharage, mchicha na kila zao kwa bei ya maslahi yako baba magufuli then watasaga mahindi hata kwa mabuti kudadadeki!!

Hakuna kama wewe mhe rais, mpemzi wa wanyonge. Ahsante kwa kutuletea ndege nzuri maana hata kama wengi wetu hatupandi, walau tunaondoa ushamba kwa kuziona zikipepea angani!!!

Ahsante kwa kufungia hela BOT Maana mabenk yalizidi utapeli, bora tu hela zipotee mzungukoni na matajiri waishi kama mashetani kama ulivyo sema rais wetu mzuri.

Yaani we mbaba ninavyo kupenda,
Mmmmwaaaaah!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…