Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Tz haina ubavu wa kutunisha msuli Mabepari juzi tu waliminya kutoa msaada wa ARV tukaanza kulialia we ngoja wakaze uone kama hatuombi poo.
 
Jiwe hutokana na mwamba.Mwamba huu upo katika kila pembe za Dunia.Mwamba ukipasuka vipande vipande huunda Mawe Ambayo nayo yakivunjika vunjika huunda vipande vidogo vidogo zaidi vya mchanga tena vya aina mbalimbali tunavyoita Udongo ambao ndio ardhi hii tunayoishi sisi binadam.
Nimeona thread nying hum Jukwaani watu wakimfananisha Rais wetu na mwamba huu ambao huwa katika ugum wake kiasi kwamba kwa mikono ya mwanadam bila kutumia nguvu ya kutengeneza hauwezi kuupasua wala kuuvunja.HAKIKA nakubaliana na wanaomwitwa hivi Rais wetu maana amekuwa ni mgum,mgum,mgum.... ((((Nkonk...Nkonk...Nkonk....kwa msim wa sasa wa kizazi cha Insta wanasema)))
Ugum wake hakika umejidhihirisha katika maamuzi yake magum ya kukwepa maslahi binafsi na kuzingatia maslahi ya MASKINI wasiokuwa na SAUTI awali.HAKUNA haja ya kuyataja,mwenye akili anaelewa.
Ugum katika kuwadhibiti wazandiki waliokuwa wanajichukulia Mali katika nchi yetu ni ugum ambao kwa sasa tunaona Rais wetu kauvaa bila hofu wala UOGA na leo hii Tanzania sio nchi ya kuingia na kutoka kama Chama Flani kilichoonyesha ulaini sana kama kifuu cha nazi kwa kuacha Itikadi na misingi na kuwakumbatia Vibaraka wa wazandiki hawa.Naona hum Jukwaani wanamwita Jiwe,Nawaunga mkonom...ni Jiwe Haswaaa...
Kwa HAKIKA Jiwe hili haliwezi kuvunjwa na vifuu vya Nazi ambavyo Labda baadae kwa kutumia sayansi ya Viumbe visivyo vya sayari hii wanaweza labda kutumia vifuu hivi kutengeneza machine itakayo Pasua Jiwe hili.
. .....
Acha watunyime misaada,Acha watuite majina Mabaya na Kutuchafua,
ILA UJAMAA wetu
KuJITEGEMEA kwetu,
Ndio MAENDELEO YETU.

Na bila Rais wetu kuwa Jiwe
Na wengine WALIMWITA Chuma awali......
Hatuwezi kupambana na Ukoloni Mambo Leo.

Mkuu wewe mwenzetu uko kazini.....unaendesha maisha yako kwa hii kazi.....kwa hiyo haina haja ya kupingana wala kukubaliana na wewe.
 
Tz haina ubavu wa kutunisha msuli Mabepari juzi tu waliminya kutoa msaada wa ARV tukaanza kulialia we ngoja wakaze uone kama hatuombi poo.
waulize wakwepa kodi wanaouza hisa zao.Waulize wafanya biashara wa korosho watakwambia Jiwe ni nani?
 
Poleni watumishi,hakika fanyeni hujuma indirect dhidi ya serikali hii onevu kwenu
 
Issue ni kuwatunishia msuli mabeberu kama anavyojaribu JIWE. Ni kwamba hafui dafu ikiwa wataamua kumkazia na ikibidi wanatumia njia mbadala kama kilichotokea kwa Muamarri.
Tukiwasapoti mabepari ni Kweli watatumia njia Mbadala ila tukimuunga mikono JIWE. ....naamini Tutashinda
 
wewe ni kiongozi wa kupigwa mfano, mwenye maono na misimamo dhabiti juu ya yale unayoyaamini. kuna wachache wanakubeza kwa unayoyoyafanya kwa kuona kwamba hayafai lakini walio wengi hasa wale wenye nia njema na taifa letu wanakuhusubu na wapo nyuma yako kukuunga mkono kwa jitihada zako. Uungwaji huo mkono tumeushudia pia ukifanyaka kwa namna mbalimbali hasa kwa baadhi kuachana na vyama vyao na kujiunga na CCM, chama chenye sera za kutekelezeka.

Tumeona namna ambavyo umejaribu kutatua matatizo sugu katika taifa letu kama ukosefu wa tiba bora, ukosefu wa vifaa tiba na madawa, upungufu wa walimu na vifaa vya kufundishia na kukalia madarasani, ufufuaji wa mashirika ya umma yaliyokufa ama kuonekana kuelemewa, ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraji, kupunguza kwa kiwango kikubwa migogoro ya ardhi na ujenzi wa reli ya kisasa ya kiwango cha SGR. Hizi ni baadhi ya jitihada zako kati ya nyingi ulizofanya na unaendelea kuzifanya.

Wewe ni kiongozi mwenye maono 'visionary leader' ambayo huchoki kuwa mfano kwa wengine. juhudi na jitihada hizi unazoonesha kwa watanzania wanakupongeza sana na wapo pamoja nawe. Usikwazike na maneno ya wachache wanaojiahidi kubeza kasoro na kuacha kuona mengi mazuri yakifanyika. Duniani kote watu kama hawa wapo wanaopinga kila kitu kwa lengo la kuongeza ufahamu lakini kwa Tanzania wanapinga kila kitu hasa yale mazuri na huwa wanachukizwa sana na juhudi zako za kuleta maendeleo hivo wanapinga kwa sababu ni vibaraka wa mabeberu na wanawatuma wapinge kwa maslahi yao na hao mabepari.

NI vigumu sana kuongoza watu wanaokupiga na kuishi nao pamoja licha kuwaona wakikupinga hata kwa yale mazuri lakini wewe mheshimiwa rais umeweza hilo na unlikabili kwa akili kwa maslahi mapana ya nchi yetu, nakupongeza sana kwa hilo. wasaliti wanatoa siri kwa mataifa mengine ili kuihujumu nchi yao bila kujua kwamba wanajaribu kukata kuti ambalo nao wamelikalia. wengi wamekuwa wakienda kinyume na malengo na wengine kujitoa kabisa jumlajumla na kuwa makuwadi wao kwa maslahi yao binafsi.

bandiko hili halijataja mtu yeyote na haliuhusiani na mtu yeyote na mhusika mkuu wa bandiko hili ni rais pekee. Nawakaribisha wanajukwa kushare nanyi pongezi zenu kwa kipenzi chetu , mzalendo na mjamaa dkt Magufuli.

FPT 2040


k
 
Pendekezo langu "ajiuzulu "awaachie viongozi yeye atafute kazi zinazomfaa kama zile za mkuu wa uchinjaji kule vingunguti.
 
Ni kweli maana huyu si kiongozi ni Mtawala. Nasi tunataka kuongozwa siyo kutawaliwa.
Ngoja Lissu aje tuone atakavyoumauma maneno,anaweza kuchukua credit (terminal mpya) ya kwamba Lissu kashukia kwenye uwanja wake wakati hata milembe hospitali wanajua ni uongo.
 
Back
Top Bottom