Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Tunashuhudia katika historia ya Taifa letu Kiongozi mkuu wa chama kikuu cha upinzani na Kiongozi wa Kambi rasmi ya upinzani Bungeni akiwa mahabusu ,huku viongozi wengi kama si wote wa upinzani wakiwa na kesi na Wengine wametumikia vifungo.
Tunapoelekea kufunga mwaka Tumpongeze Kiongozi mkuu wetu mtukufu kwa mafanikio haya makubwa ya ki historia.
 
Hii ni satire au paradoxes kwanini upinzani tuu? Je wengine hawana makosa na hawakosei kama Mungu?
 
Umefanya vema kumpongeza kwa kutimiza malengo yake mkuu.

Ila kule Geita tuna usemi,"Mbwa wako akimaliza kuiba vya jirani, atarudia vya kwako"
 
Viongozi wa upinzani wako gerezani kwa kufanya kazi yao, lakini wezi na wabadhirifu wa mali ya umma wako maofisini na mitaani kwenye magari ya kiyoyozi kwa gharama za mlalahoi; na wako huru kabisa na hilo ndio linakusukuma kumwaga pongezi?!
Anyway; ukikua utaelewa na utajutia akili yako ya usaa!
 
Hivi wale waliyokuwa wanapiga kila dk mln 7 kesi yao imeisha Je?

Ova
 
Sijasikia mtu mwenye kesi ya hujumu uchumi/ufisadi akinyolewa mpk sasa

Ova
 
Reactions: MTK
Hivi wale waliyokuwa wanapiga kila dk mln 7 kesi yao imeisha Je?

Ova
Wakuu huu uzi wa kusifia mafanikio haya makubwa ya mkuu mtawala wetu.Lawama malalamiko pelekeni pengine.
 
kumbe sukuma ndani ni moja ya ahadi yake.

viwanda ilikuwa ni porojo tuu.
 
Wafundishe wawe na discpline na kufuata sheria. Upinzani sio uhuni wakilijua hilo basi watakuwa Huru!
 
Wafundishe wawe na discpline na kufuata sheria. Upinzani sio uhuni wakilijua hilo basi watakuwa Huru!


Ukikua utaelewa tu, it may be too late lakini utaelewa tu kwani hakuna barabara ndefu isiyo na kona au mwisho, haya yatapita na kuna watu wa aina yako nguo za ndani zitawabana!
 
katika kutekeleza agizo la Rais Dk. John Magufuli, ktk kusimamia haki za wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu ‘Wamachinga’ kwa uharaka, tayari baadhi ya viongozi wa wilaya na mikoa wameanza kusimamia ugawaji wa vitambulisho kwa wafanyabiashara hao

kama tunavyojua mapema wiki hii, Rais Magufuli aligawa vitambulisho 670,000 kwa wakuu wote wa mikoa nchini, ambapo kila mkuu wa mkoa alipata vitambulisho 25,000 lengo ni kuhakikisha wafanyabiashara katika wilaya zote wanapata vitambulisho hivyo ambavo vitasaidia wajasiriamali mambo mengi ikiwa na kutambuana lakini pia kupata heshima wanayostahiki katika jamii na serikali. Wataweza kuunda vikundi kwa ajili ya kupata misaada lakini pia wanaweza kukopesheka. Tayr mkoa kama Simiyu ushaanza zoez la ugawaji wa vitambulisho
 
Ngoja kuche pingapinga watakuja na matongotongo machoni kupinga ugawaji vitambulisho.
 
Ngoja kuche pingapinga watakuja na matongotongo machoni kupinga ugawaji vitambulisho.
Kiongozi anachaguliwa ili atende mema kwa nchi na wananchi wake na ndiyo yampasayo. Lakini inapokuwa kinyume chake wananchi wana wajibu wa kunung'unika na hata kukemea. Maghufuli ni binaadamu kukosea na kutenda mema ni sehemu ya ubinaadamu huo.
 
Kiongozi anachaguliwa ili atende mema kwa nchi na wananchi wake na ndiyo yampasayo. Lakini inapokuwa kinyume chake wananchi wana wajibu wa kunung'unika na hata kukemea. Maghufuli ni binaadamu kukosea na kutenda mema ni sehemu ya ubinaadamu huo.
Achana na misukule ya Lumumba
 
Hiki ni kitenga uchumi kingine cha serikali,huwezi kutatua matatizo ya machinga kwa kuwapatia vitambulisho kwa kulipia 20,000/=. Hivi vitambulisho ni njia nyingine ya kumkamua ng'ombe maziwa wakati hana malisho mazuri ya chakula.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…