Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Sidhani kama hilo liweza kutokea, hatukumchagua kwa bahati mbaya hivyo hakuna mtu wa kumchukia.
Kwa kasi aliyokuja nayo ndugu yetu, baba yetu, rais wetu Mh.John P. Magufuli endapo ataendelea na kasi hii na akafanikiwa kutimiza ahadi zake kwa asilimia 70, basi tutarajie kuona Mh. Rais kuchukiwa na walio mchagua na kupendwa na wasio mchagua.
 
[emoji848] [emoji848] [emoji848] Hili sikubaliani nalo.
kama chaina,


mbowe apewe wizara na mnyika anaweza kuwa katibu mkuu wizara ya pesa huku waziri wake akiwa mwigulu ,yaani nchi itakua kama german
 
Mwandishi Mwingereza aitwaye Lewis Carroll aliwahi kusema, ''If you don't know where you are going, any road will get you there''.

Wakati wa kampeni za uchaguzi Mkuu, tuliwasikia UKAWA wakimponda mgombea Urais wa CCM kama hana lolote kwa sababu CCM ni ile ile. Kuna wengine walidiriki kusema CCM imeishiwa pumzi na iwekwe kando. Wengine wakasema kama CCM ni kitanda chenye kunguni kama Dk. Magufuli anavyosema, basi wao hawataki kuhangaika kuwauwa kunguni bali watakichoma moto na kununua kitanda kingine.

UKAWA walicheka na kumdhihaki Rais Magufuli aliposema amepania/kudhamiria kuleta mabadiliko bora pindi atakapoingia madarakani kwa kubana matumizi ya serikali, kuongeza mapato ya serikali, kuboresha mfumo wa utendaji na ufanisi, kupitia kodi na ushuru unaowaumiza wakulima, wafugaji na wavuvi, kupitia upya baadhi ya sheria zinazoleta kero kubwa kwa wananchi, kuunda serikali ndogo, kupunguza au kumaliza kero za watumishi wa umma na kupendekeza muundo wa kitaasisi ili kutekeleza kwa ufanisi ahadi zake.

Two weeks down the line, UKAWA kwa sasa wameanza ''kudandia treni'' ya Rais Magufuli kwa mbele wakati huo huo baadhi yao hawajatuambia kama wanamtambua ni Rais wa Tanzania.

Eti wanadai wameanza kumkubali Rais Magufuli kwa sababu ameanza kutimiza Ilani ya UKAWA! Wamesahau ni wiki mbili zilizopita walikuwa wanasema Rais Magufuli hana lolote jipya katika mchango wa mabadiliko bora nchini. Kuna wengine kwa sasa watadai Rais Magufuli ni UKAWA. Wanachofanya kwa sasa ni kutaka kuhalalisha hii dhana ya kuitwa nyumbu na bendera fuata upepo!

Kabla ya viongozi wa UKAWA kuanza 'kudandia treni' ya Rais Magufuli kwa mbele, lazima wawaombe radhi Watanzania kwa kutaka kuliangamiza taifa kupitia mgombea wao wa Urais wa Tanzania ambaye walituletea na kuanza kutuuzia kwenye gunia wakati wanafahamu ni mra rushwa, fisadi na hafai kuwa Rais wa Tanzania.

Mtu muungwana ni yule anayeomba radhi na pia taifa la waungwana ni lile linalosamehe baada ya kuombwa radhi.

UKAWA kabla hamjaungana na juhudi za Rais Magufuli, lazima muombe radhi kwa wapiga kura wengi, otherwise, endeleeni kusimama na Lowassa mwenye mabadiliko fake yakisaidiwa na Ilani yake ya Uchaguzi yenye vipao mbele vitatu, 1)Elimu, 2)Elimu na 3)Elimu.

Kwa wale wanaoamini uwepo wa Mwenyezi Mungu, kwa sasa wanasema Mwenyezi Mungu bado analipenda Taifa letu kwa kutuletea Rais Magufuli.

DSC02819.jpg
Sasa kama anatimiza ilani ya ukawa shida uko wapi, muhimu tupige kazi.
 
Mwachenu magufuli afanye kazi ya wananchi kama wewe no ccm basi najuwa 2020 I'll vote no 4 magufuli na kama we we ni ukawa na mwananchi wa kawaida watamchagua lea kishindo Jana atatekeleza wajibu wake lea wananchi.
I support you.
 
Sipendi upinzani ufutike, lakini ninapenda viongozi wa upinzani wanaofanya biashara ya kisiasa lazima wafutike.

Huwezi kutueleza kwa miaka zaidi ya nane kuwa mtu fulani ni mla rushwa na fisadi halafu baadaye ukarudi tena na kuanza kutuaminisha tumchague kuwa Rais wa Tanzania kwa sababu siyo mla rushwa na fisadi. Mbaya zaidi unatuambia hayo maneno uliyosema yalikuwa ni maneno ya kisiasa tu. Hukumaanisha kama kweli ni mla rushwa na fisadi.
Kula tano [emoji109]
 
Sidhani kama wataipata tena imani kubwa kama waliyoipata kabla ya ujio wa Lowassa na genge lake ndani ya CHADEMA.

Mbowe aliwachuuza wana CHADEMA wengi kwa kumkaribisha Lowassa na kumpa tiketi ya kugombea Urais.

Kuna watu wengi sana ambao waliweka imani zao kwa CHADEMA kwa sasa hawawezi kumsamehe Mbowe kwa kuwachuuza!
Aliwauza jumla jumla.
 
Hakuna namna nyingine Zaidi ya kuungana na Magufuli katika baadhi ya hoja. Kwa sasa naona inayotekelezwa ni Ilani ya ukawa hivyo hapo ukawa watumie busara. WAKANDAMIZE HUMO HUMO kwenye hoja za magufuli. Ccm watakimbia wenyewe watawaachia ukawa magufuli wao
Ni kuunga tu mkono uwe ukawa au ccm tuungane nchi isonge mbele.
 
Binafsi nimefurahishwa na kasi ya Dkt. Magufuli. Naamini wapo pia wengi wanaoungana nami katika furaha hii. Magufuli ameanza kwa kasi ambayo kama ataimaintain, Tanzania haimalizi miaka mitano itakuwa tayari ni nchi yenye kipato cha kati.

Hata hivyo wapo baadhi yetu ambao wanakejeli kasi hiyo. Hao kwangu ni watu waliozoea ubwete na bora liende!. Wanamwona Magufuli kuwa ni mtu atakayekuwa kauzibe kwao!

Wapigaji wote, wavivu wote na wazee Wa madili wote watamchukia Magufuli ila mi niseme na niwaombe tu kwamba tumpe support huyu jamaa kiukweli atatufikisha mahali Fulani!

Tuwafichue wote wanapanga kumhujumu (najua wanajulikana), tuwakatae kwani hawana nia njema na taifa letu.

Habari zaidi, soma =>Toka kwa Wananchi: Kero na Vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa...


Wapigaji wote (Zitto Kabwe, Lissu, Mbowe) hawa hata siku moja hawataweza kumpenda Magufuli, wamejitahidi sana kumchafua na kuwaaminisha watanzania kuwa hafai kumbe ni hasira zao tu za kukatiwa mirija zinawaumiza. Wavivu na wazee wa madili mjini (wanaume wa Dar) hawa ndiyo wajinga wa nchi hii, hawapendi kazi, wanafikiri ujinga wao ndio hali ya kila mtanzania. Hakuna zaidi ya Magufuli 2020 na hatuhitaji mtu yeyote aje badala yake.
 
Back
Top Bottom