Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Wananchi mitaani wamedai kasi hii ya Mhe Rais Magufuli kwao inawaridhisha sana na wanamuunga mkono. Wamedai mwaka 2020 wataidhihirishia dunia kuwa wanamuunga mkono Rais Magufuli kwa kumpa kura nyingi za ushindi wa kishindo.

#KasiInaridhisha #TunakuungaMkono

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani mi ndiyo kwa Magu huniambii chochote mpaka 2025
 

Kasi yangu ya kutapika imeliridhisha tumbo langu.
Kuliko kasi ya kisasi Under the gun.
 
Ni kweli Mh.Rais anauthubutu mzuri sana ,tatizo kubwa ni Kiburi cha madaraka,kusigina katiba,democrasia,kuua upinzani,kuelekeza ama kubariki siasa chafu mfano biashara ya kuunga juhudi.Vinginevyo angekuwa Raisi bora wa zama zote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vijijini watu wanashindia Mizizi na viwavi jeshi Shule hazina madarasa,yeye anasema tuko kwenye right traki.
 
Ndugu,
Miongoni mwa Habar kubwa za Magazeti ya Leo ni hii isemayo "SHULE BINAFSI ZIBANWA." Taarifa zinasema sasa shule binafsi zitabanwa kuhusu mambo ya ajabu ajabu wanayojifanyia Especially Huu Mtindo wa Kukamua wananchi wa Tanzania kwa Kulipa Ada kubwa.
Binafsi bila unafik nichukue fursa hii Kuipongeza Serikali ya Rais John Magufuli kwa kuliona hili. Shule binafsi kwa kipindi kirefu wamekuwa wakijitungia makanuni ya ajabu ajabu yanayowaumiza wazazi ikiwa ni pamoja na Kuchuja MWANAFUNZI na kuwazuwia wasifanye mitihani ya Form 4 kwa kisingizio kwamba hawajafikisha kiwango. Nilishawahi kuleta Uzi hapa kuzungumzia ujinga huu wa kukaririsha wanafunzi madarasa na au kururudia rudia madarasa ni Mchezo wa kupiga Pesa za Watanzania Kihuni!!
Wamekuwa pia wakiwafukuza MWANAFUNZI kwa sababu ya kushindwa kulipa ada hata ya mwezi mmoja tuu .
Sasa Arubaini yao imefika,kwa Tangazo hili la Waziri husika tunashukuru sana. Hongera sana Serikali kwa kuliona hili.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kilaza huyu

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
Siyo kilaza Mkuu. Kuna Shule binafsi Wanafanya enrollment ya Madarasa 5 hadi 6 tangia Form 1 wanaendelea nayo cha ajabu ni kwamba wakifika Form 3 wanachuja na kubakisha Darasa moja ama mawili !! Muda wote huo wameshapiga Pesa miaka mitatu then only two Classes ndio watakaofanya Mtihani wa Taifa!! Waliobaki warudie waendelee kulipa Mapesa once more. Huu ni wizi.
Wamekuwa na tabia ya kujipangia Ada kubwa kuliko hata Fee University.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alafu aliewaroga ni nani? Hakuna shule inayolazimisha mzazi alete mtoto wake kwao. Kama unaona shule fulani ada zao kubwa au hawataki kusumbuana na wewe kuhusu ada, usipeleke mwanao. Lawama za nini hasa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na Emmanuel J. Shilatu

Napenda kuungana na Mamilioni ya Watanzania kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Kwa hatua nyingine ya kununua ndege Mpya ya Airbus A220 - 300 iliyopewa jina la Ngorongoro.

Ndege Ngorongoro Ni Airbus ya pili kutua nchini. Ya Kwanza ni Airbus Dodoma. Tukumbuke ndege Aina ya Airbus Ni ndege ya Kwanza kabisa Afrika inayomilikiwa na Watanzania. Hiyo ni alama isiyofutika iliyoandikwa na Rais Magufuli kwa Tanzania, Afrika na Dunia Kwa ujumla.

Tukumbuke ndege iliyotua Leo Ni ya sita kununuliwa na Serikali ya awamu ya 5 inayoongozwa na Rais Magufuli. Ndege nyinginezo no Bombardier Q400 ambazo zipo 3, Dreamliner 1, na Airbus A220 - 300 ambazo zipo 2. Jumla kuu Ni ndege 6, bado ndege moja.

Ndege hizo zitasaidia kukuza utalii, kuitangaza nchi yetu Tanzania, kukuza biashara, kuongeza mapato ya ndani ambayo yataimarisha uwezo wa ndani wa Serikali kuwahudumia Wananchi na kutekeleza miradi ya maendeleo.

Tunachojivunia Kwa Rais Magufuli sio tu ndege 6 bali ameweza kutoa elimu bure kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari; kujenga miundombinu Kama flyovers; ujenzi wa reli ya kisasa kwa kiwango Cha standard gauge inayotumia umeme; ujenzi wa viwanda vipya zaidi ya 3000; ujenzi wa vituo vya afya vipya pamoja na madarasa.

Mengineyo Ni ongezeko la mapato ya ndani kutoka Tsh. Billion 800 Hadi Trillion 1.3; Ongezeko la wastani wa asilimia 1.5 ya ukuaji wa uchumi nchini; Ongezeko la Tsh. Billion 107 ya makusanyo ya mapya ya madini nchini; Ujenzi was strigler's gogle itakayozalishi zaidi ya megawats 2100.

Hayo ni kwa uchache zaidi ya Mambo mema yanayofanywa na Serikali inayoongozwa na Rais Magufuli. Hakika huyu ndio Rais Watanzania tuliokuwa tukimwitaji zaidi.

*Shilatu E.J*

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…