Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Wakuluma, wafanyakazi, wafanyabiashara, wapinzani, wasomi wahitimu na wananchi kwa ujumla kila mtu ameonja ladha ya uongozi wa Rais Magufuli kwa miaka minne. Je, ni tamu, chungu au?

Je, ipo siku tutasema bora angebaki?
 
Siku mafisadi wakipata fursa ya kurudi na kuendelea kufyonza ndio mtamkumbuka sana mzee wa watu, leo hii yapo yanaomba sana achoke ila kila siku anaibuka na nguvu mpya, Mungu amlinde, aendelee kumpa nguvu ili awamu yake ikija kuisha nchi iwe imeshavuka hadi mafisadi hata yakirudi yakose pa kuanzia.
 
Wakuluma, wafanyakazi, wafanyabiashara, wapinzani, wasomi wahitimu na wananchi kwa ujumla kila mtu ameonja ladha ya uongozi wa Rais Magufuli kwa miaka minne. Je, ni tamu, chungu au?

Je, ipo siku tutasema bora angebaki?
Kwa mada hizi Unaelekea elekea kuja kuwa mtalaam (mganga wa kienyeji) siku za usoni. Ongeza bidii
 
Una upeo mdogo Sana,aendelee ili iweje kwa mfano,Tuko wenye uwezo na maarifa zaidi yake, kwani nn Cha ajabu alichokifanya? Watanyakazi,wakulima, wafanya biashara wote wanalalamika
 
Namba 3 ina walakini mkubwa
Nadhani inaondoa maana ya bandiko lako
 
Kwahiyo mnataka awanunulie chakula na kuwaletea nyumbani? Kalaghabao! Hakuna hela ya wizi! Kafanyekazi halali kwa juhudi na maharifa utapata hela!
 
Wakuluma, wafanyakazi, wafanyabiashara, wapinzani, wasomi wahitimu na wananchi kwa ujumla kila mtu ameonja ladha ya uongozi wa Rais Magufuli kwa miaka minne. Je, ni tamu, chungu au?

Je, ipo siku tutasema bora angebaki?
Kwa huyu sidhani [emoji23][emoji23][emoji23]
 
1.Baba akisema saa 1.00 jioni familia nzima inatakiwa iwe nyumbani,wanafamilia wote akiwepo baba wanakuwa nyumbani,sio mama kwa kuwa anajua baba hurudi saa 9 usiku naye anarudi saa saa 7 usiku ,na sio watoto kwa kuwa wanajua baba hurudi saa 9 usiku na mama hurudi saa 7 husiku na wao wakike na wakiume wanarudi saa 5 usiku,hiyo haijawahi kuwa familia.Ndio maana mpaka sasa hajakwenda nchi yoyote ya Ulaya na America au Asia anasimamia familia.

2.Ameweza kuwatia hatiani watu ambao walikuwa wanajiona wakubwa kuliko serikali wakina Seth + Rugamalila wa Dowans na kadhalika.

3.Ameweza kuamua kujenga Reli ya kisasa ambayo itawanufaisha watanzania wengi zaidi kuliko wanasiasa wafanyabishara wa mizigo na abiria ambao wasingekuwa tayari reli ya kisasa ijengwe kwani ingeondoa maslahi yao,vivyo hivyo kwenye elimu,afya nk

3.Magufuli hana mshipa wa aibu,ndio mana hata uwe mshikaji wake ukiharibu anakutoa hakuangalii usoni,ndio Rais anayeweza kuwa ametengua na kuteua viongozi wengi sana kuliko marais wote waliotangulia.

4.Rais Magufuli anaamini katika vijana,yeye alipata unaibu waziri wa Miundombinu/Ujenzi akiwa mbichi about 35 years of age kama kumbukumbu zangu zipo saw a,hivyo aliweza kuonyesha kipaji chake,Mkapa akampa Uwaziri na akamudu,na akaenda wizara tofauti akang'ara na hatimaye Rais wa nchi.Vijana wana matarajio makubwa,hawaogopi kukosea wanathubutu ndio namna pekee itakayotutoa hapa tulipo umri unaruhusu wakikosea kwa nia njema wasaidie nchi itakwenda.Nakuelewa sana,wazee waliopo kwenye utumishi wa umma sahivi wanaogopa kuthubutu kwa kuwa wanalinda kutoharibu wakakosa hata hicho kidogo walichowekeza kwenye utumishi kwa muda huo wote.

5.Watu wa aina yako ni nadra sana kupatikana,naamini kwa ulivyo makini utakua umeanza kuandaa succession plan kwa ajili ya atakayekuja baada yako,vinginevyo tutarudi tulikotoka.

6.Baba yangu mzazi jina lake la kwanza ni John ,ninajisikia fahari sana ninapoona John wa aina ya kwako,najisikia furaha kumpa mwanangu jina la john.

7.Naomba kwa Leo niishie hapa,huku mtaani wameshakuelewatunawahitaji akina Harmonize wengi zaidi ambao ni wa kweli wapo kwa ajili ya maslahi mapana ya nchi.
" Ni Mimi John jina la kati"
Senseless song from praise team
 
Magufuli atakumbukwa sana kuliko Julius Nyerere

Hatutopata Rais Serious kama Magufuli kwa karne kadhaa baada ya kuondoka kwake

Magufuli ni binadamu na ana madhaifu yake na hata mie huwa nampiga madongo sometime humu ila generally ni Rais Mzuri sana sana
 
Magufuli atakumbukwa sana kuliko Julius Nyerere

Hatutopata Rais Serious kama Magufuli kwa karne kadhaa baada ya kuondoka kwake

Magufuli ni binadamu na ana madhaifu yake na hata mie huwa nampiga madongo sometime humu ila generally ni Rais Mzuri sana sana


Usiaminishe watu ujinga.
 
Umesahau kuandika majina yako kamili pamoja na kuweka namba ya simu
 
Zitasikika sauti zikisema ,Bora Magufuriii aliiba ila tuliona nini anafanya .

Zitasikika sauti zikisema, Bora Magufurii alileta nidhamu kazini, alipunguza janga la rushwa.

Zitasikika sauti nyingi sana zikisema bora bwanaa yule alikua Dictator ila alitanguliza mbele naslai ya nchi kuliko yake binafsi.

"In mrisho mpoto voice"

Muda utasema .
 
  • Thanks
Reactions: nao
Back
Top Bottom