Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Wanakwambia siasa siku hizi hailipi. Yaani imekua kama enzi za Mwalimu. Wanasiasa walikua na kazi zingine za kufanya
 
Awamu hii inaweza kuwa ndio inaongoza kwa Rushwa kuliko iliyopita.

Awamu zilizopita angalau vyombo vya habari vilikuwa vina-report taarifa za ufisadi, ila wakati huu hiki tunachoita vita ya rushwa na ufisadi inapiganwa na watu wawili tu Rais na PM wadau wengine kama vyombo vya habari haviandiki tena.
 
Zamani vyombo vya habari vilikuwa huru kuripoti vya sasa vimepigwa solotepu kuzungumzia,jibu lako subiria awamu hii ipite ndo utapata tathmini.
 
The president of Tanzania is one of his kind and is been loved genuinely. His style of leadership is second to none in the SADC region and he is there to represent his people squarely and fair. He does not entertain corruption and with him, better drink Logo than stealing government resources which I think other leaders could have copied. His government is not reckless in spending money and to set an example to his people, he doesn't travel out side his country all to save government money.

And he only has 3 suits...
 
The president of Tanzania is one of his kind and is been loved genuinely. His style of leadership is second to none in the SADC region and he is there to represent his people squarely and fair. He does not entertain corruption and with him, better drink Logo than stealing government resources which I think other leaders could have copied. His government is not reckless in spending money and to set an example to his people, he doesn't travel out side his country all to save government money.

And he only has 3 suits...
 
Hayo ni maoni ya wazambia au ni yako wewe wa praise and worship team??
 
MATAGA bana! Mtengeneze wenyewe ki tweet hiki msingizie Wa-Zambia wamesema! Pumbav zenu!
 
Vyombo vya Habari vinaripoti. Rushwa imepungua Sana.
Takukuru inafanya kazi.
 
Wanabodi,
Kwa mtazamo wangu, kama mambo makubwa ya maendeleo yameweza kufanywa katika kipindi cha miaka minne tu ya utawala huu wa Awamu ya tano, basi kuna matumaini makubwa ya watanzania kuweza kufikia Maendeleo ya kweli miaka ijayo.

Nani alitegemea kwa vikwazo vilivyokuwa vinawekwa kwenye Ujenzi wa bwawa kubwa la kuzalisha umeme mto Rufiji; Stigglers gorge ingejengwa?

Nani alitegemea ununuzi wa Ndege na kufufua shirika la ndege vingewezekana Kwa sarakasi zilizokuwepo?

Treni ya mwendo kasi Tanzania..! Nani alitegemea haya?

Hospitali ni kitu muhimu sana kwa afya za wananchi..zinajengwa kila Wilaya na Kata..!

Nani alitegemea Elimu bure ingewezekana kwa uwingi wa shule nchini..?

Watumishi wabadhirifu hata wa kujilipa 1.5m kwa safari hewa wanaambiwa wazirudishe, nani alitegemea haya.

Barabara za lami nchi nzima..

Nchi hii ina hela ila tulikuwa tunaaminishwa ndivyo sivyo..

Watumishi huko mtaani wanasema "hela ya Magu hailiki, ni ya moto"
 
Nani alitegemea wanaomaliza vyuo hawataweza kuajiriwa kama kipindi cha Kikwete?
 
Mleta uzi ubarikiwe sana umesema ukweli mtupu japo watu wanajitoa ufahamu na kuwa mapunguani wa kujifanya hawaoni. Rais Magufuli ni mzalendo namba moja na juhudi zake za kulikwamua taifa hili kutoka katika mikono ya majangili mafisadi wauza unga wabadhilifu watovu wa nidhamu wafanyakazi hewa vibaraka wa mabeberu tunaziona tunazidhamini na tuko nyuma yake tunamuunga mkono. Wapinga maendelea wachimbe mashimo wajizike!
 
Hizi propaganda za kiwango cha chini sana haziiwezi washawishi watu kwenye akili
 
Hiyo train kutoka dar kufika morogoro km 300, tu shughuli yake. Pevu, mpaka mnamtuma DPP kuomba hela kwa mahabusu,

Mwanza km 1500 mtafika lini?
 
Sawa, CAG ndio wakutupa ufahamu wa matumizi sahihi ya pesa zetu. Tusubiri.
 
Pamoja na ajira ambazo zimekuwa zikitolewa kwa Awamu kulingana na maeneo yenye uhitaji sana..

Lakini bado ukweli utabaki pale pale kuwa ajira hutengenezwa, mkakati wa uchumi wa viwanda ulioletwa na kuanza kutekelezwa utatengeneza ajira nyingi..na hilo mi nadhani lililetwa kwa wakati sahihi kwa sababu:-

Enzi zile vyuo vilikuwa vichache, population ilikuwa ndogo, lakini kulikuwa na viwanda katika mikoa mbalimbali ambavyo vilikufa baadae kwa sababu mbalimbali.Hivyo kwa mazingira yale ilikuwa rahisi wahitimu wote kuingia kwenye ajira moja kwa moja, nakumbuka wengine walikuwa wakimaliza darasa la saba, kidato cha nne, Sita nk. Walikuwa wanaingia kwenye ajira moja kwa moja tofauti na Sasa.

Mazingira ya sasa ni tofauti kabisa ukilinganisha na kipindi kile..kipindi hiki population ni kubwa, vyuo vimeongezeka, wahitimu ni wengi;

Hivyo, Kiongozi wa nchi ama serikali yoyote makini lazima aje na mkakati mahsusi wenye suluhisho la kudumu la tatizo la ajira kama Magufuli alivyokuja na mkakati wa uchumi wa viwanda katika serikali ya awamu hii.

Unapoongelea uchumi wa viwanda unagusa mlolongo wa watu mbali mbali kwa sababu:-

viwanda vinahitaji Malighafi ambazo zitazalishwa na wakulima- ajira kwenye Kilimo,

Mali ghafi zinatakiwa zisafirishwe toka mashambani zinakozalishwa hadi viwandani- ajira ya usafirishaji

Viwanda vinahitaji wafanyakazi kukamilisha mchakato mzima wa utengenezaji bidhaa viwandani-ajira viwandani

Bidhaa zinatakiwa zisafirishwe toka viwandani hadi masoko zinakohitajika

Wauzaji wa jumla na reja reja- ajira wafanyabiashara
Nk.

Hivyo, unaweza kuona eneo la viwanda lilivyo na umuhimu Kuliko sekta nyingine katika kuzalisha ajira nyingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…