TUNAJIMWAMBAFAI KWA KUELEZA MAFANIKIO YAKUTUKUKA YA AWAMU YA TANO.
Leo 13:15pm,09/10/2019.
Awamu yako tuliacha kujimwambafai wapinzani wakawatangaza wanao kuwa ndio wenye pesa nyingi Tanzania,Wapinzani wakataja kila aina ya Ufisadi uliofanyika ukiwemo Ufisadi wa akaunti ya Escrow na Ufisadi wa Epa ambapo Mmarekani Balali aliidhinisha malipo ya dola Milioni 133 na kuchenchiwa hapa Tanzania.
Kuchenchiwa hapa Tanzania kwa malipo hayo ya dola 133 kulisababisha shilingi kuwa nyingi katika mzunguko wa pesa hapa Tanzania hali iliyosababisha shilingi kushuka thamani kwa asilimia 25% kwa tukio moja tu la Ufisadi wa Epa.
Huo ulikuwa ni wakati wako Mzee wangu sasa leo unasema tuache kujimwambafai ili wapinzani waanze kutunga maneno ya uwongo juu yetu! haiwezekani lazima tujimwambafai.
Wapinzani waliitaja awamu yako kama awamu ya watu waliojilipa pesa na kugawana kwenye visandalusi na magunia na kuita vijisenti na pesa ya mboga huku Watanzania wengi wakikosa Umeme,Giza lilitanda kwa Umeme wa mgao na wahuni wachache waliendelea kujenga Maghorofa na kuyamaliza ndani ya mwezi,Sasa leo tukiwa hatuna mgao wa Umeme na Mafisadi yakifungwa kwa nini tusijimwambafai!?
Wapinzani waliitaja awamu yako kama awamu ya watu wenye connection, wakisema wenye connection walijenga visima vya mafuta kila mtaa,Wakati wako mwanao ndio alitangazwa kuwa ndiye mwenye malori yote hapa nchini,wakati wako watu wakiguswa waliuliza "unanijua Mimi ni nani" Sasa leo tukiwa hatuna hao wahuni wanaouliza "Unanijua Mimi ni nani" kwa nini tusijimwambafai kuwa tumewashinda wahuni na kujenga Taifa lenye maadili na kuheshimiana.
Wapinzani waliitaja awamu yako kama awamu ya misheni town, misheni town walipanga na kupangishiwa mitaa ya Sinza na kwenye apartment Masaki na Mikocheni,waliamka saa nne asubuhi kunywa supu,wakarudi kulala hadi saa kumi na moja jioni wakijiandaa kukesha usiku,Misheni town aliomba elfu moja ya nauli asubuhi kwenda Bandarini pale Posta na jioni alirudi na milioni moja.Sasa kwa nini tusijimwambafai hivi sasa kwa kuondoa Taifa la watu wavivu na wezi wa mali ya Umma na kujenga Taifa imara kwa Maslahi ya Taifa zima la Tanzania.
Wapinzani waliitaja awamu yako kama awamu ambayo Twiga walipandishwa kwenye ndege kuelekea Ulaya na Uarabuni,Ujangili wa pembe za ndovu na meno ya tembo,Criminals aka Investors walitua na ndege migodini na kuondoka na dhahabu zetu bila Taifa kupata faida yoyote na madini ambayo ni Mali ya asili na utajiri pekee tuliopewa na Mwenyezi Mungu.Sasa leo kwa nini kwa nini tusijimwambafai kwa kuwashinda awa Criminals aka investors na kuzuia wizi wa madini yetu ili kulinufaisha Taifa la Tanzania.
Wapinzani waliitaja awamu yako kama awamu ambayo watu walipata kazi kwa vimemo,Watoto wa vigogo walitamba katika idara kubwa kubwa za Serikali na wanyonge wasio na connection waliishia kupata kazi kwa kunyanyaswa ama kupigia magoti vigogo au watoto wao,Sasa hivi leo tunapokuwa na Taifa lenye usawa,hata ukiwa kijijini ukiomba kazi unapata,kwa nini sasa tusijimwambafai!?
-Tuhuma na Kashfa za Ufisadi vilishinda kujimwambafai kimaendeleo.
Awamu yako wapinzani walipata kiki ya kisiasa kwa ajenda za kashfa hizi saba,
Mabilioni ya Jk: Awamu yako zilitoka Sh50 bilioni kukopesha wafanyabiashara kuendeleza biashara zao, lakini sehemu ya fedha hizo hazikurejeshwa na hakuna hatua zilizochukuliwa.
Sakata la Rada ulilolirithi: Ni kashfa ya ununuzi wa rada ya kuongoza ndege kutoka Kampuni ya Bae System, Uingereza mwaka 2011. Sh73 bilioni zilirejeshwa kama chenji ya rada, lakini waliohusika hawakuchukuliwa hatua yoyote.
Sakata la Meremeta: Zaidi ya Sh205.9 bilioni zilipotea kupitia mkopo wa Kampuni ya Meremeta iliyokuwa ikimilikiwa na Jeshi na baadaye kufunikwa kuwa ni suala la kiusalama.
Sakata la Escrow: Hii iliibuka 2014 baada ya Sh306 bilioni kuchukuliwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika Akaunti ya Tegeta Escrow. Waliochota fedha hizo kupitia benki ya Stanbic hadi hawakukamatwa katika awamu yako,Walikamatwa katika awamu hii ya tano,sasa kwa nini tusijimwambafai juu ya kukamatwa kwa wezi wa Mali ya Umma.
Kashfa ya kagoda: Katika kashfa hii Sh40 bilioni zililipwa na BoT kwa Kampuni ya Kagoda Agriculture kwa madai ya kufanya kazi za usalama,lakini akili za kuambiwa ongeza na za kwako.
Sakata la Epa: Sh133 bilioni zilichotwa kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) BoT. Wachache walifungwa na wengine kusamehewa baada ya kurejesha fedha.
Sakata la Richmond: Mwaka 2006 mitambo ya kufua umeme ilikodishwa kwa Richmond, mkataba ukahamishiwa Dowans na baadaye kuvunjwa, mabilioni ya umeme yalilipwa na fidia, lakini wahusika hadi leo hawajulikani na kama si awamu hii ya tano basi tungeendelea kulipa mibilioni hadi leo,Sasa kwa nini tusijimwambafai!?
-Kwa nini tunajimwambafai katika Awamu hii ya tano.
Awamu ya tano ina miradi mingi nchi nzima,miradi inayoonekana kwa macho na sio miradi hewa ama ya kitapeli kama miradi tuliyowahi kuisikia siku za nyuma,Miradi inayofanyika sasa na inayoonekana wazi na Wananchi wanapata faraja,ni miradi ya barabara nchi nzima,meli,vivuko,umeme,maji,afya,utalii,bandari,na viwanja vya ndege,Siku za nyuma tulikuwa tunaambiwa maneno tu ama kuishia kuona ujenzi usioridhisha.
Awamu ya tano ilianza kwa vitendo na watu waliita nguvu ya soda,lakini siki zilivyozidi kwenda watu waligundua si povu wala nguvu ya soda bali mtendakazi yupo kazini.Ujenzi ulioanza na kumalizika ulitoa picha ya utendaji wa kutukuka katika awamu hii ya tano,Mwaka 2016 tulianza kuona matunda halisi ya maneno,ahadi na utendaji kazi wa Awamu ya tano.
Hostel za Chuo cha UDSM.
Hostel za Askari Magereza.
Ununuzi wa Ndege 2 (Nyingine 3 zikaja ndani ya Mwaka huo huo wa 2016).
Ujenzi wa Flyover Tazara na Ubungo
Upanuzi wa Airport Mwanza
Upanuzi barabara ya Moroco Dar es Salaam.
Upanuzi wa Kisasa Airport Dar
Kukomesha Rushwa
Kurejesha nidhamu Makazini.
-Mwaka 2017 kazi iliendelea kwa kasi zaidi na tuliona ujenzi mkubwa miradi mbalimbali ukianza.
Uzinduzi ujenzi wa reli kwa ajili ya treni ya Umeme.
Ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba
Kukomesha Watumishi Wenye Feki hivyo kuokoa Mabilioni ya Fedha.
Barabara ya kuunganisha Wilaya za Kibondo kigoma Kaliua huko Tabora.
Miradi Mikubwa ya Maji,Dar,Morogoro,Dodoma,Kigoma,Tabota,na Shinyanga.
Uwezeshaji Ujenzi Bomba la Mafuta kutoka Hoima mpaka Tanga.
Kwa kweli tunajimwambafai katika awamu hii ya tano kwa kuwa imefanya makubwa sanaa.
Kila upitapo sasa hivi ni ujenzi unaendelea.
Dar es Salaam kila kona Barabara ya Tandale-Sinza- Mawasiliano barabara imejengwa,Mitaa ya Kinondoni hivi ina lami,Ubungo Interchange inajengwa
Madaraja yanajengwa
Upanuzi wa barabara kuu ya Ubungo hadi chalinze unafanywa kwa kiwango cha barabara nane.
Daraja Kilombero miaka yote wapigaji walikuwa wanakula hela za wananchi kuwavusha ila sasa limejengwa
-Flyovers zinajengwa pamoja na barabara za ziwani na baharini.
Miradi ya umeme inajengwa na miradi mingi ni kwa hela za watanzania wenyewe,Miradi wa Umeme wa Gas wa Kinyerezi,na mradi wa Bwawa la Umeme la Rufiji (Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere)
Miaka yote maeneo ya Mbezi na kimara walikuwa hawapati maji japo yanapita njia hiyo hiyo lakini sasa maji yamefika mbezi, na bado wanaendelea kutandaza mabomba ili kupeleka maji.
Awali waliokuwa wanakula hela za wananchi ni wenye miradi ya kuuza maji kwa magari. Ila sasa wananchi wamekombolewa.
Utendaji kazi umeimarika, sasa hivi kila mmoja anaona cheo akipewa ni kama kakalia kaa la moto.Yale mambo ya kupiga hela na kukaa ofisini kupiga usingizi yameisha watu ni kazi la sivyo unawajibishwa.
Madawa sasa yanapatikana hospitali, ile hali ya madawa ya hospitali yanapelekwa katika Pharmas binafsi imeisha.
Hospitali sasa za serikali ukienda mgonjwa anajaliwa sio kama ilivyokuwa awali.
Taasisi za serikali wafanyakazi wamekuwa wanawajibika,hakika nidhamu imeimarika.
Kwa sasa taasisi za serikali zinajiendesha kibiashara na si kihasara kama ilivyokuwa awali, ilikuwa ni ulaji tuu wa hela, upigaji dili, taasisi zinakufa, hakuna gawio kwa serikali, ila sasa zinatoa gawio.
Hakika kila kitu ni usimamizi imara, ukicheka na kima utavuna mabua.
Awali watu walikuwa wanaulilia uongozi, hata wasio kuwa na elimu walikuwa wanagombea kupata uongozi, sasa uongozi umekuwa mgumu sababu kama wewe si muwajibikaji una ndoto za kupiga tuu, hupati nafasi, Uongozi umekuwa una hadhi kwa sasa.
Nimalizie kwa kusema,tunajimwambafai kwa kuwa awamu ya tano imeitendea haki Tanzania na Watanzania kwa ujumla,
Mungu Mbariki Rais wetu John Magufuli,Mungu ibariki Tanzania.
Nikiishia hapa,Mimi ni,
Msemakweli Chakubanga.
Dar es Salaam.
0755078854.