Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania


Kwani mpango wa Umeme Vijijini alianzisha Magufuli? Kwani umeme vijijini umeanza kuwaka wakati wa Magufuli tu?

Jamani hata kama kupongeza ni ajira za watu au propaganda za uchaguzi basi mkumbuke japo kidogo kuwa Watanzania nao wana akili za kuoana, kujua ukweli, na kutunza kumbukumbu.

Yaani kusifia hadi inakera!! Mbona hii nchi inafanywa kama tumepata uhuru mwaka 2015 chini ya uongozi imara Magufuli? You guys suck!! Get a job..

Simple FACT
 
"Mheshimiwa Spika;
Katika kipindi hiki tuliunda Wakala wa Umeme Vijijini (REA) ambao wamefanya kazi kubwa na nzuri ya kusambaza umeme kwa vijiji 5,336 kati ya vijiji12,423 nchini. Kazi kubwa iliyofanyika vijijini inapochanganywa na ile ya mijini imeongeza idadi ya Watanzania wanaopata umeme kutoka asilimia 10hadi asilimia 40 mwaka 2015. Uamuzi uliofanywa katika Bajeti ya mwaka huu wa kukusanya fedha kwa ajili ya umeme vijijini kupitia mafuta ya petroli, utasaidia sana kuongeza kasi ya kusambaza umeme vijijini"

Hotuba ya Jakaya Kikwete kuaga na kuvunja bunge 2015

12423-5336=

5336x100 = 42.95%
12423

Kwa hiyo aslimia 43% ya vijiji TZ vilikuwa na umeme

Hizi takwimu wanazotoa Sasa wanazipata wapi?
 
Umesahau Magufuli alipowaita wakandarasi wanaohusika na REA na kuwapa assuarance ya kuwa fedha ipo waendelee kuchapa kazi??
Fedha za MCC tulinyimwa ila mzigo umepigwa...hii ndio Serikali Kamili na Sio Serikali lemavu
 
Uyo punda wa lumumba ni tahira hana alijualo
 
Nasubiri akujibu hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tafsiri ya Vijiji kupata umeme ina utata mkubwa sana.
Umeme unafika katika Kijiji chenye Nyumba 400, nyumba 20 zinafungiwa umeme, sawa na asilinia 5 (tano) ya nyumba, kisha Serikali inatangaza kuwa Kijiji kina umeme.
Asilimia 95 waliobaki, ambao wote wanataka umeme, wanaambiwa Vifaa na MITA zilizoletwa zimeisha.
Ukiwafuata Tanesco, gharama unazoambiwa ili uunganishiwe umeme, ni tofauti na zile zinazotangazwa, ambazo ni Shs. 27,500/-.
Vi vema Tanesco itoe tamko kuhusu hali hii.
Wakati huo huo ni vema na haki kuisifia Serikali na Tanesco kwa kufikisha umeme sehemu nyingi sana.
 
Mkuu hizo ndio kero ndogondogo zinazotakiwa kusemwa ili Serikali ifuatilie kwa ukaribu...kuna baadhi ya maeneo siasa za kubishana zinapelekea miradi isimame..kuna maeneo mengine wanaiba miundombinu.
 
Hata kama kuna miradi au asilimia ya waliopata umeme imeongezeka lakini takwimu ziwe za kweli. Umeme umeanza kuwekwa tangu awamu ya nne. Kama kuna ongezeko sawa lakini haya mambo ya haijapata kutokea yanachosha. Mie nakaa Dar lakini cha ajabu nilipo hakuna umeme. Tunatumia sola. Niko ndani ya mipaka ya jiji la dsm. Hatuna umeme. Haujaletwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mjomba CCM ni moja juzi ,jana na leo.
Upo Dar mtaa gani?
 
Uongooo wa kiwango cha dunia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akikujibu nitag ndugu
 
Kweli vijiji vingi vimepata Umeme na umechochea maendeleo ya kiuchumi na huduma za jamii. Lakini nashawishika kuamini kuwa tafsiri ya kijiji ni makao makuu ya kijiji na dhana ya usambazaji wa umeme ni kufika makao makuu ya kijiji lakini si pembezoni mwa kijiji. Itakuwa vyema baadaye huduma ipanuke kujumuisha walio pembezoni tusijenge tabaka za kiuchumi vijijini. REA ingia ndani vijijini ambako watu wengi wanatumia mafuta ya taa na kuni kwa mwanga.
 
Una maanisha ngazi ya vitongoji??
 
Umesahau Magufuli alipowaita wakandarasi wanaohusika na REA na kuwapa assuarance ya kuwa fedha ipo waendelee kuchapa kazi??
Fedha za MCC tulinyimwa ila mzigo umepigwa...hii ndio Serikali Kamili na Sio Serikali lemavu

Tatizo mnapoyosha kusema Magu ndiye kaweka umeme 73% sio kweli. MCC waliweka uwewe na kuvuta sehemu nyingi sana tunawaacha kama vile hawajafanya kitu kisiasa! Uhusiano mzuri wa Kikwete na Bush ndiyo ulichangia hili. Hapa hatutaki uongo tu ndiyo ombi kuwa mkweli
 
Asilimia 95 ya takwimu za serikali ya Jiwe ni za kupika.
Si mnakumbuka walivyoshushuliwa na Benki ya Dunia kuhusu takwimu zao za ukuaji wa uchumi hapa nchini?

Usiamini takwimu zao hata siku moja. CCM ni wapenda sifa, waongo na vizabizabina.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…