Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

TUNA IMANI NA MAGUFULI 2020 - 2025 [emoji1241][emoji818][emoji818][emoji818][emoji818][emoji818][emoji818][emoji818]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi marais waliopita wote hakuna walichofanya kwenye umeme? Maana ukisema asilimia 73 ya vijiji vimewekwa umeme kipindi cha jiwe inamaanisha kabla ya hapo kulikuwa hakuna kijiji chenye umeme. Bora ungesema asilimia 73 ya vijiji vilivyokuwa havina umeme labda ungeeleweka
 
jingalao,
Kutokana na ugumu wa maisha mwananchi huyo huyo anakula milo miwili kwa siku, sasa hivi atatakiwa kulipa bili ya umeme. Na kwa kipato chake inawezekana kula mlo mmoja ili aweze kulipa bili. Hapo itakuwa umemuendeleza ama ndio umempoteza kabisa? Ni kweli umeme unaweza kuzalisha ajira, lakini je ni kweli wanakijiji wote wanaweza kuwa wauzaji wa juisi ya ukwaju? Nani atakuwa mnunuzi? Ni vyema serikali ingeliangalia tatizo la ajira kwa upana zaidi ili inapopeleka suala lenye kuhitaji kipato kuliendesha lisiwe mzigo kwa jamii.
 
Mkuu hizo ndio kero ndogondogo zinazotakiwa kusemwa ili Serikali ifuatilie kwa ukaribu...kuna baadhi ya maeneo siasa za kubishana zinapelekea miradi isimame..kuna maeneo mengine wanaiba miundombinu.
Jingalao, kuna ibilisi aitwaye 'ubaguzi' ananyemelea nchi yetu.
Ibilisi huyu anawaaminisha baadhi ya Watanzania kuwa kuna 'wao' na kuna 'sisi'.
Kauli uliyotumia ya 'kuna baadhi ya maeneo siasa za kubishana zinapelekea miradi isimame' ni kauli potofu, inayoashiria kuwa ndani ya nafsi yako, unazo chembechembe za ubaguzi, ambazo ni budi zikemewe.
Miradi ya umeme haina 'siasa za kukubaliana' wala 'siasa za kubishana'.
Waziri Dr. Medard Kalemani ni shahidi.
Sana sana kilichopo ni ufisadi ambao chanzo chake ni Wasimamizi wa REA kudai rushwa ya asilimia 10-30 kutoka kwa Wakandarasi, ambao wanalazimika kupunguza vifaa ili Watendaji hao wa Serikali wapate rushwa yao.
Kama asemavyo Rais Magufuli siku zote, anayeumizwa na rushwa ni Mtanzania masikini.
 
Heshima kwenu wa JF.

Sio mwepesi sana wa kusifia ila leo naomba niandike kidogo. Kwa vipindi tofauti nimetembelea wilaya ya Makete na kushuhudia usumbufu wa usafiri uliopo kwenye barabara ukitokea Njombe mjini. Mwaka huu kwa Mara nyingine nimetembelea na kuona juhudi za Rais wetu Daktari Mheshimiwa John Pombe Magufuli kwa kuhamisha milima na kusawazisha mabonde na kisha kuwakamilishia ujenzi wa rami watani zetu Wakingaa

Ama kweli Mheshimiwa unastahili pongezi kwa jitihada zako za kuwajali wanyonge na Maskini, Binafsi namfananisha Mheshimiwa kama yule mtu aliyekuwa anazungumziwa kwenye biblia kwamba ukiwa na imani kama chembe ya haladani, unaweza kuhamisha mlima.

Hiki ndio ninachokiona kwa Mheshimiwa Rais wetu,kweli unastahili pongezi kwa jitihada unazofanya za kuwajali wanyonge.








Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo barabara ilikuwa korofi sana. Kama imetengenezwa italeta mapinduzi makubwa ya usafiri kwa hayo maeneo
 
Tuko nyuma Sana kitechnologia ukiwezapata kuni si tayari ushaupata umeme,hapa ni suala tu la sido na veta kusambaza technology watu watumie kuni na mabaki ya mazao mfano pumba za mpunga,maranda ya mbao,mavi ya ngombe wajitengenezee umeme wapate mwanga na kutumia kwa mashine mbali mbali
 
[emoji828]Twiga walipandishwa ndege

[emoji828]Ujambazi ulishamiri

[emoji828]Watumishi wa Umma walikuwa wanakwenda kazini muda waliotaka wao

[emoji828]Tenda walipeana kindugu

[emoji828]Wanaopambana na kuzuia rushwa ndio waliokuwa vinara wa kupokea rushwa

[emoji828]Huduma muhimu za kijamii zilikuwa hazijafika kijijini kwetu(Maji safi ,huduma za afya, umeme)

[emoji828]Shirika la ndege (Atcl) lilikuwa shimoni

[emoji828]Vitendo vya hujma vilishamiri sana

#Asante JPM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CCM ndiyo iliyotufikisha huko kwani na yenyewe ilikuwa ikichota mabilioni kwenye mashirika ya umma kwa maagizo na bila maandishi, ilipiga kisawasawa! CCM nuksi.
 
Katiba inamruhusu kuwepo hapo si kujipendekeza. Ndiyo maana hata alichoongea si mapambio kama wengine.

Vipi je katiba haimruhusu Magu kujisifia??
Kweli wivu na roho korosho vinampa mtu upofu [emoji853][emoji853]
 
Wana Jf.

Anayeweza mpe sifa yake, yule mtu asitumaniwa na akaweza kuwa si mwingine bali Rais Wetu Dr. J. Pombe ambaye amebadirisha mji kutoka kuwa tambalale na kuufanya uwe na milima.

Ukitoka pugu kwenda mjini utakutana na mlima Mfugale, kabla ya kufika mjini kuna mlima mwingine maeneo ya gerezani bado haujapewa jina.

Ukitoka manzese kuelekea morogoro kuna mlima mwingine mkubwa zaidi ambao wadaku walidhani ni ndoto kuwepo.

Yote kwa yote Jogoo la Shamba limewika mjini wana miji wameshikwa butwaa.
 
Kumbe ndiyo maana wazee wa CCM na zitto wanamwita mshamba, sasa wewe umeongezeka, aisee
 
Kumbe ndiyo maana wazee wa CCM na zitto wanamwita mshamba, sasa wewe umeongezeka, aisee
Ni maana ya mshamba? Mshamba ni yule mtu aliyezaliwa kijijini akakulia kijijini mjini akaletwa na Serikali kusoma shule mbali mbali akawakuta wenyeji wasiojua lolote na kuwapa somo la maisha ya kimkakati.

Mtoto wa mjini ni yule mtu mwaribifu anayeishi kwa ujanja ujanja, ujanja ukizeeka asipokuwa omba omba atakuwa tapeli wa kutupwa.

Lakini mshamba ni mzalisha mali anayetefemewa ili wamjini aishi. Bila mshamba mtoto wa mjini lazima achungulie umauti maana ana namna. Zitto ajui alifanyalo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…