Salam wakuu,
To cut the story short, mheshimiwa JPM kiukweli anajitahidi sana kuleta maendeleo katika nchi yetu. There reaches a time inabidi kuweka Mambo ya kisiasa kando na kumuunga mkono Mh. Kiongozi wa watu katika harakati za kuendeleza maendeleo ya nchi yetu tusogee zaidi kuliko hapa tulipofikia.
Jana niliweza kupita pale shule ya mfano (Dodoma), aisee kama hii shule ikikamilika na kila mkoa na wilaya ikajengwa shule Kama hii basi tutakua tumepiga hatua kubwa Sana. Wapo watakaobeza kwamba shule sio majengo na kusahau kwamba huko dar itabidi wanafunzi wanaoingia kidato Cha kwanza wasome kwa shift ( can you imagine?).
Zikijengwa shule Bora Kama hii ya mfano ambayo unaambiwa kwamba itakua kuanzia darasa la kwanza hadi form six, kutasaidia kutoa ajira kwa walimu wazalendo na kuleta hamasa kwa wazazi kua shule bora sio za private tu, hata za serikali zinaweza kua Bora.
Mungu ibariki Africa, Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki Magufuli