Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Manabii wa kweli walikuwa wanasema jambo kabla halijatokea na kuwapa watu wao njia za kujikinga na wakaponywa, huyu nabii wako wa uongo alituambia Corona hakuna imeisha kwa maombi halafu baadae alivyoona hali inazidi kuwa mbaya akasema ipo kidogo tu.
 
Labda useme ni "Pharao (Mfalme)" wa zama hizi, ila sio "Nabii" wa zama hizi.

Nabii gani anahamasisha wananchi wasiogope usalama wao kwani mungu anawalinda, wakati yeye mwenyewe analindwa kwa mitutu ya bunduki na makomandoo. Ina maana haamini yeye binafsi katika ulinzi wa mungu???
 
Mwambie Nabii Jiwe aturudishie maiti za watu wetu kina Ben Saanane, Azory Gwanda, Kanguye kama kawaua ili tuwazike kwa heshima ndugu zetu.

Kama ni madaraka alishapata.
 
Mpelekeni hospitali aombee wagonjwa wapone muokoe budget ya wizara ya afya.

MATAGA ni wajinga wa nchi.
 
kuna aina mbili za manabii: manabii wa uongo na manabii wa ukweli.
 
Unajua umeandika ujinga ndo sababu ukajua utapondwa tu
 
Magufuli umemaliza yote Sasa limebaki moja tu suala la ajira fanya mipango vijana waliosoma Wapate nafasi nakushuru Sana kulinda soko la ndani shikilia hapohapo Tanzania tunaweza kuzalisha bidhaa zetu wenyewe tukauziana sisi kwa sisi..zingine ambazo hatuwezi kuzalisha Basi tuagize mataifa wafanye biashara ila sio kutuingilia siasa zetu sisi Ni nchi huru.ulale mahali pema muamar Gaddafi Simba wa africa.
 
Kwani raisi awezi kujiuzuru??
Au katiba hairuhusu raisi kujiuzuru akiona mambo yamemshinda??
 
Pamoja na kutofautiana kwenye namna ya kupambana na majanga ikiwemo covid-19/21,Raisi MAGUFULI ni Raisi mfano wa kuigwa katika kutambua uwezo wa Waafrica,Total independence na Namna ya kujitawala kwa kufuata misingi yetu ya kiafrica...Nina uzi wa kupinga namna MAGUFULI anavyopambana na Covid-19 tofauti na taratibu za ki_dunia,lakina ni alama ya Uhuru wa kweli na kujitambua kama ngozi nyeusi,kujitawala na kujitegemea .HUYU ATAKUWEPO KWENYE HISTORIA YA VIZAZI VYENU VYOTE MPENDE MSIPENDE
 
Back
Top Bottom