Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mimi siwezi kumuombea kwa sababu akibarikiwa hata malaika wanaweza kukubaliana na ombi lake La kuja kufungia mitandao ya kijamii kama alivyotamani malaika wafanye. haya maombi yatafanywa na wanalumumba walioshikiwa akili
 
Amina
 
Tuwe tunafikilia vyakuandika yani tumuombee MTU anayefanya maisha yanakua magumu alafu bila aibu unasema tumuombee
 
Kabla hujatoa kibanzi katika jicho la mwenzio ni vyema ukatoa boriti lililoko katika jicho lako. Usihukumu usije ukahukumiwa.
 
adui mkubwa wa raisi ni katiba mbovu isiyoendana na wakati huu
 
Mimi siwezi kumuombea kwa sababu akibarikiwa hata malaika wanaweza kukubaliana na ombi lake La kuja kufungia mitandao ya kijamii kama alivyotamani malaika wafanye. haya maombi yatafanywa na wanalumumba walioshikiwa akili
Je mwanao akinyea kiganja cha mkono wako mmoja utakikata ukitupe?
 
Kabla hujatoa kibanzi katika jicho la mwenzio ni vyema ukatoa boriti lililoko katika jicho lako. Usihukumu usije ukahukumiwa.
Mbona hata wewe umehukumu unamaana gani unaposema"Kemea maadui wote wenye hila ambao hawataki afanye mazuri"Je unawafahamu watu hao?
 
Tuwe tunafikilia vyakuandika yani tumuombee MTU anayefanya maisha yanakua magumu alafu bila aibu unasema tumuombee
Hata Musa alipokuwa anawapeleka wana wa Israel katika nchi ya ahadi walimlaumu sana, lakini mwisho wa siku Musa hakuikanyaga. Sasa najua haya mazuri mnayoyaita mabaya kwa sasa anayoyafanya Rais wetu mpendwa JPM baadaye nyie ndo mtayafaidi na watoto wenu.
 
Kwani Rais ni mgonjwa hadi tumuombee afya njema au hana busara tumuombee busara kuna haja gani ya kuomba vitu wakati unavyo je wale wasiokuwa navyo wafanyaje?

Huu nao ni ufisadi mimi sijasikia kama Rais wetu kakosa hivyo vitu unavyotaka tumuombee.

Jifunze vya kuomba kwa Mungu si kila kitu unaomba iko siku utaomba Mungu akuogeshe sababu we kila kitu unaomba
 
Mbona hata wewe umehukumu unamaana gani unaposema"Kemea maadui wote wenye hila ambao hawataki afanye mazuri"Je unawafahamu watu hao?
Adui anapaswa akemewe. Mungu kwa kupitia Roho mtakatifu ametupa mamlaka ya kumkemea adui anayepinga kazi zake. Hiyo sio hukumu.
 
Je mwanao akinyea kiganja cha mkono wako mmoja utakikata ukitupe?

yote yanawezekana ukiamua. kama akili ikikutuma ukate utakata. lakini pia unaweza kumuwekea hats sharti LA kumnyima chakula au zawaidi nyingine iwapo hatanawa kwa Mani na sabuni. kwa kuwa huyu naye anawaza kuniziba mdomo ninachofanya hapa namuombea asifanikiwe kwa anayotaka kufanya na nina imani kuwa maombi yangu yatafanikiwa
 
Maandiko yasema Yatupasa kuomba kila wakati.
 
Maandiko yasema Yatupasa kuomba kila wakati.
Tatizo si kuomba jua nini cha kuomba ndio maana nilikwambia unaweza kukesha ukiomba Mungu akuogeshe

Elewa NENO si unasoma bila kushirikisha ubongo YESU aliyesema kuomba kila wakati but hata yeye hakuwa anaomba kila wakati kuna muda alienda kupiga story kuna muda alikuwa anafanya kazi nyingine
 
Adui anapaswa akemewe. Mungu kwa kupitia Roho mtakatifu ametupa mamlaka ya kumkemea adui anayepinga kazi zake. Hiyo sio hukumu.
Kwahiyo kwa akili yako Magufuli ni Mungu mana si ndo anayepingwa na adui kulingana na uzi wako?
 
VIP Leo atasali wap?maana RC,KKT,angikana ,msikitini,kanisa la lusekelo tayari ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…