Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Magufuli anatenda kazi yake pasipo kufuata Ilani Ya ccm. Hivyo nawaomba wanasiasa mkae pembeni Hakuna Ujomba WA urafiki WA kinafiki Ktk utendaji WA Hii team Mpya. Mliozoea mteremko Kwa Mkwere ntakiona safari Hii.
 
Wanajamvi igweeeee

Wakati Mkulu anaanza walisema rimoti ipo msoga na Tv ipo Magogoni... sasa nawauliza wale waliyasema hayo je hiyo rimoti bado imeshikiliwa???
*************************
Mnapozungumza muwe mnaweka akiba ya maneno!!
 
Huyu ndiye Daud ambae watazania walimlilia Mungu awape...na sasa utawala wa Sauli umekufa..Daud yuko ikulu.
 
tutampima kwa matokeo kama vifaa vya kutosha mahospitalini, madawa ya kutosha, wafanyakazi wa kutosha hasa elimu na afya, vitendea kazi vya kutosha mashuleni, wanafunzi wenye sifa elimu ya juu wote wanapata mikopo, barabara nzuri, maji salama, umeme wa uhakika, uchumi wa mtu mmoja mmoja umekua n.k hatutampima kwa ziara maofisini
Hapa kazi tu.
Matokeo hayo hayatakuja kama muujiza ndugu.. Kama kiongozi hizo ziara za maofisini ni sehemu muhimu ya kazi zake. Viva J.J.P.M. Tanzania's dream president !
 
Wakati tuki furahia haya ya nagufuli , tuna muomba amalize ya zanzibar maalim aapishwe amsaidie naye aondoe uoza huko znz..seif hataki mzaha na kazi ...mpe haki yake Tanzania kwa ujumla ibadikike

Crabat!! Seif!! As prezidaa of....znz. No... re election first
 
Magufuli rais wetu inabidi awekewe ulinzi mkubwa na mkali. wako watu wamekaa mkao wa kutaka kuhujumu kila kitu..

Yaani wakimgusa patachimbika,nchi haitawalika tena! Tumempata kiongozi huyu katika mazingira magumu sana,rundo la watu waliitaka hii nafasi sasa iweje wao watuzulumu!
 
Wanajamvi Nina kaswali ila kananitatiza naombeni majibu kwa hiyari
HIVI MAGUFULI ANAENDA KILOMETER NGAPI KWA SAA MANA NASHINDWA KWENDA NA HII SPEED YAKE.?????
 
Wakenya wanatamani Magufuli awe raisi wao?Mwambie wabadilisha Uhuru Kenyata aje tanzania na huyu Magufuli aende kuishi huko kenya kwa sababu siyo chaguo letu .

labda wewe tu sio chaguo lako! lkn usiwachanganye nawengine wenye mapenzinaye,sema hivi- SIO CHAGUO LANGU tutakuelewa
 
yale majipu anayoyakamua rais ukawa aka nyumbu wanadai eti ndio ilani yao wakati wao wanalojipu ambalo linataka likamuliwe.
hata ilani yao hatujaiona wanazungumza kwenye midomo.
 
yale majipu anayoyakamua rais ukawa aka nyumbu wanadai eti ndio ilani yao wakati wao wanalojipu ambalo linataka likamuliwe.
hata ilani yao hatujaiona wanazungumza kwenye midomo.

Mahakama ipi wameenda kudai hivyo..?
au ndio kusema umekurupuka toka
usingizini ukaangukia kwenye key board
na kuanza kuandika madudu madudu kama haya
uliyoandika katika uzi wako.
 
nyumbu wanaweweseka kasi ya jpm inatisha...wameamua kusema anayoyatekeleza ni ya kwao hawana hata soni...

watumbue jipu lao kwanza ndio waje kidandia gari la jpm
 
yale majipu anayoyakamua rais ukawa aka nyumbu wanadai eti ndio ilani yao wakati wao wanalojipu ambalo linataka likamuliwe.
hata ilani yao hatujaiona wanazungumza kwenye midomo.
Prof Kitila Mkumbo alisema kwa kasi ya rais Magufuli UKAWA hawatakuwa na hoja tena. Na sasa tumeanza kuyaona. Kila hatua anayochukua rais UKIWA wanalalamika kawapora sera. Pathetic!!
 
12295298_779916805453557_2181181547340056272_n.jpg
 
Wanajamvi Nina kaswali ila kananitatiza naombeni majibu kwa hiyari
HIVI MAGUFULI ANAENDA KILOMETER NGAPI KWA SAA MANA NASHINDWA KWENDA NA HII SPEED YAKE.?????

mkuu swali lako mbona simple sana kujibiwa,km150 kwa saa ni zaidi ya cheetah
 
Back
Top Bottom