Tanzania nchi yangu... nakupenda sana..!! Nikifa nitazikwa ktk udongo wa nchi yangu pendwa Tanzania
Jamani, vitu vingine ni mzaha na maigizo... nakubali kuna ukomandoo etc etc...!!!
Hivi, TOFALI LA CEMENT, mm nitengeneze, nikuletee, ww hata uwe Comandoo wa wapi, UPIGE KICHWA KIMOJA TU, TOFALI LINAPASUKA KATIKATI...!!! Na kichwa cha komandoo safiiiiiiiii... hata kamasi hakuna..!!... alafu watu wanashangiliaaaaaaa...kama mazingaombwe vile...!!!  alafu ndio moja ya kitu cha kuadhimisha sherehe ya UHURU...??? Kupasua tofali kwa kichwa..!!?
Hivi tokea lini tutakuwa ktk zama za gizaaa...!!! Huu uongo jamani.. maigizo...!!
Magufuli, Mungu akulinde baba, sikukupa kura yangu, ila UMEUFANYA MOYO WANGU UKUOMBE RADHI....futaaaa futaaaaa haya maigizo, giza, na kupoteza billions bureee..
Au kama kuna mtu anasema ataweza PASUA TOFALI KWA KICHWA aseme humu, nije na TOFALI LA CEMENT.. ukipasua mara moja, ntakulipa kila mwezi tshs 1,000,000 ktk maisha yako yote duniani...!!!
Mungu watu wako WANAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA..!!