nyumba kubwa
JF-Expert Member
- Oct 8, 2010
- 10,309
- 8,379
Nasikia huko TRA mapato yanaongezeka kwa kasi ya ajabu....
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbona mimi sioni la ajabu ambalo Magufuli kafanya mpaka hivi sasa..?
Habari za matumizi mabaya ya pesa za walipa kodi na kutokuwa na vipaumbele vya maana ni jambo ambalo wengine tumelipigia kelele sana humu tokea JF ianzishwe miaka karibu 10 iliyopita.
Tumepiga sana kelele humu kuhusu watoto kukaa chini, kuhusu wagonjwa kulala chini, kuhusu aibu ya uwanja wetu wa ndege na kuhusu mengineyo mengi tu.
Tukahoji matumizi ya mabilioni ya shilingi yaliyotumika kwenye sherehe za miaka 50 ya uhuru huku madaraja yakiporomoka kwa kuzidiwa na mvua.
Halafu kuna wengine humu wakawa wanatetea huo ubadhirifu wa CCM kwa nguvu zao zote. Halafu leo hii wanajifanya ndo wapiga vuvuzela wa Magufuli.
Inastaajabisha kweli.
Mtu yeyote mwadilifu na mwenye common sense hatashangazwa na anachofanya Magufuli. Lakini, lazima angeshangazwa na jinsi serikali za CCM zilivyokuwa za kipumbavu maana hizo ndizo zimetufikisha hapa tulipo.
Siyo wa kwanza Bwana wako wengi Thomas Sankara mmoja waoNdio rais wa kwanza wa nchi ya Kiafrika kubana matumizi,si unajua tena sisi Waafrika ni maarufu kwa kutumia sana huku nchi zetu zikiwa dhohofu bin hali?
Muungwana atakemea maovu na atasifia mema. Sasa wewe muungwana gani unajua kukemea tu maovu halafu hujui kusifia mema???!!! Mi hata sikueelewi
JPM has made the impossible become possible.
Congratulations Mr President, Sir.
Rais Magufuli anashangaza dunia kwa sababu hiki anachokifanya sio kawaida ya watawala (viongozi?) wengi wa Afrika.Watawala wengi wa Afrika ni wezi wakubwa na wapenda matanuzi na anasa.Wengi wana kaliba ya Mfalme Nebukadreza.Mfano Dos Santos wa Angola,Ali Bongo wa Gambia,Jacob Zuma wa SA n.k.
Ila jamani tujiulize, what the hell was Kikwete doing all of these years katika utawala wake? Tafadhali raisi wetu Magufuli mkamate huyu mtuhumiwa pamoja na kibaka mwanawe (Mze wa Makontena ya China).
Kama unachosema ni kweli basi Waafrika tuna matatizo makubwa zaidi ya yale tuyadhaniayo!
Magufuli ameanza vizuri katika kubana matumizi ya serikali nampongeza kwa hilo. Ila tahadhari ichukuliwe mapema kwa kuepuka kumpa sifa zilizopitiliza kwa kila hatua anayochukua. Badala yake Magufuri ashauriwe kufuata sheria sio mabavu tu kila wakati. Mfano suala la vitanda, hiyo tenda MSD waliitangaza lini na wakati gani ilihali vitnda vililetwa weekeend baada ya tamko la Rais Ijumaa? Ni vizuri kununua vitanda vya wagonjwa lakini pia tuepuke kukurupuka bila kufuata sheria ya manunuzi ya umma tushiishie kupata vitu sub-standard. Na pia suala la kufuta sherehe za uhuru na pesa zake kutumika katika ujenzi wa barabara ni la kupongezwa. Isipokuwa suala la kuanza ujenzi huo bila kufuata sheria ya manunuzi kwa kutangaza tenda nalo sio la kulishabikia. Tutakuja kulia huko mbeleni na asiwepo wa kutunyamizisha.
WITO:Wakati tunampongeza Rais Magufuri tusijitie upofu wa kutoona kasoro zinazojitokeza, hatumsaidii bali tunamharibia.Tumshauri vema Rais ili kuepuka matatizo ya kuokoa pesa upande mmoja na kuziteketeza upande mwingine kwa kutofuata sheria ya manunuzi ya umma ambayo inasisitiza utangazaji wa tenda na kushindanisha wazabuni ili kumpata aliye bora .
Mkuu maliza kabisa: MIAFRIKA HATUNA AKILI
Kwani ni Kikwete tu ndiye aliyewahi kuwa rais kabla ya Magufuli?
Watu mnaongea kana kwamba ufisadi na uzembe umeanza na Kikwete.
SMDH.
Ni kweli Mkuu Nyani Ngabu watanzania wengi ni kama bendera tu, hufuata upepo unakoelekea. Kama mtakumbuka vizuri, kuna propaganda zilianza kutembea humu kuhusu waziri wa fedha. Wengi wa wapiga debe walikuwa wakimpamba Kitilya na Bade kama wangefaa kuteuliwa ubunge na hatimaye mmojawapo kuteuliwa uwaziri wa fedha. Waliwapamba watu hao kana kwamba ni malaika wameshuka leo toka mbinguni. Sasa tunashuhudia madudu yao live bila chenga! sijui hao wapiga debe wanakuja na nini tena? wengine wameanza tena mara ooh Kimei wa CRDB anafaa uwaziri wa fedha. Hii ni kwa kuwa upande wa pili wa Kimei haujajulikana bado kutokana na mfumo wa kulindana uliopo serikalini. Lakini upande wa pili wa hao mnaowapigia debe ukifunuliwa sijui mtaficha wapi sura zenu.Hao waliokunywa hadi wakalewa pombe ya Magufuli unadhani watakuelewa basi...?