Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Hakika Mungu ni mkuu. Mwl nyerere alipata kusimulia hadithi nzuri sana ambayo inawajibu wanafiki wote wanaompigia kelele Dr Magufuli. Sikiliza audio ya Mwl Nyerere hapa chini

Namwona Lowassa anasikiliza kwa makini hapo pembeni
 
Dr Magufuli hajavunja demokrasia. Ila nyie wapinzani ndiyo mnalengo la kuvuruga amani yetu. Mnahubiri chuki, mnashabikia ufusadi. Nchi hii ni yetu sote, tuache kufitiana. Hivi akina Mbowe wageenda wanahimiza wanachi wafanye kazi, wanawashukuru wananchi kwa kuwapigia kura nani angewazuia kufanya mikutano??? Lakini wao wanaenda kuwaambia wananchi wasilipe kodi, wananchi wasifanye kazi waandamane kuipindua serikali iliyoko madarakani, wanahimiza vijana wanywe viroba badala ya kazi, n.k.
Yaani Wapinzani ni hatari kuliko hata magaidi! Kabisa kwani wangekuwa wanahamasisha maendeleo ya wananchi kweli Rais angekataa? Kabisa Mh. Magufuli Usigeuke nyuma hii clip isambazwe kwenye vyombo vya habari vyooote!
 
"Rais Magufuli anafanya vizuri katika baadhi ya maeneo. Lakini mimi ningeanza tofauti. Ningeanza na walimu badala ya madawati. Bila kudeal na maslahi ya waalimu nchi hii hakuna litakalofanikiwa katika elimu. Rais Magufuli ameshika eneo moja la madawati kama sehemu ya kuboresha elimu. Lakini Madawati sio elimu, ni kitu kidogo sana ktk elimu. Elimu haiboreshwi kwa madawati, boresha maslahi ya waalimu kwanza, boresha mitaala, kisha ndio uboreshe miundombinu ya shule (maabara, maktaba, madarasa etc). Madawati hayawezi kuwa kipaumbele cha kwanza ktk elimu" Edward N. Lowassa (Waziri Mkuu 2005/08).!
 
Kama unadhani madawati siyo muhimu nenda kawaambie mkeo na watoto wako waanze kusoma wamekaa chini kwenye mavumbi kuanzia Leo
 
MWENYE ENZI MUNGU ATUONGOZE MILELE YOTE AMEN
 
Hujui historia ya nchi hii ndio maana unapayuka,amekuta vyama vipi Vingi na kuvifuta!Hujui nchi ameitoa kwa mkoloni?
Wewe unaeijua historia lakini hujui kuwa 1962 Nyerere kupitia TANU alipambana na Abbas Mtemvu kupitia ANC, Nyerere kakabidhiwa Nchi hii 1961 kaikuta na Vyama Vingi na akaja kurekebisha Katiba 1965 kwa kuvifuta. Hata 1958 wakati wa Ukoloni waliingia kwny uchaguzi wa Baraza la kutunga sheria kukiwa na Vyama vingi
Upenzi wako kwa Nyerere umepitiliza mpaka unataka ku compromise ukweli.
 
Wewe unaeijua historia lakini hujui kuwa 1962 Nyerere kupitia TANU alipambana na Abbas Mtemvu kupitia ANC, Nyerere kakabidhiwa Nchi hii 1961 kaikuta na Vyama Vingi na akaja kurekebisha Katiba 1965 kwa kuvifuta. Hata 1958 wakati wa Ukoloni waliingia kwny uchaguzi wa Baraza la kutunga sheria kukiwa na Vyama vingi
Upenzi wako kwa Nyerere umepitiliza mpaka unataka ku compromise ukweli.
Unaikutaje nchi na vyama vingi wakati nchi ilikuwa ikiongozwa na mkoloni?Chama cha wakoloni ambacho kilikuwa kinaongoza nchi kilikuwa kinaitwaje?
 
Wasalaam ndugu wana jf!
Leo na mimi napenda niseme kidogo kuhusu Rais na namna anavyoendesha nchi yetu, kwanza nampongeza sana Rais kwa kutojali watu wanasema nini kuhusu kuweka mfumo wa adabu katika utumishi wa umma, binafsi napenda niseme kuwa watanzania wengi tulikuwa tumezoea porojo, uzembe na utoro katika kutimiza wajibu wetu.
Pia napenda kumpongeza Rais kwa kuwatumbua wote ambao wanapwaya katika nafasi zao, hapa napenda niseme Rais asiogope kuwatumbua kabisaaa hata kama ni baada ya nusu saa baada ya kuwaapisha maana najua sisi watu hata kama uko wapi(polisi, jeshini,usalama wa taifa) bado unaweza kuwa na mapungufu ya kiuongozi. Pia namshari Rais, tafadhali sana sana unapotaka kusema jambo kwenye hadhara jaribu kushauriana na wasaidizi wako maana ninavyojua sio kila kitu mtu anatakiwa kukisema hadharani, la mwisho napenda nimkumbushe kuwa mabadiliko yoyote huja na resistances kutoka kwa watu hivyo usichoke kuwaelimisha wasidizi wako, kuna mambo ya ndani na nje.
Ahsanteni.
 
Maiti we
Huu ushauri wako unafikiri utamsaidia nini kapewa ushauri mwingi hadi ikulu imekuwa HALIMA SHAURI
 
Tangu CCM ishinde uchaguzi hapo 2015, nimetembelea mikoa karibia 18, kila ninakopita, ni Dr Magufuli, CCM, na Tanzania yetu mpya! Watanzania wanamshukuru sana Mungu kwa ujio wa Dr Magufuli.

Tujipongeze wote tuliopiga kura ya ndiyo kwa Dr Magufuli
 
Huko ulikopita waliongezewa mishahara,walipewa ajira,walipanda madaraja,sukari haijapanda bei,nk
Kama ni hivyo sawa ila kama sio hawajui kuwa wanatawaliwa na dikteta uchwara pia hawajitambui.
 
Back
Top Bottom