Ndugu wanajamvi,
Ukimtafuta shujaaa baada ya nyerere utataja majina mengi lakini huyu hapa ndiye Shujaa wa mabadiliko Tanzania. Waswahili wanasema nyota njema huonekana asubuhi. Na Mimi nimeshamwona huyu MWANAMAGEUZI wa kweli katika nchi yetu.. Ni nani huyu? Ni swali nyepesi kama kichwa kiko tupu ila ni swali gumu kama unafiria kwa undani na kuweka fikra zako kwa umbali zaidi jibu lake fupi naye ni RAIS MAGUFULI, kwanini yeye?
1: Kujenga uwajibikaji na uwazi (Responsibility and transparency) kwenye taasisi za umma; Rais magufuli amejenga nidhamu kubwa mno kuwahi kutokea hapa Tanzania, watumishi wa umma wanafanya kazi kwa uzalendo na uadilifu mkubwa mno. Wananchi wanashukuru kwa dhati kazi aliyoifanya rais magufuli pamoja na jopo lake.
2: Kuusambaratisha mtandao wa mafisadi; hili ni jambo ambalo limepigiwa kelele sanaaa lakini kwa Bahati nzuri tumempata muasisi wa mahakama ya mafisadi. Ni katika awamu hii ndipo tumewaona vigogo wenye hela na wenye ushawishi mkubwa ndani na nje ya serikali wanalala kwa kunyimwa dhamana kitu ambacho watawala wengine huogopa kwa kuangalia usalama wake. Lakini huyu nguli anakwambia yupo kufa lakini hawa mafisadi nao waonje hukumu ya dhuluma yao.
3: Kujenga demokrasia ya kweli; watu wengi hasa wapinzani wanapotosha dhana ya demokrasia kwa kutumia propaganda nyingi. Lakini ukweli ni kwamba MAGUFULI ni mwanademokrasia wa kweli kwa sababu anatawala kwa kufuata misingi ya katiba ya nchi yetu. Demokrasia ya kweli haipo duniani tokea mungu alivoiumba hii dunia? Rejea maandiko matakatifu na soma kila Quran vizuri uonevu ulikuwepo tokea zamani.
Ata shetani alipotaka demokrasia ya kweli kwenye utawala wa mungu alionyeshwa mlango wa kutokea. Demokrasia wanayotaka wapinzani mi kushindana na mtawala kitu ambacho hakiwezekani ata kidogo. Wananchi wapo huru kabisaa kama wanasema demokrasia haipo wasiwashawishi wananchi kwa maana maana wananchi ndio wanapima uongozi uliopo na sio kuhamasisha kwa kutumia propaganda ambazo hazina kichwa wala miguu.
Hata wao wenyewe hawana demokrasia ya kweli kwenye vyama vyao kwa sababu kungekuwepo demokrasia ya kweli ZITO KABWE asingefukuzwa chadema na CHACHA WANGWE asingekufa akidai demokrasia kwenye chama lakini wao wamekuwa kipofu na wamezibwa macho hawawezi kuyaona bali wao kwa ajili ya kupinga utawala uliopo.
4: kujenga uongozi imara kwenye taasisi za umma; ni mara ya kwanza Tanzania kwa vijana kupewa taasisi nyeti za serikali hii ni ishara tosha kuwa MAGUFULI ni mwanademokrasia aliyekomaa. Vijana kama POLEPOLE, MAKONDA, JANUARY, UMMY,JAFFO,MWIGHURU na wengineo.
Kwa kuwa vijana inaaminika wana maono ya mbali katika kuleta maendeleo na kuwajibika bila kujali nyakati wala sehemu asante sana kwa hili RAIS MAGUFULI. Pia ni kwa Mara ya kwanza Tanzania watumishi wa umma kuongozwa na wasomi wenye taaluma zinazokidhi na kuakisi hali halisi ya Tanzania tuitakayo.
My take: Naomba tuwapuuze wote wenye mrengo wa kupambana na utawala wa RAIS MAGUFULI kuwa wanadai demokrasia kwa kuwa hili ni genge la mafisadi ambao wana mtandao mpana ndani na nje ya nchi. Tuwapuuze na kuwakataa tulivofanya hivi 2015. Tuwaogope kama ukoma hii genge Ikulu wamelisaka tokea 1995 kwa nguvu za pesa na Giza lakini mungu naye anawajibu na anatupenda watanzania.
Mfano: MAO DON kipindi anaingia kwenye utawala wake China alikuta nchi hiyo ina uchumi kama Tanzania lakini alikaa chini na kufikiria kwa umakini Mkubwa mno na akaamua kuwa jambo la kwanza ni watu kufanya kazi na katika hili Mao alikuwa mkali sanaaa akapiga marufuku hadi shughuli za kidini zilizokwamisha watu kufanya kazi.
Mao akaenda mbali mno na kusema kuwa mtandao wa kijamii full stop wapinzani wake walizunguka huku na huko kuhamasisha maandamano za kumpinga Mao kuwa ni dikteta lakini kwa Bahati nzuri walishindwa. Lakini Leo mafanikio ya China ni chini ya kivuli ya MAO wananchi wanaabudu hadi sanamu zake katika majiji tofauti China hadi mtoto atakayezaliwa China kesho basi ni sharti Amjue Mao kwa kuwa ndiye baba na mama wa China.
Tukumbuke kipindi Mao anahamasisha watu wakafanye kazi kulikuwa hakuna ajira na vijana wengi wakafuzwa sehemu za mijini Mao aliamini kuwa asingeweza kuajiri vijana wote ndio maana alifanya vile na ilimsaidia kuongeza uwezo maalum wa kushindana katika kuonyesha ujuzi maalum na ndio imeipelekea China kuwa kama sasa hivi.
Lakini kwa Bahati nzuri na sisi watanzania tunampata RAIS mwenye maono kama ya MAO halafu inatokea genge la mafisadi na mabwenyenye wanataka kutuhujumu hatuwezi tukakubali kamwe tuwapuuze na kuwapinga hadharani.
Kusema ukweli wanaoupinga utawala huu ni wale ambao watoto wao walikua wakiugua mafua wanaenda kutibiwa China ni walewale waliozoea kuishi kwa madili kama mgombea wao na walipanga kuendelea kuishi kwa madili lakini mtandao wao umesambaratishwa ni wale ambao watoto wao walikuwa hawakai chini wakati wa kusoma kwa kweli hawa watu tuwapuuze kabisaa.
Safari ya kuelekea kwenye uchumi wa kati bado inaendelea;
Ni wako kijana muadilifu, mwanaharakati na mzalendo wa kweli katika taifa letu.
SIMON MATO.
0762189733