Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Utumbuaji wa MTUKUFU MAGUFULI wamkumba mpaka Diwani. Diwani wa kata ya Mwangud katika wilaya ya Meatu ANTHONY PHILIPO amehojiwa na TAKUKURU kwa tuhuma ya wizi wa mamilioni ya kijiji cha makao wilayani humo. Hii imekwnda sambamba na kuhojiwa kwa wengine kama Ofisa mtendaji.
Hii inatujengea picha ya kwamba hakuna atakayesalimika kama ataendeleza au kuanzisha tabia tya ubadhilifu ndani yake.
[HASHTAG]#SerikaliYaCcmInasafishaNchi[/HASHTAG]
 
Kwanza kabisa niwasalimu wanajamvi sasa naomba nianze mada yangu watanzania tulitaka tupate kiongozi mkali atakaye weza kuisimamia serkali ipasavyo nashangaa sana Leo tunapo geuka kauli zetu wenyewe tulisema mkwere anachekacheka tumempata kiongozi kalamba ndimu bado hatutaki tunataka nini mkwere alituacha tufanye siasa kadili tulivyoweza sasa hakuna siasa mpaka 2020 hatutaki sasa ili mambo yaende sawa tukamuombe radhi mkwere laana itaondoka maombi yetu ambayo mh aliomba tumuobee yatafanya kazi tofauti na sasa kila tukiomba linazuka jipya tusipo Fanya haraka kumuangukia mkwere tujiandae kuwa na chama kimoja sasa wastaafu wakubwa staiki zao naanza kuona Giza sefu hakutoa mkono mkuru amechimba biti Kali huu ni ushauli tuuu
 
Mwl Julius Kambarage Nyerere hayati Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema aliwahi kutuasa vijana kuwa waasi wa mifumo ya uongozi katika jamii yetu isiyo wajibika, inayotunyonya na kutukandamiza hivyo kuturudisha nyuma na kuendelea kutuacha katika lindi la umaskini.

Leo tumempata Rais aliyeamua kuwa muasi wa mifumo na vitendo vya kifisadi, uwizi, upigaji dili na inayotunyonya na kuiumiza nchi yetu kwa manufaa ya watanzania maskini ambao ni wanyonge.

Hatuna budi kusimama, kumuunga mkono na kumlinda dhidi ya maadui na mawakala wa mabepari kutoka ndani au nje ya nchi wasiofurahishwa na haya anayofanya kwa ustawi wa Tanzania yetu.

Tukifanya hivyo tutamtia moyo zaidi zaidi lakini tutakuwa tumewatumia salamu kuwa wanyonge tumeungana kuwakabili wenye nguvu na hakika tutashinda!

Wanaompinga Rais Magufuli tujue hata sisi wanyonge hawatupendi. Hivyo lazima tuwakabili pia kwa kumuunga mkono Rais wetu.

Kwa pamoja tumhakikishie Mhe Rais Magufuli kuwa Daima pamoja naye, kanyaga twende [HASHTAG]#HapaKaziTu[/HASHTAG]
 
Ndugu wanajamvi,

Ukimtafuta shujaaa baada ya nyerere utataja majina mengi lakini huyu hapa ndiye Shujaa wa mabadiliko Tanzania. Waswahili wanasema nyota njema huonekana asubuhi. Na Mimi nimeshamwona huyu MWANAMAGEUZI wa kweli katika nchi yetu.. Ni nani huyu? Ni swali nyepesi kama kichwa kiko tupu ila ni swali gumu kama unafiria kwa undani na kuweka fikra zako kwa umbali zaidi jibu lake fupi naye ni RAIS MAGUFULI, kwanini yeye?
1: Kujenga uwajibikaji na uwazi (Responsibility and transparency) kwenye taasisi za umma; Rais magufuli amejenga nidhamu kubwa mno kuwahi kutokea hapa Tanzania, watumishi wa umma wanafanya kazi kwa uzalendo na uadilifu mkubwa mno. Wananchi wanashukuru kwa dhati kazi aliyoifanya rais magufuli pamoja na jopo lake.

2: Kuusambaratisha mtandao wa mafisadi; hili ni jambo ambalo limepigiwa kelele sanaaa lakini kwa Bahati nzuri tumempata muasisi wa mahakama ya mafisadi. Ni katika awamu hii ndipo tumewaona vigogo wenye hela na wenye ushawishi mkubwa ndani na nje ya serikali wanalala kwa kunyimwa dhamana kitu ambacho watawala wengine huogopa kwa kuangalia usalama wake. Lakini huyu nguli anakwambia yupo kufa lakini hawa mafisadi nao waonje hukumu ya dhuluma yao.

3: Kujenga demokrasia ya kweli; watu wengi hasa wapinzani wanapotosha dhana ya demokrasia kwa kutumia propaganda nyingi. Lakini ukweli ni kwamba MAGUFULI ni mwanademokrasia wa kweli kwa sababu anatawala kwa kufuata misingi ya katiba ya nchi yetu. Demokrasia ya kweli haipo duniani tokea mungu alivoiumba hii dunia? Rejea maandiko matakatifu na soma kila Quran vizuri uonevu ulikuwepo tokea zamani.

Ata shetani alipotaka demokrasia ya kweli kwenye utawala wa mungu alionyeshwa mlango wa kutokea. Demokrasia wanayotaka wapinzani mi kushindana na mtawala kitu ambacho hakiwezekani ata kidogo. Wananchi wapo huru kabisaa kama wanasema demokrasia haipo wasiwashawishi wananchi kwa maana maana wananchi ndio wanapima uongozi uliopo na sio kuhamasisha kwa kutumia propaganda ambazo hazina kichwa wala miguu.

Hata wao wenyewe hawana demokrasia ya kweli kwenye vyama vyao kwa sababu kungekuwepo demokrasia ya kweli ZITO KABWE asingefukuzwa chadema na CHACHA WANGWE asingekufa akidai demokrasia kwenye chama lakini wao wamekuwa kipofu na wamezibwa macho hawawezi kuyaona bali wao kwa ajili ya kupinga utawala uliopo.

4: kujenga uongozi imara kwenye taasisi za umma; ni mara ya kwanza Tanzania kwa vijana kupewa taasisi nyeti za serikali hii ni ishara tosha kuwa MAGUFULI ni mwanademokrasia aliyekomaa. Vijana kama POLEPOLE, MAKONDA, JANUARY, UMMY,JAFFO,MWIGHURU na wengineo.

Kwa kuwa vijana inaaminika wana maono ya mbali katika kuleta maendeleo na kuwajibika bila kujali nyakati wala sehemu asante sana kwa hili RAIS MAGUFULI. Pia ni kwa Mara ya kwanza Tanzania watumishi wa umma kuongozwa na wasomi wenye taaluma zinazokidhi na kuakisi hali halisi ya Tanzania tuitakayo.

My take: Naomba tuwapuuze wote wenye mrengo wa kupambana na utawala wa RAIS MAGUFULI kuwa wanadai demokrasia kwa kuwa hili ni genge la mafisadi ambao wana mtandao mpana ndani na nje ya nchi. Tuwapuuze na kuwakataa tulivofanya hivi 2015. Tuwaogope kama ukoma hii genge Ikulu wamelisaka tokea 1995 kwa nguvu za pesa na Giza lakini mungu naye anawajibu na anatupenda watanzania.

Mfano: MAO DON kipindi anaingia kwenye utawala wake China alikuta nchi hiyo ina uchumi kama Tanzania lakini alikaa chini na kufikiria kwa umakini Mkubwa mno na akaamua kuwa jambo la kwanza ni watu kufanya kazi na katika hili Mao alikuwa mkali sanaaa akapiga marufuku hadi shughuli za kidini zilizokwamisha watu kufanya kazi.


Mao akaenda mbali mno na kusema kuwa mtandao wa kijamii full stop wapinzani wake walizunguka huku na huko kuhamasisha maandamano za kumpinga Mao kuwa ni dikteta lakini kwa Bahati nzuri walishindwa. Lakini Leo mafanikio ya China ni chini ya kivuli ya MAO wananchi wanaabudu hadi sanamu zake katika majiji tofauti China hadi mtoto atakayezaliwa China kesho basi ni sharti Amjue Mao kwa kuwa ndiye baba na mama wa China.

Tukumbuke kipindi Mao anahamasisha watu wakafanye kazi kulikuwa hakuna ajira na vijana wengi wakafuzwa sehemu za mijini Mao aliamini kuwa asingeweza kuajiri vijana wote ndio maana alifanya vile na ilimsaidia kuongeza uwezo maalum wa kushindana katika kuonyesha ujuzi maalum na ndio imeipelekea China kuwa kama sasa hivi.

Lakini kwa Bahati nzuri na sisi watanzania tunampata RAIS mwenye maono kama ya MAO halafu inatokea genge la mafisadi na mabwenyenye wanataka kutuhujumu hatuwezi tukakubali kamwe tuwapuuze na kuwapinga hadharani.

Kusema ukweli wanaoupinga utawala huu ni wale ambao watoto wao walikua wakiugua mafua wanaenda kutibiwa China ni walewale waliozoea kuishi kwa madili kama mgombea wao na walipanga kuendelea kuishi kwa madili lakini mtandao wao umesambaratishwa ni wale ambao watoto wao walikuwa hawakai chini wakati wa kusoma kwa kweli hawa watu tuwapuuze kabisaa.

Safari ya kuelekea kwenye uchumi wa kati bado inaendelea;

Ni wako kijana muadilifu, mwanaharakati na mzalendo wa kweli katika taifa letu.

SIMON MATO.
0762189733
 
Nikivyo soma hapo # 3 Haraka haraka nikajuwa unatafuta kula......nikajuwa hujasukumwa na weledi wala utaishi kuandika ulicho andika bali tumbo...
 
Kama unataka kumsifia Mao kasome tena Cultural revolution na after ya hiyo kitu alafu urudi ku argue your point
 
Wanajamvi huyu hayumo kwenye category ya uchochezi kweli?!!
Mbona kama anatuchochea tuvurumishe maneno yatakayoonekana kumkwaza "gendaeka" ambalo ndio kosa kisheria.

Kwa nini asishughulikiwe hata na moderator incharge.
 
Wanajamvi huyu hayumo kwenye category ya uchochezi kweli?!!
Mbona kama anatuchochea tuvurumishe maneno yatakayoonekana kumkwaza "gendaeka" ambalo ndio kosa kisheria.

Kwa nini asishughulikiwe hata na moderator incharge.
Mbona hamna hoja ya msingi zaidi ya kukashifu, kukebehi na kudhihaki zaidi mnafanya hivi ili kuwafurahisha wanaowatuma
 
Nasema ni kheri serekali ifungue ajira sasa Maana huku ni zaidi ya kujikomba
 
Naanza kupata mashaka kuwa kuna watu anawatuma yeye mwenyewe kisha anawateua kuwa DED au DAS.
Maana hayo mnayoandika hata huko kwenye chama chake hawaamini hivyo kwani hata ukiitisha kura ya siri ya kutokuwa na imani na mwenyekigoda itapata zaidi ya 75%
 
Ur one of the lowest IQ i have ever heard...!!

Wewe umesikia ukimsifia Mh. Rais utapata cheo, au nafasi ktk taasisi ya umma..!! Ur a crook..!! hupati kitu..!! Andika hata ufie kwenye keyboard... hupati kitu
 
Wewe jamaa una akili nyingi sana....
Al Haj Ally Hassan Mwinyi 1985-1995 HASTAIILI KUJENGEWA SANAMU LA HESHIMA

Ben Mkapa 1995-2005
HASTAIILI KUJENGEWA SANAMU LA HESHIMA

Jakaya Kikwete 2005-2015
HASTAIILI KUJENGEWA SANAMU LA HESHIMA

John Pombe November 2015- September 2016
ANASTAIILI KUJENGEWA SANAMU LA HESHIMA

Wewe ni jini azi...watu wametumikia hii nchi kwa mlongo mzima wewe unaona aliyetumikia mwaka kasoro ndo anayefaa

Hata hivo endelea.....
Kuna unachotafuta.... Sote tunajua AJIRA NI NGUMU ILA UTEUZI NI RAHISI.
 
Back
Top Bottom