Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Msema kweli mpenzi wa Mungu, nimefuatilia kwa makini walalamikaji wengi wanaolalamikia serikali ya awamu ya tano ni wana CCM,hii ni kutokana na wao kuwa wanufaika wakubwa wa mfumo wa kupiga dili uliozoeleka ndani ya serikali zilizopita.

Ebu jiulize maswali machache

1-Nani walikuwa wanufaika na akaunti hewa na watumishi hewa?

2-Nani walikuwa wanafaika na miradi hewa ilikuwa ikizinduliwa na mbio za mwenge?

3-Nani walikuwa wanufaika na manunuzi yote yaliokuwa yanafanywa na serikali?

4-Nani waasisi wa wizi na ujangili ndani ya mbuga za wanyama?

Wanaoisoma namba ni CCM maana ndio waliokuwa wameshikilia mpini na mirija yote ya ufujaji wa mali za umma uliasisiwa na wao

Yale yote walikuwa wanatetea kama safari za nje na n.k ndio Magufuli kaziba
Hongera Magufuli.
 
Usiseme CCM Sema viongozi BAADHI WA CCM ndo wanaisoma namba. Ukisema CCM ina maana hata wanachama wanahusika Kwa hio itakuwa wananchi wote.. Rekebisha
 
Wale vibwengo ambao hata shule hawana wanaopiga vuvuzela hapa jamvini wakitegemea ajira za kuzawadiwa na hawakuzipata ndiyo wanaisoma namba
 
Usiseme CCM Sema viongozi BAADHI WA CCM ndo wanaisoma namba. Ukisema CCM ina maana hata wanachama wanahusika Kwa hio itakuwa wananchi wote.. Rekebisha
Na WENYE Chama ambao ni wananchi hawakuwahi kufaidika na hayo uliyoyataja Kwa msingi WA hoja yako hawawezi kuisoma namba.. Usichanganye mambo
 
zaidi ccm mana ukivaa shati la kijani unakula kwa ubua kwa sasa madogo arusha had wanapigania ofis
 
Usiseme CCM Sema viongozi BAADHI WA CCM ndo wanaisoma namba. Ukisema CCM ina maana hata wanachama wanahusika Kwa hio itakuwa wananchi wote.. Rekebisha
Labda umesahau kuwa wana ccm ndio waliokuwa wanatetea kwa nguvu zote kisa walipewa t-shirt na kofia na pesa ya chumvi. kwani hao viongozi walikuwa wanaongoza nini?
 
Na WENYE Chama ambao ni wananchi hawakuwahi kufaidika na hayo uliyoyataja Kwa msingi WA hoja yako hawawezi kuisoma namba.. Usichanganye mambo

Nani alikudanganya ccm ni chama cha wananchi? zaidi ya watu milioni 30 hawana chama, pia ccm ni chama cha wana ccm siyo wananchi kama unavyodhani maana nchi hii ina vyama vingi
 
Sasa kama CCM wanaisoma namba nyie mnalialia nini mara UKUTA mara mnaenda kuangalia mechi ya simba na yanga si mtulie

Mwenyekiti CCM JF
 
Kidumu chama cha mapinduzi wana JF!
Juzi kati hapa nilisafiri vijijini mikoa ya kanda ya ziwa, baadaya ya hapo nikapita zangu kuelekea Arusha nikashuka zangu Dodoma na kurudi nyumbani Dar kwenye jiji la Mh. Paul Makonda.

Nikiwa kanda ya ziwa nilijionea na kusikia yafuatayo:

  1. Wananchi hasa wavuvi wanalalamika sana juu ya katazo la kutumia zana haramu za uvuvi. Ila wakati huo huo wanashukuru kwa kusema sheria lazima itekelezwe. Wanaendelea kutoa maoni zaidi kwa kusema iwapo katazo litazingatiwa na sheria kufuatwa basi uvuvi utakuwa na tija kwa miaka inayokuja. Asilimia kubwa wanaipongeza serikali ya CCM na Mh. Dkt Magufuli kwani kuna baadhi ya wavuvi walitumia hadi net kuvua mpaka vitoto vya samaki.
Nikiwa njiani Arusha na Dodoma
  1. Wananchi wengi wanashukuru serikali ya CCM chini ya uongozi wa Dkt Magufuli kwa kuleta heshima mitaani.
Tuzidi kumuombea rais wetu Dkt Magufuli ili asikatishwe tamaa na waongo, waleta uzushi na wanafiki wanataka kumkatisha tamaa.
 
[HASHTAG]#lizaboni[/HASHTAG],[HASHTAG]#ndege[/HASHTAG] JOHN na [HASHTAG]#Njanga[/HASHTAG] tz,"hakika mnanena msiyoyasadaki na mnashangilia yanayowachoma"...lakini siwezi wahukumu maana "ngazi itaendelea kuwa ngazi,haitabadilika katka matumizi yake kama ngozi"
 
[HASHTAG]#VIVIANET[/HASHTAG],kumpigia mbuzi gitaa ukitaraji atacheza ni kazi bure..utatumia nguvu kubwa kumsaidia mtu asiyejielewa.."hakuna kitu kibaya hapa duniani kama mjinga/kihiyo kukataa kuelimika"..
 
Binafsi nimefurahishwa na kasi ya Dkt. Magufuli. Naamini wapo pia wengi wanaoungana nami katika furaha hii. Magufuli ameanza kwa kasi ambayo kama ataimaintain, Tanzania haimalizi miaka mitano itakuwa tayari ni nchi yenye kipato cha kati.

Hata hivyo wapo baadhi yetu ambao wanakejeli kasi hiyo. Hao kwangu ni watu waliozoea ubwete na bora liende!. Wanamwona Magufuli kuwa ni mtu atakayekuwa kauzibe kwao!

Wapigaji wote, wavivu wote na wazee Wa madili wote watamchukia Magufuli ila mi niseme na niwaombe tu kwamba tumpe support huyu jamaa kiukweli atatufikisha mahali Fulani!

Tuwafichue wote wanapanga kumhujumu (najua wanajulikana), tuwakatae kwani hawana nia njema na taifa letu.
Big up uncle magu piga kazi.
 
Ninaamini wazungu hawana ufahamu wa kumwelewa JPM,na watapata shida kumwelewa..
Natalaji wengi kuja kufanya thesis zao hapa Tanzania..

Tuna historia za viongozi wengi waliotukuka kwa misimamo yao thabiti kwa maslahi ya nchi zao kama toka kwa simba wa afrika kina Hayati Dr Kwame Nkhurumah,Hayati Patrice Lumumba,Hayati Thomas Sankala,Robert Mugabe,Fidel Castro,Kanal Gaddafi,Hayati Julius K.Nyerere,Hayati Mahatma Gandi,Hayati Samora Matchel,Hayati Che Guevara,Hayati Bob Marley na wengine wengi..

Ukoloni mamboleo utafikia kikomo hivi karibuni tukifanikiwa kuziba mianya yote ya makusudi ya kutufanya maskini licha ya utitiri wa utajiri tulionao..

JPM aendelee kutohudhuria mikutano,vikao,mikusanyiko yenye mbwembwe za siasa za maendeleo lakini kiuhalisia ni fulsa ya kutawaliwa kisiasa,kijamii na kiuchumi..Tegemea vikwazo vingi toka kwa inayoitwa jumuiya ya kimataifa {Sababu ya msingi sio kinachoitwa demokrasia wala haki za binadamu ambao wao wanazivunja kwa kuvamia na kusababisha vita mfano:Libya,Iraq,Syria...Sababu ni kuwaminya ktk upigaji,uchumaji zabibu za bure kwenye shamba la bibi...unawabana walipe kodi!!! }

JPM aendelee kugomea mikataba ya ulaghai na unyang'anyi kama ya kina sultani Mangungo wa Msovero mfano,EPA,Bilateral agreements,...yenye sura ya unyonyaji,ukandamizaji,uporaji rasilimali..

Nafahamu JPM hatoishi milele ,nafahamu JPM hatotawala Tanzania milele,Nafahamu Yamkini waovu/walaghai/wanyonyaji hawawezi furahia utendaji wa kizalendo na uliotukuka kwa maslahi ya nchi toka kwa JPM..

Ni furaha ya wanyonyaji kuona wananchi wakiishi kwa umaskini mkubwa huku mali zao zikiwanufaisha wanahisa wa makampuni ya kikoloni mamboleo Mashariki ya mbali,Magharibi ya mbali,Kaskazini ya mbali...

Si kitu cha aajabu leo kusikia wamiriki wa makampuni yanayochimba madini,mafuta na gesi katika nchi za Tanzania,Congo DRC,Uganda,Sudani Kusini,Zambia,Malawi ni wananchi wa Australia,Canada,USA,UK,EU,China,Russia....inasikitisha,si ni ukoloni huu?!!

Zarisha Simba wengi wadogo,wakubwa...kila sekta,kila idara..watafanya hira kukukwamisha lakini Mungu atakushindia,ataishindia Tanzania,ataishindia Afrika..tumechoka kuwa maskini tunaotegemea bidhaa za wengine..tumechoka kuwa shamba lisilokuwa na mwenyewe kupitia mikataba ya ulaghai,unyang;anyi,kikoloni...

JPM NI SIMBA WA AFRIKA...UKOMBOZI WA AFRIKA UNAENDELEA..
RASILIMALI ZA AFRIKA KWA MAENDELEO YA AFRIKA..
 
tutampima kwa matokeo kama vifaa vya kutosha mahospitalini, madawa ya kutosha, wafanyakazi wa kutosha hasa elimu na afya, vitendea kazi vya kutosha mashuleni, wanafunzi wenye sifa elimu ya juu wote wanapata mikopo, barabara nzuri, maji salama, umeme wa uhakika, uchumi wa mtu mmoja mmoja umekua n.k hatutampima kwa ziara maofisini

Fanyeni kazi na kulipa kodi Mkiongozwa na uzalendo, hapo Mtapima, sio kushinda vijiweni na maandamano mtegemee kumpima hamtatenda haki kabisa.
 
Nawaza au kutafakari tu!
1. Aliahidi Elimu Bure, Imewezekana - ametekeleza!
2. Akasema atadumisha nidhamu ya wataumishi, ametekeleza!
3. Akasema atapunguza matumizi ya serikali, kweli tumeona!
4. Akasema atapambana na wanaokiuka kanuni za matumizi ya fedha za umma, kweli tunaona!
5. Hili la ndege ni by the way tu! zimenunuliwa, hata kama zina pangaboi lakini zimenunuliwa!

wazee wa lumumba ongezeni mengine! na wale wa ufipa leteni changamoto, ila msitukane.
 
Nawaza au kutafakari tu!
1. Aliahidi Elimu Bure, Imewezekana - ametekeleza!
2. Akasema atadumisha nidhamu ya wataumishi, ametekeleza!
3. Akasema atapunguza matumizi ya serikali, kweli tumeona!
4. Akasema atapambana na wanaokiuka kanuni za matumizi ya fedha za umma, kweli tunaona!
5. Hili la ndege ni by the way tu! zimenunuliwa, hata kama zina pangaboi lakini zimenunuliwa!

wazee wa lumumba ongezeni mengine! na wale wa ufipa leteni changamoto, ila msitukane.

Hata Lugumi ameweza,na kumpangia bajeti IPTL ili abadilishe Mitambo yake pia ameweza,Kuvunja Katioba Ya Jamuhuri wa Muungano ya Tanzania ameweza.Kuwanyima wapinzani haki ya kwenda kutibiwa nje na kuwapa wa CCM haki ya kutibiwa nje ameweza.Kutugawa kwa itikadi ameweza pia
 
Back
Top Bottom