Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Nawaza au kutafakari tu!
1. Aliahidi Elimu Bure, Imewezekana - ametekeleza!
2. Akasema atadumisha nidhamu ya wataumishi, ametekeleza!
3. Akasema atapunguza matumizi ya serikali, kweli tumeona!
4. Akasema atapambana na wanaokiuka kanuni za matumizi ya fedha za umma, kweli tunaona!
5. Hili la ndege ni by the way tu! zimenunuliwa, hata kama zina pangaboi lakini zimenunuliwa!

wazee wa lumumba ongezeni mengine! na wale wa ufipa leteni changamoto, ila msitukane.

Lumumba washakuwa mzigo hao, hakuna mshahara hapo ni mihayo kwenda mbele, na hata ukipita pale lumumba kile kijiwe cha kahawa naona kimefutika, jamaa zako wanapostia nyumbani kwao ccm lumumba hali ni mbaya sana, kilichobaki ni kujikomba tu waone kama watakumbukwa au kuhukwaa uDC au uDED
 
Hata Lugumi ameweza,na kumpangia bajeti IPTL ili abadilishe Mitambo yake pia ameweza,Kuvunja Katioba Ya Jamuhuri wa Muungano ya Tanzania ameweza.Kuwanyima wapinzani haki ya kwenda kutibiwa nje na kuwapa wa CCM haki ya kutibiwa nje ameweza.Kutugawa kwa itikadi ameweza pia

Very SAD, where do we make mistake?
 
alisema atatoa ajira utumishi wa umma baada ya miezi miwili..lakini hajatekeleza mpaka sasa ni miezi minne kasoro..sijui miezi miwili kwake anaihesabu vipi.?
 
Very SAD, where do we make mistake?

Kwa sababu tumekubali kugawanywa na watawala,mapka tutakapobadilika na kujiona kwamba sote ni watanzania.Na vibaraka ni watawala waliouza UHURU na RASLIMALI zetu kwa wakoloni aka wawekezaji
 
Wadau amani iwe kwenu.

Sina mengi sana,ila nawathibitishia tu kwamba;Mtaani sasa kuheshimiana kumerudi...

Zile kauli""unanijua mm nani""kwa sasa zimebaki historia.

Huyu mh.pia kajitahidi kipunguza sana gape la wenye nacho na wasionacho.

Hata maofisini sasa urasimu kama sii kuisha basi umepungua kwa kiasi kikubwa.

Kwenye mabar sasa hivi zile tabia za wape kama walivo hisikii tena.Ibebaki tu mhudumu anaitwa kwa ishara.

Aiseee!!!Huyu mzee noooma.
 
The fact that bar bado ziko wazi na watu wanaendelea kupiga maji means pesa bado zipo na rushwa iko pale pale magu kafeli
 
Katika vitu vya kijinga ambavyo watu tunashabikia ndio kama hicho!!
Huwezi furahia mtu fulani eti sasa hivi hali bata sasa ivi badala ya kuangalia wewe binafsi maisha yako yameborekaje.. .
Ndio kauli zilizopo mtaani sasa hivi eti heshima imerudi......kurudi kwake kwa hiyo heshima katika maisha ya kawaida umenufaika nini????
 
Ndio, ni lazima atishe kwa kuweza kuigeuza kanuni ya muumba inayowaruhusu viumbe kuishi hapa duniani sawa na malaika wa mbinguni kuishi kama mashetani! Anatisha kwa ubunifu na usimamizi.
 
Binafsi nimefurahishwa na kasi ya Dkt. Magufuli. Naamini wapo pia wengi wanaoungana nami katika furaha hii. Magufuli ameanza kwa kasi ambayo kama ataimaintain, Tanzania haimalizi miaka mitano itakuwa tayari ni nchi yenye kipato cha kati.

Hata hivyo wapo baadhi yetu ambao wanakejeli kasi hiyo. Hao kwangu ni watu waliozoea ubwete na bora liende!. Wanamwona Magufuli kuwa ni mtu atakayekuwa kauzibe kwao!

Wapigaji wote, wavivu wote na wazee Wa madili wote watamchukia Magufuli ila mi niseme na niwaombe tu kwamba tumpe support huyu jamaa kiukweli atatufikisha mahali Fulani!

Tuwafichue wote wanapanga kumhujumu (najua wanajulikana), tuwakatae kwani hawana nia njema na taifa letu.

PENGINE. Income ya Mtanzania hivi sasa ni dola 844 kwa mwaka au dola 1770 kwa kipimo cha PPP (Purchasing Power Parity)...lakini hata kuongeza dola 10 tu yataka kaaaazi kweli kweli!
 
Chamsingi kabisa mh rais asilegeze kamba yupo ktkt mstari mzuri, Akilegeza tu kamba kwa kelele za wachache basi atakua ameharibu.
 
Huu ni ukweli mchungu sana.

Najua tulizoeshwa na kuzoea vibaya.

Najua tuliaminishwa kuwa hii ni nguvu ya soda lakini ukweli haujifichi na unaendelea kujidhihirisha...

This is the MAN....
THE ONE AND ONLY MR PRESIDENT OUR PRESIDENT JPJM ...he is awesome!
 
Back
Top Bottom