Unaweza kujiuliza kwanini nimepongeza ila wengi mnaona utendaji wa kazi yake katika TAIFA hili kikubwa ni kumpatia ushirikiano kwa lengo lakupeleka TAIFA letu kwenye maziwa na hasari kauli mbiu ni hapa kazi tu ila tambua kwenye maisha ukifurahi kupongezwa pia kubali kukosolewa ili kujua wapi umekosea na nini kifanyike na andika haya sipo mwimili wowote ila na sifu na kupogeza mazuri yaliofanywa.
Pongezi kwa Mh. rais kwa kufufua shirika la ndege lililokufa kwa malengo ya watu wa chache ambao wanajinufaisha wenyewe kwa njama mbalimbali za kibiashara na zakisiasa kuna wengi wamezungumzia ndege hzi kwa kuziongerea vibaya Ila mkubwa walizoea kutuona tukikopa kwan wanafananisha na ndege za nchi nyingine na kuzungumzia mengne hapo mwanzo ilikuwa ngumu kukuelewa.
Ila now nimekuelewa watanzania wengi wanapenda makubwa kuliko uwezo wao Ila wanabidi watambue kuna mengi yakufanyika atuwezi kununua ndege za gharama kubwa na uendeshaji kwa gharama za juu wakati tuna mengi yakufanya swala zima la elimu bure madawati na uduma za afya nimefurahi kusikia tumenunua ndege hatujakopa na tutanunua zingne kwani ni pesa za watanzania, wengi wanapitisha chuki kwa wenye uelewa mdogo kwa sababu ya kukosa UDALALI, tumezoe kuona kila kitu kinachafaya na serikali kuna dalali ndani yake mpaka TCU pia kwenye maswala ya elimu kudaili wanafunzi kuna madalali dah Tazama hili mweshimiwa upigaji uwe mwisho mwaka huu.
KITU KINGINE KIKUBWA kwanini ukitaka kupata huduma mbovu tu nenda katika ofisi za serikali, nakumbuka kuna mbunge moja alizungumza hili msimu wa mwaka jana kama sijakosea, Tanzania kila kitu kinachofanyika unatengenezewa mazingira ya kutoa rushwa tu, mfano TRA kuchukua TIN namba tu unaweza chukua siku nzima, wakati ukimpa kishoka ni nusu saa tu au lisa, mtu anamua kutoa pesa yake ili kuokoa muda wake.
Tuboreshe huduma, huduma za serikali huko hospitali ndo hakuelezeki swala la dawa na madaktari ni tete, ila za binafsi huduma ziko vizuri pale ndo unapoona kila kitu serikali inahitajika kutoa tenda kwa watu wafanye kazi ambayo wao wameishindwa, mambo haya ndo yameleta madhara ya ESCROW kulipishwa shirika la umeme, kushindwa ubunifu kabisa kwani wasomi wa taifa hili wako wapi serikali kuwatumia hamuwezi au makampuni au mashirika binafsi tu ndio wanawatumia kwani yao yanapiga hatua kwani wafanyakazi wapi wanaonekana wabunifu na wako katika usimamizi mzuri kwanini, ila mifano tu kwani vitu vingi vinatokea ukiangalia katikati kuna udalali au mtu kapewa tenda.
Lengo ni kwamba tumefufua shirika la ndege na mmeamua kutoa mafunzo ya urubani Tanzania chini ya chuo cha usarifishaji, angalia shirika lisifirisike ataye firisi achukuliwa hatua kali,, wala sitemegemei kusikia kubinafishwa kwa kushindwa kwa serikali kuliendesha ni hatua kubwa sana tumeipiga ila tambua kuna mengi umetuhaidi na tunasubiri utekelezaji wako kasi yako ni nzuri nakupongeza kwa hilo.
Mh. hivi kwanini tukija kwenye swala la kimahakama sasa kwanini serikali yako hupoteza kesi za msingi hupelekea mpaka serikali kushindwa kesi na kupatia pesa za walipa kodi kutumika tu kiholela nina mashaka na hili hapo narudi tena kule juu sijui nini kifanyike hofu za watu zimerudi kimazoea.
Nakupongeza mh. rais kwa hatua kubwa ulifikia na ufanisi mzuri ulionao pia hongera kwa umoja na ushirikiano wako na pongezi zangu za dhati kabisa kwa uteuzi wako mzuri kwa vijana katika serikali yako kwani ni wabunifu na wachapaka kazi, mwisho niwape pole ndugu zetu wa Kagera kwa maafa walioyapata Mungu yu pamoja nao.
Mungu bariki Tanzania Mungu bariki Afrika