Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Kumbukumbu
2009 nilipata bahati ya kujiunga na chuo kikuu cha mtakatifu Augustine mwanza Tanzania..kwa masomo ya shadaha ya mahusiano ya umma na masoko.
2010 nikapata fursa ya kujiunga na ccm pale pale chuoni
mwaka 2011 nilichaguliwa kuwa kuwa mjumbe wa halmashauri kuu ya tawi kabarange Saut Mwanza moja ya changamoto tulizokutana nazo wakati ule kama chama ndani ya chuo ni idadi ndogo ya watu waliyokubali na kusapot ccm ndani ya chuo na maeneo mbali mbali ya mkoa wa mwanza, ilikuwa nijambo la kushangaza wasomi ukionekana unatosapoti kwa ccm, vijana waliyokuwa wakivaa sare za ccm ndani ya chuo walizomewa na kutengwa..2011 vijana wasiopungua wa tano au sita ndoo walikuwa na msimamo mkali wa ccm ikiwepo kuvaa hata sare adharani naweza kuwakumba kidogo
# Silvesta Yaled aliyekuwa mwenyekitinwa tawi
# Mohamed katibu
# Amani Nkulu
[HASHTAG]#Mdashiru[/HASHTAG] saidi
[HASHTAG]#Khalifa[/HASHTAG] mtambazi
N.k
Vijana hawa na wengine wachache niliyowasahau walifanya kazi kubwa ya kunyesha mlengo wa serikali kwa awamu ile kwa ugumu sana ilifikia hatua yakufanya mbinu mbadala mpaka baadhi ya vijana niliyowataja hapo juu kuingi kweye serikali ya wanafunzi SAUTSO nakumbuka Silvesta Yaled alikuwa waziri wa Mikopo na Naibu wake alikuwa Mdashiru Saidi, Amani Nkulu alikuwa waziri mambo ya nje.
Chuoni kulikuwa na upinzani mkubwa uliyokuwa ukipewa msimamo na Wenje,Mkosamali, badae Machali, visent Nyerere abaye hakuwa mwanafunzi pale na wengine niliyowasahau
VITU VIKUBWA VILIVYOKUWA VIKIFANYA CCM NA SERIKALI YAKE IPINGWE WAKATI ULE
1. Kucheleweshwa kwa mikopo
2. Mikopo kupewa wasiyostahiki
3. Migogoro ya wananchi kule mara kwenye migodi ya bulyagh'uru ambayo wanasiasa waliyokuwa wakitembelea chuoni wajengea hoja(zito kabwe)
4.ukosefu wa ajira
5. Ufisadi
6. Rushwa kwenye tasisi za umma
7. Ukikwaji wa katiba na sheria
8. Hali ngumu ya kipato mpaka kupelekea watoto kwenda shule
9. Ukosefu wa uhuduma za afya za uhakika
10. Uhaba wa nishati ya umeme
11. Upendeleo wa utoaji wa huduma katika ofisi za umma
12. Raia wenye fedha kuvunja sheria adharani
13. Mauwaji ya vikongwe na albino
N.k
Mambo haya na mengine mengi yalipigiwa kelele sana.
NYOTA NJEMA
2012 Tukahitimu masomo yetu wakati wa mahafari mgeni rasmi alikuwa Mh. Magufuli ambaye ndiye Rais wa awamu ya tano ya JMT.
Akitoa hotuba yake kama mgeni rasmi alisema hivi.
"Nchi hii inachangamoto nyingi ikiwemo ajira, nendeni mkaazishe makampuni jiunge vikundi kaazishe makampuni ya ukandarasi mimi kama waziri priority itakuwa kwenu wazawa..Nijifunza kitu kwake niliona ni mtu anayetaka watanzania na raia wake kunufahika na nchi yake.
Akimalizia hotuba yake mh.Magufuli alitoa shilingi Milioni Moja kwa wahiti na akasema watachagua chakuifanyia kama nikuongeza vinywaji hama soda but alisisitiza ataifatilia kama imefika kwa walengwa na imatumika ipasavyo...nijifunza kitu kingine kwake UFUTILIAJI na KUTIMIZA LENGO
Nilimnogoneza mwenzagu nafikiri Alikuwa Abdul Maheta kwamba " huyu jamaa akiwa Rais nchi itabadilika ghafla hatafuta unjinga wote tunaopambana nao kwajili ya kulinda chama hapa chuoni" Rafiki yangu alijibu neno moja sahihi.
Mungu sio Kimambi au Athumani miaka mitatu badae Mh. Magufuli amekuwa Rais wa Tanzania ndani ya miaka miwili tu katatua na meandelea kufanya hivyo kuondoa changamoto zote ambazo zilikiumiza chama chetu, leo hii wanaccm wanaona fahali na chama chao, wananchi tunaona fahali na nchi yetu.
Nataka nimwambie Mh. RAIS mungu amekutuma huyatekeleze hayo yanayorudisha faraja na tumaini kwa watu waliyowengi..faraja hii ndio iwe amani ya moyo wako..nakufanananisha na dhamani ya mwanga wa mshuma au kibatali kwenye giza nene..
Mwanga huu uwa nidhamani kubwa kuliko yowe za wanyama wakali katika giza nene.
Dhamani yako haitapote itaishi milele na zawadi hii upewe watu wachache ndani ya ulimwengu huu.
Songa baba..
Mungu anakulinda kutokana na faraja na dua zetu kwako na tupo wengi**
 
Kweli kabsa MKUU,RAIS MAGUFULI he is the best PRESIDENT EVER......Ninaanza kuona MAGUFULI kuendelea kuwa RAIS wa nchi hii kwa zaidi ya miaka kumi kwa SHINIKIZO LA WATANZANIA..... ni suala la MUDA tu
 
Mkuu, uandishi wako hauna urari na kiwango chako cha elimu ulichokisema. Tulia uandike jambo la maana kwa herufi sahihi. Kama posho utaipata tu Mkuu.
 
Sema yote mkuu siku ile ya graduation alivyoanza kutaja takwimu zake nini kilimpata hadi Dr. Kitima akatuliza upepo?? Sema pia Dr. Kitima alimkabidhi nini ili asome na wafanyie kazi na je ameyafanyia kazi?? Kabla sijaenda kwenye kukubalika na kutokukubalika kwa CCM tawi la Kambarage SAUT mkiwa na ofisi yenu pale Nyamalango na mbinu chafu zote!
 
tutampima kwa matokeo kama vifaa vya kutosha mahospitalini, madawa ya kutosha, wafanyakazi wa kutosha hasa elimu na afya, vitendea kazi vya kutosha mashuleni, wanafunzi wenye sifa elimu ya juu wote wanapata mikopo, barabara nzuri, maji salama, umeme wa uhakika, uchumi wa mtu mmoja mmoja umekua n.k hatutampima kwa ziara maofisini
Kwa kazi hii hayo yote tutayapata tu.
 
Hiyo speed ni ipi? Biashara zinafungwa hali ya wakulima ni hoi, maisha ni magumu kila kona.

Kama mheshimiwa wetu anafanya vizuri kwa nini hataki kukosolewa?
 
Rais wetu Ni Rais mzuri Sana ambaye hayupo ktk kizazi cha sasa na wala hakuna wamfano wake kwa sasa Africa na uwenda hata duniani.

Kiukweli kabisa pasipo kumumunya mim naweza kusema wachache ambao walijivika umungu watu nakuifaidi national cake ndio wanatuvuruga maana walinunua watu na makanisa na misikiti. Sio jambo lakushangaza haya tunayaona sasa ni kaz yakundi dogo lawatu walivuna pasipo jasho ama kupanda. Wao walikula kwa jasho la masikini uku wakitua adaa kwa peremende na karanga.

Kiukweli kabisa wengi hwashangai drama zinachezwa na vyama fulan vya siasa na taasisi za dini. Yote haya yalipangwa na sasa wanatekeleza walichopanga hakuna jipya. End

Ndugu zangu watanzania kama huyu Rais angekuwa sio mwaminifu na mlinda masilahi yawakubwa nikiongoz kweli anaichukia rushwa kweli toka moyoni nawala hatanii. Ni Rais kweli ameapa kuitokomeza rushwa nankweli atafanikiwa. Ni Rais kwel ameapa mbele za Mungu hatokula rushwa wala pokea na Mungu wake kweli amsaidie.

Tunamchukua poa ila kweli hatanii na kweli hana huruma na majizi. Huyu ndio Mh Dr Magufuli ninaye mjuwa.
Wengi tunafikiri serikali yake ina undugu ama masilahi na mtu ila nawaambia hana na kamwe hatokuwa nao.

Muda ni mwalimu mzuri wakati unakuja mtamvisha taji za heshima na wengi mtamtaka arudi kuwa Rais nakujutia dhihaka mnamfanyia.

Mungu hawezi kuacha dhihaka hizi zipite salama wakati unakuja atatujibu kama kweli vile yuna mbrand kiongozi wetu ni swa ama laa.
Shime Rais wangu Magufuli
 
Hahahahahaaaaa.
Nimesoma tu hii aya nimeacha

''Rais wetu Ni Rais mzuri Sana ambaye hayupo ktk kizazi cha sasa na wala hakuna wamfano wake kwa sasa Africa na uwenda hata duniani."
 
Back
Top Bottom