Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Record ya mauaji, kejeli, udicteta, ufisadi, ubaguzi, ukanda au record gani?

Tueleweshe tafadhali!
 
Watanzania daini katiba mpya na tume huru CCM itoke vinginevyo mtapata tabu Sana
 
Hiyo namba (1) hebu mtuweke list ya viwanda basi tuvijue ....au ndy mafundi cherehani nao inahesabika viwanda,We mashine za kutengeneza juisi za miwa nayo viwanda,wenye blenda majumbani nazo viwanda hebu tuwekeni Sawa Kuhusu Hizo viwanda wana lumumbaaa

Ova

Kiwanda cha juice ya miwa ni sawa na kiwanda kinachotengeneza Azam mango juice!
 
Nilivosoma heading ikanifanya niingie kwenye content ila nilivosoma hoja yako ya kwanza nikawa nimeuona upeo wako WA kufikiri unapoishia,,,,,,,,pole sana
 
Hayo ni malengo yake ambayo hajayatimiza na vigumu kuyatimiza hata baba wa taifa JKNyerere alikuwa na fikra pana zenye maslahi na Taifa sana tena sanaaa. Alitaifisha Viwanda,Mabenki,Majumba,Mashamba,Mashule na kila kitu chenye uchumi wa juu alitaifisha na kutukabidhi zikawa ni mali zetu ila mwishowe nch ikatushindaaa chaliii nyan'ganyang'a ndembemdembeee taabaaaani tukajipiga kipigo cha mbwa kokooo. Hata JPM anajitahidi lakini kama tulivyo rushwa imetujaa vichwani ulafo wa mali na ufisadi na uzembe uliokitihri hatafika
Baadhi ya mambo yanakwamishwa na mbwa koko lakini tutashinda
 
Uko sahihi!!!
Atakumbukwa kwa kujenga miundombinu muhimu kama Wakoloni waliomtangulia, yaani Wajerumani na Waingereza. Wakoloni hao walijenga RELI toka Dar es Salaam kwenda Kigoma, Mwanza, Tanga, Arusha mpaka Voi, nchini Kenya.
Wakoloni walijenga RELI toka Mtwara mpaka Nachingwea.
Lakini Wakoloni hao hao walitunyima UHURU wa kuamua mambo yetu wenyewe!!!!
Pamoja na yote waliyofanya, tuliona kuwa bora tuwe masikini lakini TUKIWA HURU!!
Wapinga UKOLONI, akiwemo BABA WA TAIFA, walikamatwa na POLISI na kupelekwa mahakamani.
Baba wa Taifa na wenzake walinyanyaswa sana lakini hatimaye tukapata UHURU.
Hakika, Rais Magufuli anao uhuru wa kuamua jinsi anavyotaka Watanzania wamkumbuke!
Kwa mwenendo wake wa sasa, tutamkumbuka kwa kujenga Reli ya Kisasa, SGR, kwa kujenga Stiglers Godge, kwa kujenga fly-overs, kwa kujenga makao makuu.
TUTAMKUMBUKA KAMA TUNAVYOWAKUMBUKA WAKOLONI WALIOTUJENGEA RELI NA MELI YA MV LIEMBA!!!!!!!

Mbowe utamkumbuka kwa lipi!
 
listi ya vi
Hiyo namba (1) hebu mtuweke list ya viwanda basi tuvijue ....au ndy mafundi cherehani nao inahesabika viwanda,We mashine za kutengeneza juisi za miwa nayo viwanda,wenye blenda majumbani nazo viwanda hebu tuwekeni Sawa Kuhusu Hizo viwanda wana lumumbaaa

Ova
listi ya viwanda ni kubwa kwa hapa haitatosha, maaana ww ukiwa na printer moja na computer nyingi kiwanda. ukiwa na jiko la kuchomea chipsi ni kiwanda, mama ntilie ni kiwanda na hata kinyozi ni kiwanda

utaorordhesha wangapi

kwa kweli Magufuli ni Rais ataewacha historia hilo halina ubishi ila sijui historia itakua in positive or negative? time will tell
 
listi ya vi

listi ya viwanda ni kubwa kwa hapa haitatosha, maaana ww ukiwa na printer moja na computer nyingi kiwanda. ukiwa na jiko la kuchomea chipsi ni kiwanda, mama ntilie ni kiwanda na hata kinyozi ni kiwanda,marekani,jpan ujerumani etc wote hawatuwezi pongezi nyingi zimuende uncle magu aise


utaorordhesha wangapi

kwa kweli Magufuli ni Rais ataewacha historia hilo halina ubishi ila sijui historia itakua in positive or negative? time will tell
Mkuu basi tuko vzuri kwa viwanda....naona mpk sahv dunia tunaongoza kwa viwanda

Ova
 
Huu ni utaahira uliopitiliza, Jamani mnamtia rais aibu kwa sifa za kijinga,
Kwani ni Rais gani ktk Africa asiyefanya aya?
Aya ni mambo ya kawaida na ni wajibu wa rais kuyafanya maana analipwa km mwajiriwa yoyote yule,taja kitu unique alichofanya hata kukumbukwa nje ya uliyotaja
Kiufupi sana Mhe Magufuli ni mwafrika wa kipekee mwenye madaraka ya urais anaye waza tofauti sana na marais n.a. raia wengi wa Africa.

Mtu huyu anaenda kuweka rekodi ya kipekee kabisaa ktk mambo yafuatayo:-

1. Kuitoa TZ daraja la chini kwenda la kati kiuchumi KWA ujenzi wa viwanda na biashara zenye uwazi n.a. manufaa KWA taifa pasipo unyonyaji KWA wazawa. Hii itaongeza ajira nchini miaka michache ijayo.

2. Kuweka nidhamu ya kazi na kuongeza ufanisi ktk utumishi wa umma.

3. Kujenga n.a. kuboresha miundombinu mikubwa ya usafiri n.a. uzalishaji umeme nchini.

4. Kuboresha huduma za afya, elimu n.a. maji nchini.

5. Kupunguza matumizi yasiyo n.a. tija serikalini na kuokoa fedha za walipa kodi KWA ujenzi wa taifa

6. Kutimiza ndoto ya kuhamisha makao makuu ya serikali kuwa dodoma.

Kwa haya machache mhe rais wetu amejitofautisha sana na viongozi wengine afrika

Mungu mbariki sana rais wetu mpendwa mpe afya na maisha marefu.

Hata Yesu wa Nazareth alipingwa na baadaye kuuwawa sembuse wewe.

Piga kazi mkuu wabaya mwisho wao huwa ni kuambulia aibu.
 
Wadau
Serikali ya JPM imethibitisha ubora wake kwa kutoa Tshs Bilioni 23 kila mwezi Kugharamia Elimu Bure kwa Watanzania nchi nzima.
Hiyo ni sehemu tu ya mambo mengi makubwa na mazuri yanayofanywa na Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli Mzalendo nambari moja na Kiboko ya Mafisadi
Viva JPM
Viva CCM
 
Tangu Uhuru Tulikua Na Hospitali Za Wilaya 77.
Kwa Miaka 2 Na Nusu Ya Rais Dkt Magufuli Ametoa Tsh Bilioni 105 Kwajili Ya Hospitali Za Wilaya 67 Zinajengwa.
Kati Ya Vituo Vya Afya 517,Vituo 115 tu Ndio Vilikua Vinatoa Huduma Za Upasuaji.
Kwa Miaka 2 Na Nusu Ya Dkt Magufuli Vituo Vya Afya 208 Vinawezeshwa Kufanya Upasuaji.
Hongera Sana Kwa Serikali Ya Serikali Ya Awamu Ya Tano.
IMG-20180502-WA0047.jpg
IMG-20180502-WA0064.jpg
 
Ngoja na mimi nijitahidi kureply kilumumba,niupate u-DC.

Kweli haya ni maajabu,hongera sana rais wetu,wewe ni mkombozi wetu tangu kuumbwa kwa Tanzania. Unatenda maajabu nami siwezi kueleza,ni nani kama wewe rais wetu?ni nani? Tumepata jembe,tunakuunga mkono!
 
Back
Top Bottom