Mimi bado Niko shuleni KUHUSU uongozi wa raisi wangu ndugu JPM. Kila siku najaribu kumtafakari. Katika kumtafakari kwangu yapo mambo niliyoandika, haya yanahusiana na hapa Mbeya mji ninaoishi.
1. Tangu HUYU mheshimiwa aingie madakani ninaona wamachinga walivyohuru kutembea bidhaa zao, migambo hawawasumbui tena. Nakumbuka miaka ya nyuma Akina mama wanaotembeza bidhaa walikuwa kutwa kucha ni kukimbizana na migambo wa jiji utafiri sio watanzania.
2. Jiji la Mbeya lilikuwa ni kuunguruma majenereta ya UMEME kila duka, sababu ya umeme kukatika katika. Leo hii hili suala limekuwa historia. Nafikiri hata biashara ya majenereta imeshuka maana siioni tena. Na sidhani kama amefanya lolote jipya ZAIDI kudhibiti mifumo fulani fulani huko juu.
3. Madawa ya kulevya yalikuwa ya kawaida hapa kwetu. VIJANA waliharibika mno na wengi nawaona wakifuata matibabu hapa hospitali ya rufaa. Leo hii hali naona haipo.
MAGUFULI ANAWEZA kuwa na madhaifu yake lakini nikitazama haya mambo ninaiona NURU kiasi ikiangaza. Mungu IBARIKI TANZANIA.
Mimi si mpenzi wa CHAMA chochote cha siasa.