Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Habari wakuu,

Kama tuna kumbukumbu kidogo miaka ya nyuma tatizo la mgao wa umeme lilikuwa kama kansa inayoitafuna nchi hii nchi ilikuwa haimalizi mwaka bila kuwa na mgao wa umeme mara maji Mtera yamepungua mara hivi mara vile yani zilikuwa sarakasi zisizokuwa na mwisho kiasi cha kwamba wajanja wacheche walijinufaisha kupitia tatizo la upungufu wa umeme.

Tumeshuhudia mikataba mingi mibovu iliyoitikisa nchi na kulitia taifa aibu na hasara ya hali ya juu. Tumeshuhudia mikataba kama Richmond na Escrow ikiingizia taifa hasara kubwa sana na kusababisha baadhi ya mafisadi kama mzee lowassa kujiudhulu na baadae kukimbilia katika CHADEMA baada ya kutambua hakuna nafasi ya madudu chini ya mh rais Magufuli.

Tangu utawala wa awamu ya tano uingie madarakani zaidi ya miaka mitatu nyuma, suala la mgao wa umeme limekuwa historia.

Mh. Rais amejitahidi sana kumaliza tatizo hili hivyo kupelekea kuleta unafuu kwa viwanda ambavyo viilikuwa vinatumia gharama kubwa kuzalisha umeme kwa kutumia mafuta pia kuwaondolea hasara waliokuwa wanapata wafanyabiasha ndogo ndogo kama mabutcher, wauzaji wa soft drink pamoja na wamama wauza mabarafu na ice cream.

Vijana na wananchi wengi tunakubali sana utendaji wa mh Rais hatuyumbishwi na wazurulaji watanzania tunataka maendeleo
Mgao upi ukliomalizwa? Wa kutangazwa au wa kimya kimya?
 
Back
Top Bottom